Skip to main content
Salama Na

Salama Na

By Salama Na

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society.
Available on
Amazon Music Logo
Apple Podcasts Logo
Google Podcasts Logo
Overcast Logo
RadioPublic Logo
Spotify Logo
Currently playing episode

SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE

Salama NaMar 02, 2023

00:00
59:34
SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE

SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE

Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa zaidi ukipata sasa nafasi ya kumuona anapokua kazini kwake hapo ndo utakaposhia kumpa nyota zake zote anazostahili kama bondia. Tena popote pale, iwe akiwa gym au ulingoni ambapo kadhaa washachezea shurba kutoka kwake.

Mfaume ni kama wengi wetu ambao tumetokea katika familia za kawaida tu ambayo malengo ya wazazi wetu kwetu ni kuhakikisha unasoma ili uweze kupata kazi nzuri na uje uwasaidie wao na Ndugu zako utakapokua mkubwa, vile vile mambo ya michezo ni kawaida maana kama mtoto unapokua unakua shuleni na mtaani ni lazima kunakua na kucheza, chochote ambacho kiko mbele lakini zaidi huwa ni mpira wa miguu kwa Kaka zetu ingawa sasa dunia imebadilika kiasi, siku hizi hata watoto wa kike kucheza soka ni jambo la kawaida tu na kwa hilo napenda sana.

So kwa Mfaume ni kama kwetu wengine tu, alianza kwa kucheza mpira lakini baadae interest yake ikatoka kutoka kwenye mpira na kuhamia kwenye ngumi, kwa wazazi wake huo ulikua mitihani hasa. Kwa mzazi kukuona mtoto wake akichezea vitasa mara kwa mara haliwezi kuwa jambo la kupokelewa kwa mikono miwili ndani ya nyumba, mtoto anarudi nyumbani kutoka kujifua nae anakua kafuliwa kwelikweli au akijua kwamba una pambano na mwamba flani aliye shindikana ndo hofu inapanda mpaka juu ya dari na inaeleweka kwanini inakua hivyo na kama mpaka sasa hujaelewa au hujaipatia picha basi mwenzetu huna moyo lol.

Alinipa story moja kwenye maogezi yetu haya kuhusu Mama yake, ananiambia kuna wakati alikua na mechi na bondia ambaye alikua anaongea sana, anajisifia na kumtishia sana maisha yake, kwamba atamchakaza vibaya sana tena mbele ya Mama yake, na aliyasema hayo akijua fika Mfaume huwa anaenda na Bi Mkubwa wake kwenye fight zake zote za ndani, ananiambia Mama yake aliogopa sana, alimsihi sana lakini kwa jitihada zake na maguvu ya Allah aliweza kumaliza mchezo wake huo vizuri tu.

Mabondia ni watu ambao wana roho za kipekee sana, unaweza ukamkuta mtu akiwa uliongoni anatoa dozi nzito kwa mpinzani wake ukadhani ni mtu mwenye roho mbaya sana, lakini ukimkuta nje ya ulingo na kwa watu wake utajua ni mtu wa aina nyengine kabisa. Kwa bahati nzuri nna marafiki ambao wanacheza mchezo huu wa boxing ikiwa pamoja na Mfaume mwenyewe, huwa ni watu wakarimu sana na wana mapenzi ya kweli lakini akiwa uliongoni anakua mtu mwengine kabisa, nadhani hiyo ndo tofauti ya masumbwi na michezo mengine.

Yangu matumaini uta enjoy session yetu hii ya mwisho ya msimu huu na mwana huyo humble kutoka kitaa, na pia kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusogeza sehemu.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Mar 02, 202359:34
SE7EP37 - SALAMA NA TOUFIQ | Um'PENDAE

SE7EP37 - SALAMA NA TOUFIQ | Um'PENDAE

Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan Abdullah Turky aka Mr White ambaye na yeye akiacha ukweli kwamba alikua tajiri na mfanya biashara nzuri huko visiwani ila yeye pia alikua kipenzi cha wananchi wa Jimbo la Mpendae ambapo sasa Toufiq ndo anaye liongoza jimbo hilo baada ya Mzee wake kutangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu Amrehemu.


Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chetu kikukuu Taufiq anakumbuka wakati wa msiba wa Mzee wake bado wa moto kabisa watu walikua wanakuja nyumbani kwao na kumshauri yeye agombee ubunge wa jimbo hilo ambalo Mzee wake alikua akiliongoza. Ikumbukwe Mzee wake Mr White alifariki kipindi ambacho wananchi walikua wanajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge wawakilishi na Rais, ananiambia kwanza aliwafukuza watu hao, wakarudi tena baada ya maziko bado Toufiq akawakatalia, baadae baada ya mambo kutulizana na kuombeleza kupungua watu ambao anawaheshimu walimfuata tena na kumueleza umuhimu wa yeye kugombea jimbo hilo. Wakamuelezea umuhimu wa Marehemu Mzee wake kwa watu wa Mpendae na kwamba kama hatofanya hivyo basi haitakua jambo zuri kwa wakazi wa eneo hilo. Ndugu Turky ilibidi akubaliane na ombi hilo na kutimiza matakwa ya wana Mpendae ambao walimpa kura nyingi za ndio.


Yeye mawazo yake yalikua kwenye kuendeleza biashara zaidi ambayo kwa kiasi kikubwa Mzee wake alikua alimshirikisha nayo toka akiwa mdogo. Kuweza kufanya yote hayo kwa kijana mdogo kama yeye pengine ingekua mambo mengi sana so kwa heshima wakati mambo mengine yanaenda Toufiq ilibidi aachie majukumu mengine kwa Mdogo wake wa Kiume Ndugu Abdallah Salim na Dada yake Bi Khaytham Salim Turky, ingawa bado yeye ndo Mwenyekiti wa makampuni hayo ambayo yamejikita katika biashara mbali mbali ambazo zimestawi visiwani Zanzibar na nchi nyengine.


Toufiq alikuja kwenye maongezi haya akiwa na mambo yake mengine ya ki majukumu kwenye meza yake na ki ukweli hatukupata wasaa teeele wa kuweza kuyachambua mengi kama ambavyo tungependa lakini pia hatukukosa lolote jambo la lolote jambo hilo ndo tumaini letu litasaidia kwenye kukusogeza kwenye sehemu fulani katika uelewa na uchambuzi wako wa mambo.

Tafadhali enjoy hiki kidogo ambacho tuliweza kukukusanyia kwenye muda mchache.


Love,

Salama.

