Skip to main content
RadioRahma

RadioRahma

By radiorahma

Tutakuwa tunaweka makala ya mada mbali mbali katika mtandao wetu wa podcast yetu. Karibu sana
Available on
Apple Podcasts Logo
Google Podcasts Logo
Overcast Logo
Pocket Casts Logo
RadioPublic Logo
Spotify Logo
Currently playing episode

Unyanyasaji wa wanawake walio na matatizo ya akili.

RadioRahmaDec 30, 2021

00:00
13:48
STORY YANGU NA MWENYE UMAR SHARIFF

STORY YANGU NA MWENYE UMAR SHARIFF

story yangu na Mwenye Umari
Nov 27, 202341:29
STORY YANGU NA MOHAMMAD ABBAS

STORY YANGU NA MOHAMMAD ABBAS

Story Yangu
Nov 13, 202335:04
STORY YANGU NA SALIM MOHAMMED

STORY YANGU NA SALIM MOHAMMED

Professional diver
Oct 10, 202349:56
STORY YANGU MOHAMMED THABIT

STORY YANGU MOHAMMED THABIT

Kisa cha Ferry ya Mtongwe Kuzama
Sep 30, 202335:04
STORY YANGU NA SWALEH YAHYA

STORY YANGU NA SWALEH YAHYA

Vile Mwanabaharia Swaleh Yahya alipata kisanga akiwa baharini na ndugi yake na Mtalii
Sep 19, 202330:33
STORY YANGU NA MURAD SWALEH

STORY YANGU NA MURAD SWALEH

Vile kijana Murad Swaleh aliingilia Dawa za Kulevya tokea utotoni na kueza kujitoa baadae
Sep 13, 202350:44
STORY YANGU NA CHARITY CHIGULU

STORY YANGU NA CHARITY CHIGULU

Vile Mwanahabari alipoteza macho yake kwa ugonjwa unaoitwa Glaucoma
Sep 08, 202327:18
Nipe Sanitary pads na miti nikupe chupa za plastiki tukabili climate change

Nipe Sanitary pads na miti nikupe chupa za plastiki tukabili climate change

Utunzaji wa mazingira umekua changamoto kubwa sana kote ulimwenguni kwani mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri vigezo vingi katika jamii ikiwemo afya, hewa safi, maji safi ya kunywa,chakula na makazi salama.

Kufuatia hali hio wanafunzi katika shule ya Salex Transition Academy iliyoko eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa wamejitosa katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi,kwa kutumia mbinu ya kubadilishana chupa za plastiki kwa sodo,miti na vifaa vingine vya masomo.

Fatuma Hamisi mwenye umri wa miaka 13 ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Salex Transition Academy.Yeye ni mwanafunzi wa gredi ya 6 na  pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira katika shule hiyo.

Mwandishi:Athuman Luchi

Aug 08, 202308:52
WANAWAKE WATUMIA TEKNOLOGIA KUJIIMARISHA KIUCHUMI

WANAWAKE WATUMIA TEKNOLOGIA KUJIIMARISHA KIUCHUMI

Licha ya idadi ya wanawake katika taalum ya teknologia kuwa ndogo ikilinganishwa na idadi ya wanaume, wanawake wameonekana kupambana ili kukabiliana na tofauti hiyo.

Ripoti kutoka benki kuu ya dunia inaonyesha kuwa wanawake wako chini ya thuluthi moja ya wafanyikazi ulimwenguni katika nyanja zinazohusiana na teknolojia.

Ambapo wanashikilia asilimia 28 ya kazi zote za kompyuta na hisabati, na asilimia15.9 ya kazi za uhandisi na usanifu

Mwandishi:Nuru Mwalimu

Aug 07, 202312:02
Mtiririko wa taka baharini, tishio la kuangamia kwa viumbe vya bahari

Mtiririko wa taka baharini, tishio la kuangamia kwa viumbe vya bahari

Makala haya yanazungumzia kuhusu uchafuzi wa bahari hasa katika eneo la Mbuyuni-Mji wa Kale kaunti ya Mombasa.

