Skip to main content
Ijumaa Ya Sayansi

Ijumaa Ya Sayansi

By ResearchCOM
Hujambo na karibu katika Ijumaa Ya Sayansi, podikast inayokujia kila Ijumaa kutoka ResearchCOM, ikiangazia mada maarufu na muhimu zenye msingi wa utafiti wa kisayansi. Lengo kuu? Kukujuza kuhusu maendeleo.
Currently playing episode

Ijumaa Ya Sayansi(trailer)

Ijumaa Ya Sayansi

1x
Utafiti wa kisayansi unathaminiwa Tanzania?-Sehemu ya Pili
Ni Ijumaa nyingine ya sayansi, karibu usikilize.
21:03
February 25, 2022
Utafiti wa kisayansi unathaminiwa Tanzania?-Sehemu ya kwanza
Katika Ijumaa Ya Sayansi leo, tunaangazia dira ya Tanzania katika utafiti wa kisayansi. Hii ni sehemu ya kwanza ya mada hii na tunazungumza na Profesa Karim Manji, mbobezi katika utafiti & tiba ya magonjwa ya watoto kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.  Karibu. 
16:17
February 18, 2022
Magari ya umeme Tanzania: Sauti za wavumbuzi na wachumi
Tangu Julai mwaka jana, Umoja wa Ulaya (EU) umependekeza kuwa ifikapo mwaka 2035, uuzaji wa magari katika masoko makubwa ujikite katika magari ya nishati ya umeme pekee, badala ya dizeli na petroli. Nchi kadhaa, zikiwemo baadhi za Afrika zimeanza kuwekeza katika mifumo na sera ili kuchochea mabadiliko haya.  Kutana na mvumbuzi akutoka Tanzania ambaye anatengeneza mifano ya magari hayo nchini, akiona fursa licha zilizopo licha yakukumbwa  na changamoto lukuki. Pia, msikilize mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dkt Hildebrand Shayo akionyesha jinsi Tanzania  invyoapaswa kuamka mapema kujipanga na teknolojia hii mpya ya ujio wa magari ya umeme.
14:09
February 10, 2022
Wanasayansi ambao maandiko yao kuhusu UVIKO-19 yamevutia wafadhili kutoka Tanzania
Tanzania imefungua lango kwa wanasayansi kuanza kutafiti kuhusu UVIKO-19. Watafiti wengi wamekuwa na shahuku yakujua jinsi ugonjwa huo ulivyoathiri jamii hapa nchini. Kutana na baadhi ya wanasayansi ambao maandiko yao yamevutia wafadhili kutoka ndani ya nchi. Hawa ni baadhi ya watafiti 8 kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) waliopata tuzo za ufadhili kutoka mfuko wa Amne Salim ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani Dkt Salim Ahmed Salim utakaowawezesha wataalam hao kufanya tafiti kuhusu UVIKO-19.  Kuanzia sasa, usikose kufuatilia podcast yetu kujua mengi zaidi kuhusu Sayansi. Kumbuka, Ijumaa Ya Sayansi, ni podikast inayokujia kila Ijumaa kutoka ResearchCOM, ikiangazia mada maarufu na muhimu zenye msingi wa utafiti. Lengo kuu? Kukujuza kuhusu maendeleo. Tunajikita kwenye uvumbuzi, kilimo, afya, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Wiki hii uko na mtayarishaji wetu  Deusdedity Masemba, katika kipindi chetu cha kwanza Baada yakusikiliza hii, karibu tena Ijumaa Ijayo,  Weekend Njema!
11:55
February 04, 2022
Ijumaa Ya Sayansi(trailer)
Hujambo na karibu katika Ijumaa Ya Sayansi, podikast inayokujia kila Ijumaa kutoka ResearchCOM, ikiangazia mada maarufu na muhimu zenye msingi wa utafiti wa kisayansi. Lengo kuu? Kukujuza kuhusu maendeleo.
06:10
February 03, 2022