Feb 23, 202335:56
SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…

SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…

Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka tunaenda mtamboni kiiila msomaji wake anapeeenda ambayo yameandikwa na ambayo anaendelea kuyaandika.

Wakati msimu huu unaanza Ally Bee hakua moja ya majina ambayo yalikua yameandikwa kama mmoja ya watu ambao tungependa kujua story ya maisha yake, kutaka kujua nini kinampa hamasa ya kufanya ambacho anafanya na pengine mambo mengine tele ambayo atakua na uhuru wa ku share na sisi. Ila kuna siku nilikua nyumbani na Rafiki yangu ambaye pia ni mdogo wangu Ndugu Sadam Almando Sanare ambaye nilikua namuuliza maswali kuhusu Dj mwengine kabisa huku nikilalamika kuhusu huyo mtu kwamba pengine kuna jambo haliko sawa kuhusu simulizi zake za baadhi ya mambo maana amekua kama anaongelea sana skuizi, then yeye akaniambia kuhusu Ally Bee (binafsi hupenda kumuita Ally Bee kwasababu wote tunamjua nyuki, na ukali wake lakini asali yake sote ndo kama hivyo, hopefully it will make sense kwake someday 😄). So wakati ananiambia nami tayari nilikua nishamuona, basi mengine yakaendelea kwenye meza yetu adhimu.

Story ya maisha yake Ndugu yetu huyu ni ya mateso mengi sana, ila kwa sasa na hata pengine mwanzo kwa adha zote hizo tunamshukuru Allah kwa hayo yote maana hayo ndo yameleta hasira za yeye kutaka zaidi, kuomba zaidi na kufanyia kazi zaidi yote ambayo anayo leo. Ally anakumbuka jinsi alivyofika Dar es Salaam mara ya kwanza na pia amenihadithia adha ya kutokua na sehemu ya kukaa hasa unapokua umekuja mjini mara ya kwanza. Alinifanya nijiulize maswali mengi sana mimi kama binadamu wa kawaida kabisa, au ambaye Mwenyezi kanibariki kwa mengi zaidi ya wengine, nini nafanya kuwasaidia ambao nawaona barabarani? Au ambao hawana uwezo wa kunifikia lakini wana uhitaji? Kanifundisha kuhusu kutochukulia maisha au nafasi ambazo tunazo kwenye maisha yetu kwamba ni kawaida tu. Ki ukweli kila ambacho tunacho kwenye maisha yetu TUNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU AMBAYE AMETUPA. Ila pia inabidi mara moja moja tujipigie makofi kwa mbali ambapo tumetoka na ambapo tumefika lakini zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu azidi kutuimarisha na kutufungulia milango ya Kheri, ZAIDI.

Niamini mimi nikikuambia kuhusu kutoa, kwamba kutoa ni raha zaidi kuliko kupokea ingawa wengi wetu tunapenda zaidi kupokea, ukitaka kujua hilo jaribu kwa kuanza kumpa hata mtu zawadi ndogo tu, hata pipi ambayo alikua hategemei kama utampa au utakumbuka, sura yake itakueleza mengi hata kama yeye ataamua asikuambie kwasababu zake zozote tu. Ally alisaidiwa na mtu ambaye hata walikua hawafahamiani na kuamua kumpa hifadhi katika sehemu ambayo yeye alikua anakaa. Pengine yeye alipofanya wala hakujua kama Ndugu Ally atakuja kuwa mmoja wa ma DJ HODARI na Hyper Man bora ambae nchi hii imewahi kuona.

Leo ningependa tujifunze kuhusu hilo, kuhusu kuwa kind, kuhusu kuwapa watu nafasi kwenye maisha yetu na kutosubiri malipo kutoka kwao maana pengine yanaweza yasije lakini wewe tayari unakua ushamaliza kazi yako.

Yangu matumaini story ya DJ Ally Bee itakua na impact kwenye maisha yako kama ambavyo imekua kwenye maisha yangu.

Enjoy and stay BLESSED.

Love,

Salama.

Feb 16, 202301:04:32
SE7EP35 - SALAMA NA EVANS BUKUKU | STICK - TO- ITIVENESS

SE7EP35 - SALAMA NA EVANS BUKUKU | STICK - TO- ITIVENESS

Ulikua muda mwingi hasa umepita toka mara ya mwisho nilionana na Evans wa Bukuku na kukaa naye chini kisha tukaongea. Na ki ukweli hajawahi kuwa rafiki yangu wa karibu ila ni mtu ambaye tunafahamina na kuheshimiana. Hustle zake nazifahamu kwa ukaribu maana industry ambayo tunafanya kazi ndo hiyo hiyo kwahiyo nikama chakula, tusipokutana jikoni basi tutakutana kwenye sahani. Kama ilivyo kwa watu wengi nimekua nikimsikia kwenye radio mbali mbali katika safari yake kama mtangazaji wa vipindi mbalimbali lakini pia nimekua nikimuona kwenye majukwaa mbalimbali akifanya shughuli zake za ku host sherehe au matamasha kadhaa.

Kwenye kitabu changu yeye ni mmoja wa hustlers timamu kabisa ambao Tanzania yetu inayo na mazungumzo yetu haya pia kwa kiasi kikubwa yamenipa picha nyengine ya aina ya mtu ambaye yeye ni, kwanza alikuja kwenye set na binti yake (ambaye tayari kashanizidi urefu) na inavyoonekana ni rafiki yake mkubwa maana huwa yuko naye benet mara nyingi, nadhani kwa experience yake ya kukutana na watu wengi kutoka sehemu tofauti kumemfanya naye pia ajifunze mambo flani kutoka kwao na hili ni jibu kati ya majibu ambayo niliyapata kutoka kwenye maongezi yetu. Watu wengi ambao amekua akikutana nao wanamfundisha mambo mengi na ukiachana pia kwamba na yeye amekua kwenye maisha ya ‘ki familia’ zaidi maana yeye na wazazi wake na Dada pamoja na Marehemu Kaka yake wako karibu sana.

Moja ya mambo aliniambia ni jinsi ambavyo anaangalia anachokula na kujitunza yeye na mwili wake, anahakikisha anapata muda mzuri wa kupumzika na vilevile kufanya mazoezi. Anajua umuhimu wa haya yote na anayafanyia kazi. Binafsi kwanza nilitaka kujua kwanini amekua akimua kufanya vipindi vya radio vya asubuhi tu na sio wakati mwengine? Nini hasa maana ya hiyo? Majibu yake yatakufurahisha kama nawe utakua mtu wa kujifunza.