Eneo hilo limeathirika na maji taka yanayotoka katika nyumba zinazopakana na ufuo wa bahari.Makala haya yametayarishwa na Ruth Keah.

May 15, 202312:58
Challenges of teenage pregnancy facing girls with mental disability.

Challenges of teenage pregnancy facing girls with mental disability.

17-year-old Jane is among the children with mental disabilities who were molested and impregnated. Jane is currently raising a three-month-old baby boy.

By Rose Tawa.

Apr 25, 202308:23
Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change

Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change

Mabadiliko ya Tabia Nchi yameathiri sana wakulima na wafugaji hatua inayo wafanya wengi kukumbwa na tatizo la afya ya Akili.Kufuatia hatua hio sasa baadhi ya wakulima wanajizatiti kukabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na mabadiliko hayo.Sasa wakulima hao,wamejitosa katika ufugaji wa nyuki na vipepeo,huku wengine wakifanya biashara ndogo ndogo za kukimu mahitaji ya familia.

Athuman Luchi,ametuandalia makala hayo aliyoyapa jina la Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change

Apr 03, 202304:40
Kumaliza Dhulma za Mtandao Hatua kwa Hatua

Kumaliza Dhulma za Mtandao Hatua kwa Hatua

Makala haya yanazungumzia kuhusu hatua ambazo zimepigwa na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa dhulma za mtandaoni zinaripotiwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Yametayarishwa na Ruth Keah.

Mar 17, 202310:54
Ujangili wa viumbe vya baharini

Ujangili wa viumbe vya baharini

Makala haya yanazungumzia kuhusu ujangili unaofanyiwa viumbe vya baharini. Yametayarishwa na Ruth Keah.

Mar 09, 202309:21
Teknolojia ya Rangi Katika Kukabiliana na Uhalifu Mombasa

Teknolojia ya Rangi Katika Kukabiliana na Uhalifu Mombasa

Makala haya yanazungumzia kuhusu mbinu ya Rangi ambayo wanabodaboda kaunti ya Mombasa wanatumia kutofautisha sehemu wanazohudumu kama njia moja ya kukabiliana na visa vya uhalifu. Makala yametayarishwa na Ruth Keah.

Mar 07, 202311:13
Ushirikiano unavyosaidia kupambana na mbinu za uvuvi haramu Shimoni-Kwale.

Ushirikiano unavyosaidia kupambana na mbinu za uvuvi haramu Shimoni-Kwale.

Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi za mashirika mbalimbali ambayo yamekuja pamoja kukabiliana na uvuvi wa kutumia mbinu haramu katika eneo la Shimoni Kwale. Yametayarishwa na Ruth Keah.

Mar 06, 202315:56
Mti Wa Kukabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi Katika Kila Boma.

Mti Wa Kukabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi Katika Kila Boma.

Ukataji wa miti kiholela umesababisha mabadiliko ya tabianchi,kiangazi,mmomonyoko wa udongo,mafuriko na ongezeko la hewa chafu hatua inayochangia athari mbali mbali kwa jamii.

Kufuatia mabadiliko hayo ya tabia nchi,sasa jamii imejitokeza kuja na mbinu mbali mbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Makundi ya wanawake na vijana katika kaunti ya kwale yanaendeleza mpango wa upanzi wa miti,walioupa jina la Mti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kila boma.

By Rose Tawa.

Mar 02, 202308:09
Uhifadhi Wa Mazingira Umesababisha Kujengwa Kwa Mkahawa Unaovutia Watalii Dabaso.

Uhifadhi Wa Mazingira Umesababisha Kujengwa Kwa Mkahawa Unaovutia Watalii Dabaso.

Makala haya yanazungumzia kuhusu jamii ilivyoungana kulinda mazingira hasa mikoko katika eneo la Mida Creek Dabaso. Hatua iliyowafanya kujenga mkahawa juu juu ya mikoko na kwasasa mkahawa huo umekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka humu nchini na hata nje ya nchi. Mtayarishi ni Ruth Keah.