Hatukuweza kuacha kumuongelea Marehemu Roy ambaye alikua ni Kaka yake, nami nilijua hiyo siku, muda wote nilikua nikidhania yeye ndo mkubwa. Roy ni mmoja wa wapishi wazuri wa Bongo Flava tamu ambayo tulianza kuipenda kwenye miaka ya mwanzo ya 2000, Roy ndo mpishi wa Mr Blue, kina Ally Kiba, kina ParkLane na wengine tele, heshima yake ni kubwa na binafsi nilitaka aliskie hilo kutoka kwangu. Na nilitaka kujua kitu ambacho kilisababisha kifo chake pia, haikua rahisi kuuliza maswali kama haya lakini pia hakukua na budi maana maua ya Kaka yake ilikua ni wajibu wake kuyapokea.

Pia tulimuongelea Enika ambaye ni Dada yake pia, nilitaka kujua nini ambacho kimemfanya asifanye tena Bongo Flava, na nini ambacho anafanya sasa, na je ana furaha? Tuliongelea pia hustle yake nyengine ya comedy ambayo nayo amekua akiizingatia na kuisimamia kwa miaka sasa, hakuna comedian yoyote kwenye nchi hii ambaye kwa kiasi chochote kile hana mchango wake ndani yake, na si lazima awe amepita mikononi mwake, bali hata njia (nyingi) ambazo amewahi kuzitengeneza na ambazo anaendelea kuzisimamia.

Evans mtu, tena wa watu na yangu matumaini utakubaliana nasi mara tu baada ya kuangalia au kuskiliza maongezi yetu haya.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Feb 09, 202301:13:36
SE7EP34 - SALAMA NA FETTY DENSA | KUTOKA UBAVUNI...

SE7EP34 - SALAMA NA FETTY DENSA | KUTOKA UBAVUNI...

Kwa ambao wanafuatilia mpira hapa nyumbani wanamjua mchezaji huyu mahiri wa Simba Queens lakini ambao wanafuatilla soka la wanawake hawa watakua wanaelewa uwezo binafsi na uhodari wake wa kucheza namba tofauti tofauti uwanjani ila ukimkuta kaikamata mbavu ya kulia aidha kwa Simba au timu ya Taifa ya Tanzania. Fatuma Issa ni mtu na nusu, hakuna mpenzi wa mpira au kocha yoyote wa mpira anaweza akamuacha kwenye benchi wakati team inatafuta matokeo au inataka kuwaonyesha walofika kuwaangalia vipaji ambavyo wanavyo kwenye kikosi chao. Kwa yoyote yule na kwa vyovyote vile, Fetty Densa, ni lazima AANZE.

Ananikumbusha sana mimi na rafiki zangu wakati tunakua, tulikua chizi michezo hasa baada ya kufika shule ya Sekondari, ilikua kama lazima kila mmoja kuwa na uwezo wa kucheza zaidi ya mchezo mmoja ili tuwe na vikosi imara inapotokea kwenda kufanya uwakilishi wa shule, mkoa au nchi. Binafsi nilikua na uwezo wa kucheza Basketball na table tennis tu ila nina marafikia kama kina Kalova na Mboni Mntambo ambao wao walikua wanacheza Basketball, Netball, Volleyball na chochote kitakajokuja mbele ambacho kinatumia mpira kucheza lol, na tena VIZURI, sio kujazia namba tu uwanjani. Naye Fetty ni kama wanangu hao kutokana na maongezi yetu. Ananiambia hata shuleni mwalimu na wanafunzi wote katika shule yao walikua wakifahamu na kujivunia yeye sana.

Akiwa anakua huko Morogoro Fetty ni ‘mtoto wa Bibi’ zaidi, yeye ndo alomlea na kumtunzia siri zake zote, na ndo alomfundisha kupika na kumkumbusha kwamba yeye ni mtoto wa kike kwahiyo alihakikisha pia mjukuu wake kwenye masuala ya kupika na usafi wake na wa nyumba pia haachi kujifunza. Bibi pia ndo alipewa ahadi ya kwamba kuna siku mjukuu atakuja kuwa mchezaji hodari kuwahi kutokea hapa nyumbani na so far, so good. Babu yake nae hakua nyuma kwenye kumsifia mjukuu wake pale anapofanya vizuri jikoni kwasababu pengine kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili ampe moyo mjukuu wake.

Fatuma anatuambia humu kwenye maongezi yetu jinsi ambavyo alihangaika mkoani Morogoro kupata team ya kucheza na jinsi ambavyo alijutuma toka siku ya kwanza kuhakikisha ndoto zake zinatimia. Ukimsikiliza kwa makini utagundua kama ni mtu mwenye mawazo ya mbele kuliko hata umri wake, hiyo inamsaidia pia inapofika wakati wa kufanya maamuzi anapokua ndani na nje ya uwanja. Unaweza ukajiuliza kwa kipaji chake na ujuzi wake kwanini hachezi nje ya nchi? Kwanini amekua Simba huu msimu wake wa nne na amekua akicheza kwa kiwango cha juu sana? Densa anatupa majibu ya swali hilo ambalo nina uhakika wengi wao wamekua wakijiuliza.

Mahusioano yake na Mama yake ambaye alikua mmoja kati ya wanenguaji wazuri miaka iliyopita na ndo alimfanya pia mwanae naye atake kuwa Densa (ndo jina la Fetty Densa lilikotokea). Wana mahusiono ya aina gani? Mama alilichukuliaje suala la Binti yake kuchagua soka? Na Mzee wake nae yuko wapi? Nafasi yake kwenye team yake? Team ya Taifa je? Experience ambayo waliipata Morocco wakati Simba ilipoenda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Africa? Vipi kuhusu mpira wa miguu wa wanawake hapa nyumbani? Pesa ipo? Muelekeo je?

Haya maongezi ni moja ya maongezi bora ambayo nimeshawahi kufanya na natumai yatafungua milango kwa watoto wa kike na wazazi wao wengi kuelewa na kuipambania fursa hii ambayo Dunia nzima imeanza kuielewa.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Feb 02, 202301:12:18
SE7EP33 - SALAMA NA MR BLUE | KHERI

SE7EP33 - SALAMA NA MR BLUE | KHERI

Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi, ana swagg ya kuongea na hata jinsi alivyokua anajibeba. Alikua wa moto sana unaweza kusema hivyo, au niseme hivyo. Kila ‘mtoto’ na kijana alitamani kuwa kama yeye kwa kila kitu, muonekano mpaka hit songs kwenye radio na TV.

Blue alikua na mtu ambaye anamsimamia na huyo hakua mwengine bali G Lover, meneja na Dj ambaye alikua anasimamia kazi zake yeye pamoja na wasanii wengine kama Ally Kiba, Ally Com na Abby Skills kwa kuwataja kwa uchache na wasanii wake hao wote walikua wa moooto sana. Ngoma kali, video mbaya, show nyingi na kwa ‘mhindi’ wanauza sana. Na kuanzia hapo kwa mhindi na kuuza sana ndo ambapo kuliweza kuwapoteza wengi kwasababu wengi walikua wadogo sana na pesa ilikua nyingi. Fitna na utovu wa nidhamu wa kupindukia ulianzia hapo. Wakati naandika hii nilimuwaza Ally Kiba na jinsi ambavyo ameweza ku maintain class flani toka siku ya kwanza tunamskia na mpaka leo regardless ya mengi ambayo yametokea hapo katikati, HAKUWAHI KUPOTEA. Kwa hilo naamini anastahili HESHIMA na recognition ya hali ya juu pengine kuliko tunayompa maana dah, mambo yalikua mengi sana enzi hizo.

Kuna usemi kwamba wakati ni mwalimu mzuri sana na kwa uelewa wangu hakuna ambaye anaweza kuelezea experience kama ilivyo elezewa kwenye usemi huo. Wakati ndo ambao unatufunza na kutuonyesha vitu na watu wengi, ambao tulikua tukiwaamini na wengine kuto kuwaamini, kuwapenda na wengine kuto wapenda, kudhani unajua na ki ukweli hujui, kudhania umezama kwenye dimbwi na mapenzi na huyo alo nae ndo wako wa milele na kumbe si hivyo na hayo yote unayaelewa within kipindi fulani, miaka inavyokwenda ndo na wewe unaelewa na kujifunza mambo kwa uwezo na uelewa wako. Moment za ‘anha’ na ‘wow’ huwa nyingi sana. Wakati ni MWALIMU na majuto huwa ni mjukuu, nadhani utakua umenielewa.

Mr Blue alikua na dunia kwenye miguu yake, ilikua yeye tu aseme anatakaje na anataka ielekee wapi na hivyo ndo ingekua ila haikua hivyo ndo jambo la kusikitisha lakini bahati kubwa ambayo mwenzetu alikua nayo au yuko nayo ni kwamba hayo yote yalitokea mapema sana, wakati yuko mdogo sana kwenye dunia ambayo wengi walikua wakimuangalia na kumpenda sana. Yeye baada ya kuona mapenzi na shangwe hilo basi akadata na akaanza kuwa mgumu kufanya nae kazi, akawa na marafiki tele ambao hakua anawajua kabla hajawa Lil Sama na baadae Mr Blue. Akawa hasikii la muadhini wala mnadi sala. Akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi isokua na staha, akaondoka nyumbani na kwenda kuishi kwenye ma ghetto na wana wasokua na ramani. Akawa ana party Jumatatu mpaka Jumatatu. Studio haonekani, kwenye interview hatokei na wale watangazaji ambao walikua wanapiga mgoma zake kwenye Radio akawa hata salaam hawapi. Producer na meneja nao wakagombana nae kwasababu sitofahamu ya pesa kwa mhindi ilishika hatamu.

Mwanzo nilisema Blue ana Kheri sana kama jina lake kwasababu hayo yote yalitokea wakati mdogo sana, dunia ilimfunza nae akafundishika, wakati dunia hiyo ikiwa inamfunza alikua mwanafunzi mzuri sana kwasababu darasa alilolipata wakati kakata ringi ndo ambalo limefanya awe BORA na ajitambue LEO HII.
Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu Blue ananielezea hustle zote ambazo alishawahi kuzipitia wakati anakua na huku akiwa anajitafuta na kwa uelewa wangu itasaidia wengi ambao wanaaza au wataanza kuzishika pesa mapema au hata ambao watapata mafanikio huko mbeleni watajua jinsi ya ‘kujibeba’ kutokana na maongezi yetu haya.

Maongezi haya yalikua yafanyike mapema tu lakini u busy wa Lil Sama na kupishana kwa ratiba zetu ndo kulifanya yatokee
Jan 26, 202356:32
SE7EP32 - SALAMA NA MRISHO NGASSA | MACHACHARI…

SE7EP32 - SALAMA NA MRISHO NGASSA | MACHACHARI…

Mrisho Halfani Ngassa alikua top top top footballer na kwa bahati nzuri nishawahi kumshuhudia akiwa kazini kwake, tena ukimkuta kaamka vizuri basi uhakika wa burudani ni UHAKIKA . Na kipindi ambacho alikua kwenye peak yake pia kulikua na vitasa imara na magolkipa wazuri tu lakini nna uhakika kila mmoja kati yao ana la kusema kuhusu winga na forward hii machachari ambayo nchi yetu ishawahi kuona. Hakuna kitasa ambacho hakijawahi kukataa kufungua mlango muda ambao Mrisho Ngassa alikua anakuja kupiga hodi.

Uzuri wake alianza kucheza mapema sana na kwasababu alikua machachari basi hata utulivu kidogo wakati anakua ulikua sio mzuri sana maana alikua na haraka. Ananiambia kwenye session hii vile ambavyo ali sign Yanga pasi na kumskiliza kocha wake kutoka Mwanza ambaye alikua anaamini kama dogo bado hajaiva, Pengine miaka miwili au mitatu ya kuendelea kujijenga ingemfanya awe bora zaidi na zaidi lakini kwenye kichwa na fikra za kijana huyu ambaye alikua na uchu wa mafanikio na kutaka kufika mjini maongezi hayo ya kusubiri yalikua ni kama kumuona sisimizi kwenye sukari alafu unamuambia asile leo badala yake ataila asubuhi, isingewezekana. Hivyo kocha akaona basi si mbaya, aende akayaone na kujifunza akiwa kazini.

Yanga ndo Yanga, kwa wachezaji wote wanao chipukia au ambao ndo wanatafuta maisha kuichezea klabu kama ya wananchi ni heshima kubwa sana na zaidi kama wao ndo wametaka iwe hivyo. Kwa kijana mdogo ambaye alikua na spidi na uchu mkubwa wa kuzitia nyavuni basi klabuni pale ndo ilikua steji muafaka ya kuonyesha kipaji chake. Mrisho anakumbuka aina ya ‘vifaa’ ambavyo vilikua vinapatikana mitaa ya Jangwani. Majina makubwa na kazi ilotukuka ambayo walikua wakiifanya ilikua inajielezea. Kwa kijana kutoka mkoani kuweza kupata namba haikua kazi rahisi, ila pia haikua kazi ngumu maana ulichokisia ndo ambacho unakiona, kuanzia mazoezini mpaka anapopatiwa nafasi wakati wa mechi.