Mar 02, 202313:13
Watu wenye ulemavu wanavyokabili climate change

Watu wenye ulemavu wanavyokabili climate change

Mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuathiri kila mtu kila siku,kufuatia hayo watu wenye ulemavu wamejikita katika mbinu mbali mbali za kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi jijini Mombasa.Mwanahabri wetu Nuru Mwalimu ametuandalia makala yanayosimulia juhudi za watu wenye ulemavu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mar 01, 202306:04
Wanahabari wa Radio Wanavyopambana na ongezeko la habari za Kupotosha

Wanahabari wa Radio Wanavyopambana na ongezeko la habari za Kupotosha

Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi mbalimbali ambazo wanahabari wa Radio wanafanya kuhakikisha kuwa habari wanazopeperusha hewani ni za uhakika. Yametayarishwa na Ruth Keah

Feb 13, 202311:08
Soka inavyotumika kukabili mimba za mapema Kilifi

Soka inavyotumika kukabili mimba za mapema Kilifi

Kaunti ya Kilifi katika miaka ya hivi karibuni imetajwa kuwa Moja wapo ya kaunti zinazoongoza Kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba za mapema nchini.

Takwimu kutoka kwa mfumo wa taarifa za afya nchini yaani Kenya Health Information System zikionyesha kuwa jumla ya wasichana 4,909 walio na umri wa kati ya miaka 15-18 walipata mimba katika kipindi Cha mwezi Januari Hadi Agosti Mwaka 2021.

Na kama anavyosimulia Ali Mwalimu kwenye makala haya, mashirika mbalimbali kaunti ya Kilifi yamejitokeza kukabiliana na tatizo hilo.

Feb 04, 202315:00
Kifafa Siyo Uchawi

Kifafa Siyo Uchawi

Kifafa ni ugonjwa wa ubongo unaosababisha mtu kupoteza fahamu kwa muda.

Ugonjwa huu unaweza kumsababishia mtu kufanya vitendo visivyokuwa vya kawaida kama vile kuanguka, kufifitika na hata baadhi ya wagonjwa kutojielewa.

Kulingana na takwimu kutoka kwa shirika la afya dunia WHO, takriban watu milioni 50 duniani wanaugua maradhi haya, na kuyafanya kuwa miongoni mwa maradhi maarufu zaidi ya ubongo duniani.

Jan 31, 202303:10
Uji Wa Chekechea

Uji Wa Chekechea

Makala haya kuhusu Uji wa chekechea yametayarishwa na Baya Kitsao.

Jan 27, 202302:32
Saratani Ya Matiti Sio Kifo, Inatibika.

Saratani Ya Matiti Sio Kifo, Inatibika.

Idadi kubwa ya wanawake wenye saratani ya matiti maeneo ya vijijini wamezongwa na kasumba kwamba saratani ya matiti ni kifo na sio rahisi kwa mgonjwa kupona.

Ili kufutilia mbali kasumba kuwa saratani ya matiti ni kifo,nilifanikiwa kufanya mahojiano na Anna Nyambura ambaye alipona saratani ya matiti baada ya kupata matibabu humu nchini pamoja na Daktari Riyaz Kasmani ambaye ni mtaalamu wa ungojwa wa saratani.

Mwandishi: Rose Tawa.

Jan 17, 202312:01
Habari ghushi kuhusu corona

Habari ghushi kuhusu corona

Makala ya habari ghushi kuhusu Corona ambazo zilikuwa zikisambaa kuwa madaktari wa kienyeji walikuwa wakitibu virusi vya Corona. Imetayarishwa na Baya Kitsao.

Jan 11, 202305:11
Dosari Ya Shilingi katika kaunti ya Mombasa

Dosari Ya Shilingi katika kaunti ya Mombasa

Makala ya Dosari Ya Shilingi yalioandaliwa na Oscar Ochieng yanahusu madeni katika kaunti ya Mombasa. Makala haya yanazamia sababu zinazopelekea kaunti hii kushuhudia madeni ya kiwango cha juu ndani ya miaka mitano ya kifedha iliyopita wakati ambapo utawala wa sasa umeunda jopo kung'amua ukweli kuhusu madeni hayo.