Kwenye episode hii tunazungumzia aina ya mitihani na maamuzi ambayo ilikua inabidi yafanyike. Kwenye wasifu wake Mrisho amewahi kucheza kwenye team zote tatu kubwa hapa nyumbani kwetu. Kashawahi kuwa muajiriwa wa Yanga, Azam na Simba ambapo alienda kwa mkopo kutoka Azam FC, lakini pia ashawahi kupatiwa majaribio katika team kadhaa nje ya nchi yetu na wakubwa wanasema kama Ndugu yetu angekua katuliza akili na angefahamu aina ya nafasi ambayo alikua nayo kipindi kile basi yeye ndo angekua mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi pendwa ya Uingereza. Trials kwenye klabu kama Westham alipata na ofa kwenye vilabu kadhaa kutoka hapa hapa barani Afrika nazo zilikua hazikati.

Sasa, nini haswa kilitokea? Wapi hasa alienda mrama? Ni kweli alikosea? Au malengo yake si malengo yetu? Au tulipokua tunamuona sisi yeye alikua hapaoni huko? Vikwazo vilikua nini? Mambo yepi hasa ndo ambayo yanaweza yakawa ndo chachu ya hayo yote kutotokea? Kama Mrisho angekua anawez kufunguka zaidi nami kwenye episode hii naamini tungeweza kupata funzo lilonyooka kwa wenetu na ukichukulia sasa mambo ndo yameanza kufunguka. Naamini angekua mwalimu mzuri kwa wake wote ambao wangetaka kusoma somo ambalo lina uhitaji mkubwa.

Yangu matumaini utaweza kuelewa na kupata chochote kitu kutoka kwenye maongezi haya.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Jan 19, 202301:20:33
SE7EP31 - SALAMA NA KUSAH | NG’WANA AZAIZA!!

SE7EP31 - SALAMA NA KUSAH | NG’WANA AZAIZA!!

Kutoka zake Lushoto huku mkoani Tanga ni kijana mtanashati ambaye anajua kama amekuja town au jijini Dar es Salaam kwasababu ya kusaka pesa ili abadilishe maisha yake na ya wale ambao wamemzunguka. Na kila alikumbuka ambapo ametoka basi spidi ya kuhakikisha kalamu yake haivuji na inaandika kwa muandiko mzuri ili kila ambaye atabahatika kusoma kile ambacho yeye kakiwaza na kukiandika basi azame kwenye dimbwi lake na endelee kumsikiliza mpaka pale yeye mambo yake yatakapoenda, na kwa story ambazo amenipa basi ukinasa kwenye kitabu chake itakuia vigumu kutoka kwasababu amepanga kuwepo kwa muda mrefu sana, nia na madhumuni yake ni kuhakikisha yupo yupo sana.

Kusah ananihadithia aina ya kazi ambazo ilibidi afanye wakati anakua, ilikua inabidi aende shuleni ila pia amsaidie Bi Mkubwa wake ambaye alikua anafanya kazi nyingi kuhakikisha watoto wanakula na kusoma, ikiwa pamoja na kuuza pombe za kienyeji ambazo ni haramu. Uvunjaji huo wa sheria ulikua unaifanya familia iingie matatani na anakumbuka kipindi ambacho ilikua inabidi amsaidie Mama kuficha vitendea kazi na vithibiti pale msako wa ghafla unapotokea. Kama mtoto wa kiume kwa utashi wake tu toka akiwa na umri mdogo aliona huo ulikua ni wajibu wake kuhakikisha Mama yake yuko Salama.

Tukizungumzia suala zima la kazi ambayo ameichagua kufanya sasa yeye ni fundi, moja ya mafundi hodari ambao ameshaanza kujijengea na fan base yake nzuri tu, show za ndani na nje anafanya na anaelewa jinsi ya kuji brand na nini cha kufanya wakati gani na kitamfaaje. Mambo ambayo anayafanya na kuyafanikisha ni ambayo yawewachukua baadhi ya watu muda kuweza kuyakamilisha lakini yeye kwa kipindi kifupi ameweza kupiga hatua kubwa na pengine ingekua kubwa zaidi kama kusingekua na kuchelewa flani hivi ambako kulitokea baada kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Ruby ambao kwa taarifa tulizokua tunazisikia na nyengine kuzisoma mtandaoni mahusiono yao hayakua mazuri kwa afya ya kila mmoja wao.

Kusah anazungumza nasi kuhusu hilo, kuhusu Mama yake, kuhusu Lushoto na plan ya maisha yake. Ameongea na sisi kuhusu kazi alizowahi kufanya maishani mwake, jinsi alivyoweza kutoka kwenye ‘toxic’ relationship ambayo ilikua ikimuumiza yeye na aliyekua partner wake. Pia anatuhadithia suala la yeye kuwa Baba kwa mara ya kwanza na mara ya pili. Tumeongelea pia mahusiano yake na Aunt Ezekiel na plan zake za huko mbele akiwa kama mwanamuziki ambaye amejikita zaidi.

Yangu matumaini uta enjoy kila sekunde ya maongezi yetu haya na mawili matatu utayapata ya kukufunza jambo.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Jan 12, 202350:39
SE7EP30 - SALAMA NA BRENDA | MY DEAR…

SE7EP30 - SALAMA NA BRENDA | MY DEAR…

Ushawahi kumuangalia mtu kwa mbali na kujiuliza maswali mengi juu yake? Maswali kama siku yake ikoje, amewezaje? Kama ana familia? Ki kawaida huwa anaamka saa ngapi? Amesoma wapi? Siku yake anaipangaje? Ana watoto? Mtoto? Huwa anawaandaa kwenda shule? Muda je wa kukaa nao? Elimu yake ameipatia wapi? Kwenye familia aliyotoka je? Wazazi wake wapo? Na je wanajivunia yeye kwa kiasi gani?

Sasa ili kupata majibu ya maswali hayo yote ilibidi tumtafute Bi Brenda Msangi-Kinemo ambaye ndo nilikua namzungumzia hapo juu. Kama wewe utakua mtu wa kujua ambayo yanaendelea nchini, na pia kama ni mkazi wa Dar es Salaam basi lazima utakua unajua kuhusu hospitali ya CCBRT ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia na inaendelea kutoa huduma za macho, mifupa na magonjwa mengine kwa watu wengi kwenye nchi yetu. Sasa Bi Brenda yeye ndo Mkurugenzi pale. Na amekua kwenye cheo hicho kwa zaidi ya miaka minne sasa na hiyo ukiachilia mbali miaka ambayo alikua akifanya kazi pale wakati bado hakua Mkurugenzi.

Yeye ni mtaalamu wa masuala ya afya, hicho ndo ambacho aliendea skuli huko nchini Uingereza na kwa mujibu wa baadhi ya majarida ambayo nimesoma maisha yake kama yalikua yanataka kubaki huko baada ya kuhutimu ila aliporudi nyumbani na kupata nafasi pale hospitali mambo mengi yalibadilika. Kwenye kipindi hiki anatusimulia jinsi ambavyo hayo yalitokea. Na aina ya maamuzi ambayo ilibidi ayachukue ili mambo yatuwame.

Kwa wasichana wengi hasa wale ambao wanakua na kuanza kujitafuta Brenda ni role model wao sana na ni nafasi ambayo kwake yeye ilikuja baada ya kuwa anaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu kupambana na kuweza kuvaa kofia zaidi ya moja kwenye maisha ukiwa kama mwanamke. Humu pia ananiambia jinsi ambavyo hizo nondo za ku inspire zilivyoanza, ananiambia jinsi ambavyo alikua akisoma na kufanya kazi na wakati mwengine jinsi ambavyo majukumu yalikua yakimzidi mpaka anakaribia kukata tamaa ila msukumo ambao alikua akiupata kutoka ndani yake ndo ambao ulimfikisha alipo. Aliamini kwamba kuna wanawake na wasichana wengi ambao wanapitia kwenye mitihani ambayo yeye alikua nayo na kama yeye aliweza kushinda basi aliona atumie sauti yake na busara zake kuwaambia wengine kama hakuna kinacho shindikana kama nia inakuwepo.

Binafsi nilijichotea mengi sana kutoka kwenye kisima chake cha busara na uthubutu na bado darasa naendelea kulipata kwasababu nafuatilia yale anayo yafanya na ambayo anayaandika ili kusaidia wengine wasijione wako peke yao.

Mungu amueke na aendelee kumsimamia kwenye kazi zake na maono yake ambayo yanasaidia watu wengi wengine kuanzia ofisini kwake mpaka kanisani na nyumbani.

Yangu matumaini nawe uta enjoy na kupata faida kwenye episode hii kama ilivyo nia yetu.

Love,

Salama.

Jan 05, 202301:06:18
SE7EP29 - SALAMA NA DEO GRATIUS | PRIVILEGED?!

SE7EP29 - SALAMA NA DEO GRATIUS | PRIVILEGED?!

 Deo Gratias, jina tu linatosha kujielezea kama wewe nawe utakua kama mimi wa kutaka kujua maana ya majina ya watu ili uweze kujua tabia zao au ujiulize wazee wake walikua wanafikiria nini wakati wanaamua kumpa jina hilo mtoto wao. Kwa Deo maana imejibeba na imejikamilisha na kwa yeye kuamua kubaki na jina lake hilo hilo mpaka kwenye stage ambako ndo sehemu yake ya kazi inabidi hilo nalo likuambie jambo kuhusu yeye na jinsi ambavyo anajichukulia na kuyachukulia mambo ambayo ameyachagua kuyafanya.

Shukrani ziende kwa Mungu ndo maana ya jina lake, shukrani ziende kwa Mungu kwa kila alifanyalo leo, shukrani ziende kwa Mungu maana baada ya wazee wake kumsomesha kwenye shule ambayo walikua wameianzisha wao na kuhakikisha kijana wao anapata elimu ambayo anastahili lakini yeye akaamua kuiacha fani ambayo aliisoma na kuamua kuwa mchekeshaji basi nadhani Shukrani ziende kwa Mungu, Shukrani ziende kwa Mungu kwa wazazi wake kuelewa, Shukrani pia ziende kwa Mungu kwasababu mwanga umeanza kuonekana kwenye lile alifanyalo sasa.

Yeye na rafiki zake ambao ni vijana wenzake wamejikusanya na kuanzisha kundi lao linaloitwa Watu Baki, ila hawakuamka tu wakaanzisha, kuna ka story hapo nyuma yake ambapo ndo panaleta maana kwenye maisha yetu na yao kama watafutaji. Deo anakumbuka audition ya kwanza ya Stand Up Comedy ambayo aliwahi kuifanya na akashinda huko Mbagala, chini ya shindano lililokua likisimamiwa na Evans Bukuku, Deo anakumbuka kushinda MILIONI nadhani kwenye shindano hilo ingawa alipofika home aligundua kuna mwana alichomoka na elfu kumi yake, yaani kuna mwana alimuangalia Deo, kisha akakiangalia kibunda alafu akasema nah, hawezi kumpa yote lol.

Courage ya kufanya mengine mengi ikiwa na pamoja na ambayo yanaendelea leo ilianzia hapo. Mengine yakabaki story!

Story ya kujikusanya na wanae enzi za Cheka Tu na baadae kuamua kundoka na kuanzisha WatuBaki ilikua mmoja inabidi awe na uthubutu na uthubutu huo uliwezekana na mpaka leo wamesimama na wana time yao kwenye DSTV ambayo inatoa burudani nzuri tu kwa watu wao na vile vile bado matamasha ya nje wanafanya wao kama wao.

Kwa wengi ikiwa pamoja na mimi tulipewa story kwamba Deo ni mtoto flani wa kishua alokua kutoka kwenye familia inayokula wali kwa kijiko na ndo maana baadhi ya mambo ilikua rahisi kwake kufanyika kwasababu ana uwezo wa kurudi nyumbani kwa Baba na Mama na akarudi na mzigo wa kutosha ambao unasaidia mambo yaende. Ila kwa mujibu wake, hiyo si habari na wala yeye hajatoka kwenye mazingira hayo ambayo wengi wanadhani ametokea.

Bado safari ndo kwanza imeanza na kwa wenzake yeye akiwa kama kiongozi anaamini kama wakitulia pamoja na kufuata maono yao basi mengi mazuri tu yatakuja, ila sasa huo uwezo wa kuweza kutulia pamoja na kutengeneza kitu kikubwa na kizuri ndo inawezakana ikawa mtihani. Si wengi wameweza ingawa wapo ambao wameanza pamoja na mpaka leo wanaunguruma pamoja. Inawezekana na yangu matumaini wao pia wataendelea kuwa WatuBaki kwa muda wote ulobaki.