Dec 29, 202210:07
Wanawake wakumbatia kilimo cha agrivoltaics kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Wanawake wakumbatia kilimo cha agrivoltaics kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Hali ya kiangazi na mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kukumba sehemu mbali mbali humu nchini, hivyo basi inasababisha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mazao ya chakula.Hali hii imeathiri mapato na kupanda kwa bei za vyakula.

Katika kutafuta suluhu zinazowezekana kukabili hali hii, kikundi cha wanawake wakulima kutoka eneo la Lunga Lunga,walianzisha mradi unaoitwa "agrivoltaics,"yaani kutumia paneli za jua katika ukulima ambao husaidia kukabiliana na hali ya ukame unaozidi kuongezeka.

Dec 25, 202209:03
Malkia wa Gasi

Malkia wa Gasi

Kwa mara nyingi sekta ya usambazaji wa gasi safi imechukuliwa kama kazi inayofanywa na wanaume. Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake kutoka kaunti ya Mombasa waliojiingiza katika sekta hiyo na kujipatia kipato na kuimarisha maisha yao. Mtayarishi wa makala haya ni Ruth Keah.

Dec 22, 202215:35
Changamoto za mimba za utotoni kwa wasichana wenye matatizo ya akili

Changamoto za mimba za utotoni kwa wasichana wenye matatizo ya akili

Wizara ya afya nchini Kenya ilirekodi visa 45,724 vya mimba za utotoni mnamo Januari na Februari mwaka 2022.Visa hivyo ni vya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 19 wakiwemo watoto wenye ulemavu wa akili.Watoto hao wenye ulemavu wengi ubakwa na kupachikwa mimba na kuachwa wakiangaika pasi usaidizi.

Mwandishil:Rose Tawa

Dec 05, 202208:14
Mwelekeo Kwa wajane waliodhulumiwa

Mwelekeo Kwa wajane waliodhulumiwa

Licha ya kuwa na haki ya urithi pindi mwanawake anapofiliwa na mumewe, jamii imekua tishio kubwa kwa kina mama pindi wanapofiliwa kutona na mila na desturi potofu katika jamii huku takwimu nchini zikionesha kuwa takriban wajane milioni 8 nchini wametelekezwa kutokana na mila potofu na umaskini.

Mwandish:  Nuru Mwalim.

Nov 25, 202221:32
Kaa La Wanawake

Kaa La Wanawake

Makala haya yanahusu wanawake wanaopata mafunzo ya kujikimu kimaisha wakati ambapo suala la ajira limekuwa changamoto nchini. Kando na kujikimu ki maisha, mafunzo wanayopata vile vile yanalenga kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Nov 22, 202216:59
Kilimo Baharini/Part 2

Kilimo Baharini/Part 2

Wakazi wengi ukanda wa pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu.

Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye makala ifuatayo.

Nov 10, 202211:19
Kilimo Baharini/Part 1

Kilimo Baharini/Part 1

Wakazi wengi ukanda wa Pwani wamekuwa wakitegemea kilimo cha nchi kavu.

Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha hali ya ukame kukithiri, Sasa baadhi yao hasa wanawake wamegeukia kilimo mbadala cha baharini kama anavyoeleza Ruth Keah  kwenye makala ifuatayo.

Nov 10, 202210:50
Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 2

Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 2

Kina mama wanaolea Watoto walio na maradhi ya kichwa maji (hydrocephalus) na mgongo wazi (Spinabifida) hupitia changamoto chungu nzima ikiwemo kutelekezwa na waume zao.

Hata hivyo chakutia moyo hapa ni kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaume ambao wameanza kuwa na ufahamu kuhusu magonjwa hayo,

Na wanasaidia wazazi wa kike kuwapeleka Watoto hao hospitalini kwa matibabu, na mazoezi.

Kama anavyoeleza Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.