Love,

Salama.

Dec 29, 202201:11:01
SE7EP28 - SALAMA NA GARA B | BABA SHUGHULI

SE7EP28 - SALAMA NA GARA B | BABA SHUGHULI

Jina MC Gara B ni miungoni mwa majina makubwa sana kwenye ulimwengu wa kazi ambayo mwenzetu huyu amechagua kuifanya. Familia yake, mke na watoto, wazazi wake na wa mkewe pengine, Ndugu jamaa na marafiki na waajiriwa wake wanakula vizuri kwasababu ya kipaji chake Ndugu yetu huyu. Ni mwanaume ambaye akiwa kazini kwake furaha na burudani ambayo huwapa wateja wake ndo inayomfanya azidi kuenda mbali kwenye tasnia hiyo ya ushereheshaji. Again, yeye ni mmoja ya BORA kadhaa ambao wanafanya kazi kama yake.

Mtandao wa kijamii ni kitu kimoja chenye nguvu sana kwenye miaka ya hivi karibuni, kwa ushahidi tulonao tushawaona wengi ‘wakitoboa’ kwasababu ya Instagram au sehemu nyengine. Mitandao iko mingi na kila mmoja na tobo lake la kufikia mjini. Kazi ambayo MC huyu huifanya yeye huenda na team yake kuiweka vizuri kisha ana post kwenye page yake yenye watu karibia MILIONI MOJA NA NUSU. Akizifikisha mjini kazi hizo wengi huvutiwa nazo na ambao wanakua wana shughuli nao bila ya shaka watamtafuta na kutaka kufanya nae kazi. Ubunifu wake ni wa kipekee kutokana na vingi na wengi ambao tumekua tukiwaona kwa miaka mingi sasa. Mtandao wa kijamii umemsaidia na unaendelea kumfanya awe bora zaidi ya jana.

Sasa, shughuli hii anayo ifanya ndo ambayo ilikua ndoto zake? Pengine alikua huku anamuona mtu fulani akiwa anaifanya hii kazi kwa ufanisi na ikamvutia? Ilikuaje mpaka akaingia huko? Kwa kumtizama haraka haraka tu utagundua Ndugu yetu ni MCHESHI, yeye anapenda kucheka na kuongea, ingawa hapo kwenye kuongea nako sio kiviiiile ila ni mtafutaji ambaye AMETIMIA. Story yake alotupa kwenye episode hii inajumuisha yeye kufanya kazi zaidi ya mbili kwenye kipindi flani hivi cha maisha yake ili aweze kuishi vizuri. Ki professional mwenzetu ni MWALIMU, ambaye hiyo kazi aliifanya hasa, na akaijumlisha na kazi ya huduma kwa wateja pale Tigo na wakati huo huo akawa anafanya kazi kwenye kiwanda kimoja hivi huko Pugu Road, hakua na wa kumdekea wala kumsubiria na hustle yake hiyo ndo ambayo anaenda nayo mpaka leo kwenye maisha yake.

Sasa kama Baba na mume kwa mkewe kipenzi ambaye naye alikutana nae sehemu ya kazi yake, Gara B ananijibu kuhusu uaminifu ambao anao kwa mkewe ambaye kwa mujibu wangu kama amekutana nae kwenye mazingira hayo, vipi hujiskia kila mara anapokua kazini mumewe ukichukulia huko ndipo walipo kutana na ndo ambapo wanawake wengi wazuri huwepo? Jibu lake lilikua na kuukonga moyo.

Alituhadhia pia kuhusu wazazi wake na jinsi ambayo ameweza kujitengenezea jina, siku ya kwanza alipopata kimeo cha ku host harusi ya watu ambayo kwa mujibu wake aliibembeleza sana na hakua amepewa nafasi, ila nafasi ilipojileta akanyoosha kwa umbali mrefu mpaka mengine yamebaki story tu. Na hii ndo ilikua simulizi yangu bora kabisa kuhusu kupata nafasi na kuzitumia vyema.

Yangu matumaini utaskiliza na kuangalia kwa makini maana humu anatupa simulizi zote za kutokata tamaa na jinsi ya kuchukua nafasi, ila pia anatuhadithia baadhi ya mitihani ambayo huja na umaarufu pia na jinsi ya kupambana nayo. Mimi nili enjoy na natumai itakua hivyo kwako pia.

Happy Holidays.

Love,

Salama.