Nov 08, 202208:48
Wazazi wakiume waanza kukumbatia ulezi wa watoto walio na Maradhi yanayosababisha ulemavu/Part 1

Nov 08, 202207:50
Ahudumia jamii licha ya changamoto ya kuona

Ahudumia jamii licha ya changamoto ya kuona

Kila mwaka Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ni maalumu kwa kuelimisha jamii kuhusu ulemavu wa kuona, athari zake na njia za kuzuia matatizo ya macho.

Mwaka huu,siku hiyo iliadhimishwa tarehe 13 mwezi wa Oktoba. Makala haya ambayo yametayarishwa na Ruth Keah, yanazungumzia kuhusu mwanamke ambaye ana changamoto ya kuona lakini amepuuza changamoto hiyo na anahudumia jamii kwa njia mbalimbali.

Oct 31, 202207:50
Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part Two

Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part Two

Makala haya yanazungumzia kuhusu jinsi idara ya afya gatuzi dogo la Rabai kaunti ya Kilifi ilivyoweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa homa ya Chikungunya.

Hii ni baada ya homa hiyo kuripotiwa kaunti jirani ya Mombasa.

Imetayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Oct 21, 202210:51
Hamasa zilivyosaidia wakazi wa Rabai-Kilifi kuepuka homa ya Chikungunya - Part One

Oct 21, 202207:58
Mradi wa Skills Mtaani waboresha elimu kwa Vijana Mombasa

Mradi wa Skills Mtaani waboresha elimu kwa Vijana Mombasa

Tangu ya kuanzishwa kwa Mradi wa Skills Mtaani eneo bunge la Mvita zaidi ya Vijana 11,000 wamenufaika na mradi huo na sasa wengine wameajiriwa na wengine wamefungua biashra zao.

Mwanahabari wetu Athuman Luchi ametuandalia makala,kuhusu mradi huo.

Oct 21, 202213:07
Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part Two

Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part Two

Makala haya yanazungumzia kuhusu wanawake katika Kijiji cha Kibokoni kinachopatikana na bahari kaunti ya Kilifi waliokuwa wakikata miti na kuuza kuni.

Wanawake hao sasa wamebadilika, kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa samaki vidimbwini na kuuza ili kujikimu kimaisha.

Makala haya yametayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Oct 21, 202209:58
Wanawake wafaidika na ufugaji wa Samaki vidimbwini Kibokoni Kilifi - Part One

Oct 21, 202207:54
Uhifadhi wa Mikoko kupitia ufugaji wa Nyuki

Uhifadhi wa Mikoko kupitia ufugaji wa Nyuki

Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi ambazo wakazi wa Kijiji cha Ganahola, eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanafanya kulinda mikoko baharini.

Wakazi hao wanafanya ufugaji wa nyuki ambao hutoa ulinzi kwa mikoko eneo la Tudor Creek hiyo saa 24/7 hivyo hakuna watu wanaweza kuiharibu.

Imatayarishwa na kusimuliwa na Ruth Keah.

Oct 21, 202211:07
Kijana anayesakata soka ya kimataifa licha ya ulemavu wake

Kijana anayesakata soka ya kimataifa licha ya ulemavu wake

Makala haya yanaangazia juhudi za kijana kutoka kaunti ya Kilifi-Kenya anayeng'aa katika soka ya kimataifa licha ya kuwa mlemavu. Licha ya kukatazwa kucheza na wazazi wake, hakufa moyo na kuendeleza kipaji chake na kwasasa anategemewa na familia yake kutokana na kipato anachopata kutokana na kucheza soka.

Oct 13, 202211:59
Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part Two

Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part Two

Kijiji cha Jimba, wadi ya Ruruma eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi, ni kijiji ambacho kimetegemea sana ukulima kama njia ya kujipatia riziki.

Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za kilimo zimepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo basi kupelekea jamii nyingi katika kijiji hicho kuishi katika hali ya chini ya Maisha na kushindwa kujiendeleza kimasomo.

Lakini kuna matumaini ya tatizo hilo kuzikwa katika kaburi la sahau kupitia mchezo upendwao na wengi wa soka.

Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.

Oct 10, 202207:32
Wasichana waendeleza elimu kupitia mchezo wa soka Rabai Part One.

Oct 10, 202210:07
Chupa zageuzwa kuwa mazalia ya Samaki baharini.

Chupa zageuzwa kuwa mazalia ya Samaki baharini.

Mirundiko ya takataka sio tu katika nchi kavu bali pia baharini kwa miaka mingi imekuwa shida kubwa kuthibiti, taka za baharini zikichangia kuharibika kwa miamba ya matumbawe.

Lakini katika Kijiji cha Mkwiro kaunti ya Kwale Ukanda wa pwani, baadhi ya taka za baharini na zile za nchi kavu zimegeuzwa kuwa thamani kwa kutumia mchakato mbadala wa kutengeneza chupa za matumbawe.

Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala yafuatayo.

Oct 10, 202211:33
Kukomesha Unyanyapaa na Ubaguzi kwa wanaokabiliwa na tatizo la Afya ya Akili

Kukomesha Unyanyapaa na Ubaguzi kwa wanaokabiliwa na tatizo la Afya ya Akili

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu nchini Kenya asilimia 0.3% ya watu wanaugua ulemavu wa akili jijini Mombasa.

Wengi wa wenye ulemavu wa akili ukumbwa na unyanyapa,msongo wa mawazo na utengwa katika jamii,hivyo wanajipata wakirandaranda mitaani.

Juma Ali ni kijana mwenye umri wa miaka 30, aliyepona matatizo ya akili yaliyomsumbua kwa muda wa miaka 5.

Anasema alianza kurukwa na akili baada ya kumpoteza mchumba wake katika ajali ya barabarani.Anataja kifo hicho kilimfanya kukabwa na msongo wa mawazo na kuanza kutembea uchi na kushambulia watu.

Mwandishi:Athuman Luchi.

Oct 10, 202208:46
Kilio cha mtoto mwenye ulemavu wa akili aliyebakwa na kupachikwa mimba

Kilio cha mtoto mwenye ulemavu wa akili aliyebakwa na kupachikwa mimba

Watoto wengi wenye matatizo ya akili upitia unyanyasaji wa kingono,kupachikwa ujauzito na wengi wa wanao bakwa usalia kimya wasijue wapi pa kuripoti kisa hicho,Mariam mwenye umri wa miaka 16 ni kati ya watoto wenye ulemavu wa akili walionajisiwa na kupachikwa mimba.

Mariam ambalo si jina lake kamili alibakwa na kusalia kimya bila hata kumjulisha mamake.

Kwa Sasa Mariam analea mtoto mvulana mwenye umri wa miezi mitatu.Anataja kuwa alikuwa ameenda msalaani kujisaidia na huko ndiko alikumbana na jamaa aliyemdhulumu kwa kumbaka.

Mwandishi:Athuman Luchi

Sep 27, 202207:07
Changamoto za usalama wa barabarani kwa watu wenye Ulemavu

Changamoto za usalama wa barabarani kwa watu wenye Ulemavu

Bara la afrika limemulikwa sana katika ukuaji wa miundo msingi yake katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi na upanuzi wa barabara.

Licha ya miradi hiyo kurahisisha usafiri kwa mwananchi,bado kuna changamoto kubwa kwa jamii ya watu wenye ulemavu kutokana na ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwao.

Kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.

Sep 25, 202210:26
Jinsi Homa ya Chikungunya Ilivyokabiliwa Mombasa/Part 2

Jinsi Homa ya Chikungunya Ilivyokabiliwa Mombasa/Part 2

Mwaka wa 2017 hadi mwaka 2018, kaunti ya Mombasa ilishambuliwa na mkurupuko wa homa ya Chikungunya.

Homa ambayo ilikua mara ya kwanza kushuhudiwa.

Ili kukabili mkurupuko huo,kaunti ya Mombasa iliweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhusisha wahudumu wa afya wa kujitolea.

Hatua ambazo zilizaa matunda kama anavyoeleza mhariri wetu Ruth Keah kwenye Makala haya.

Sep 25, 202211:47