Dec 22, 202201:00:26
SE7EP27 - SALAMA NA BARAKA KIZUGUTO | NEUTRAL

SE7EP27 - SALAMA NA BARAKA KIZUGUTO | NEUTRAL

Baraka Kizuguto si moja ya majina yajulikanayo miungoni mwa wa Tanzania wengi ambao asilimia kubwa ya wenye simu za mkononi hupendelea zaidi habari za maisha ya watu maarufu na mashuhuri, kutaka kujua wanakula nini, wanaishi wapi, wanalala wapi, wanalala na nani na kadhalika. Na kama wewe ni mmoja wa watu hao na si mpenzi wa mpira basi kumfahamu mgeni wetu wa kwenye kiti chakavu wiki hii itakuwia vigumu. Ila kwa wale watu wa mpira, au wafanyakazi kwenye Vyama vya mpira hapa kwetu na Afrika kwa ujumla au wachezaji au waalimu wa mpira jina na sura yake si ngeni kabisa kwao. Mimi na yeye tulifahamiana hapa mjini miaka kadhaa iliyopita na rafiki yetu mmoja ndo alituunghanisha. Mapenzi yangu kwa mpira wa miguu nayo yalifanya urafiki wetu ukolee zaidi, amekua kiungo kwenye mambo yangu mengi yanayohusiana na kiwanda hiko kwa muda sasa. MSHAURI wangu pia baada ya mimi kupata kibali cha kuweza kuwasisamia wachezaji wa mpira wa miguu duniani. Yeye ni mtu ambaye anawajua wachezaji karibia wote wanaocheza mpira nchi hii na nje, na msaada wake kwangu ni wa kipekee kabisa. Nia na madhumuni ya kusema aje tuongee nae kwenye kipindi chetu ni kwasababu ambazo nimezieleza hapo juu kwenye wasifu wake. Waswahili wanasema ‘kizuri kula na nduguzo’ na kwa msaada na elimu ambayo mimi hupata kutoka kwake nikasema kwanini sasa tusimlete mezani na wengine wakamsikia? Ukichukulia suala la ajira mi kipengele kweli kweli kwenye nchi yetu. Baraka yeye ana ajira ambayo kama tukimsikiliza vizuri basi wengi wanaweza kuchagua njia hiyo na wakapata chochote kitu. Sasa NINI ambacho Baraka hufanya? Kwenye episode hii anatuelezea majukumu yake ya muda mwingi kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania na Shirikisho la Mpira la Africa. Kukiwa na michezo mbali mbali kama ya nchi na nchi, au klabu kwa klabu yeye ndo huwa msimamizi wa kwanza kwenye michezo hiyo. Safari za kila wikiendi haziishi na kaniambia nidhamu na kujifunza kila siku ndo msingi wake, na je ungependa kujua kikubwa zaidi ambacho ni muhimu kuliko hayo yote? Baraka anasema ni kuweza kuheshimu WAKATI. Hiyo ndo siri ya mafanikio yake, na ndo siri ya yeye kuweza kupata kazi zaidi na zaidi na kuheshimika pia. Kama akiwa kapangiwa mechi ya kusimamia tuseme nchini Angola, labda Kuna mechi kati ya Angola na pengine Madagascar au mechi za klabu kutoka nchi hizo, yeye ndo anakua wakwaza kufika kabla ya team na waamuzi. Kazi yake ni kuhakikisha kila anaye husika na mchezo huo anafanya jambo lake kwa wakati unaotakiwa. Ukaguzi wa hoteli watakazokaa wageni wa mchezo, waamuzi, team, jinsi watakavyoenda uwanjani, mikutano ya waandishi wa habari, ulinzi wa waamuzi wa mchezo huo, kuhusu ball boys, jinsi team zitakavyo ingia uwanjani, kuhakikisha mchezo unaanza kwa wakati na kila kitu kwenda sawa sawa. Jinsi ambavyo unafanya kazi yako vizuri ndo jinsi ambavyo Shirikisho linakuamini na ndo ambavyo CV yako inazidi kukua. Kwahiyo mmoja anawezaje kupata nafasi ya kufanya hayo yote? Yeye aliwezaje mpaka akafika huko? Nini challenge ya hizi kazi? Je kuna ambao Shirikisho linawaandaa kwaajili ya kuzifanya kazi hizo pia? Na wako wangapi ambao wanaliwakilisha Taifa kwenye hiyo kazi? Na je vipi kuhusu malipo yake? Ni kitu ambacho mmoja anaweza kusema ndo anataka kukifanya kama kazi? Misingi yake ikoje? Mtu anatakiwa aanzie wapi hasa? Na ni kitu ambacho anaweza kufanya kwa muda gani mpaka afikie huko ambako yeye yupo sasa? Vipi kuhusu FIFA? Huko yeye ana mpango nako? Ki ukweli yalikua mazungumzo mazuri kwangu na kwake na natumai pia yatakua na uzito flani kwako na kama si kwako ambaye ushajichagulia cha kufanya, basi hata kwa mwengine ambaye unamjua na ana interest na mpira ukamuelekeza juu ya hili. Tafadhali enjoy. 

Love, 

Salama.

Dec 15, 202201:12:42
SE7EP26 - SALAMA NA MASOUD KIPANYA | HERI KUFA MACHO…

SE7EP26 - SALAMA NA MASOUD KIPANYA | HERI KUFA MACHO…

Habibi Masoud Kipanya ni Ally Masoud Nyomwa ambaye ni LEGEND. Kwa mujibu wake alizaliwa huku kakunja ngumi na dhana yake ni kwamba alizaliwa ili awe bondia! Kwa anacho kifanya na ambacho amekua akikifanya tena kwa ufasaha kwa miaka nenda miaka rudi bila ya shaka ni UBONDIA. Hakuna ambaye atabisha juu ya hilo. Amekua akipigania mambo tele na kuyasemea mengi pamoja na kuchekesha na kuelimisha kupitia kalamu yake. Kwa mujibu wake yeye ni mbobevu katika taaluma ya kupuuza na kuchukulia mambo poa kwa kipindi sasa. Lakini pia anaamini yeye ni MTATA. Tukienda mbele na kurudi nyuma, hapo kwenye UTATA hakuna ambaye anaweza kumbishia, hasa kwa wale ambao kalamu yake imewanyoosha kwa kiasi kikubwa.

Mimi na yeye tulikutana kwa mara ya kwanza takriban miaka kumi na tisa iliyopita, wakati huo mimi mbichi hasa na yeye akiwa kashajielewa na chemchem yake ya kipato tayari ilikua inatoa neema. Mimi nilikua ndo kwanza naanza kazi ya kujishikiza pale Times FM kipindi hiko bado ilikua kule Kamata. Masoud alikua analichorea gazeti la Majira ambalo lilikua liko kwenye mwamvuli mmoja na Radio ambayo nami nilikua nimejishikiza baada tu ya kumaliza skuli. Urafiki wetu ulikuja naturally tu maana sote tunapenda kucheka. Kupitia Zuhura Yunus na Binti mwengine wa kuitwa Rahma ndo mimi naye tulifahamiana. Wakati huo yeye alikua na gari kwahiyo lifti za hapa na pale zilikua hazikauki. Pia tulikua tunaitumia gari yake kama sehemu ya ku chill na kuskiliza muziki kwenye parking za Times FM.

Huwezi kukaa kwenye tasnia moja kwa muda mrefu kama wewe si hodari na mwenye kujielewa. Moja ya vitu ambavyo naviusudu kutoka kwake ni uelewa wake wa mambo tele wa tele, IQ yake ni ya juu sana na jinsi ambavyo ana reason ndo huwa anamaliza kabisa, kama binadamu wakati mwengine ni bora kukubaliana kuto kukubaliana na kwakwe yeye wakati mwengine jinsi anavyo wachora baadhi ya matukio na watu huwa haviishii kuzuri lakini hiyo haikuwahi kuwa sababu ya yeye kuacha kufanya ambacho anakifanya na ambacho amekua akikifanya kwa muda sasa. Uelewa wake kwenye mambo ambayo yanaendelea, uwezo wake wa kuona mbali na kuweka sanaa yake hiyo kwenye karatasi kisha kutuachia sisi tung’amue maana yake kwa kweli ni kipaji cha kipekee ya sana. Mmoja anatakiwa akae tu mbali na ku admire akifanyacho na hiko ndo ambacho mimi nimeamua kufanya.

Nilikua nataka anielezee maana halisi ya baadhi ya michoro yake ambayo iliacha gumzo kwa muda mrefu lakini kwa sababu ambazo niliziheshimu alisema asingependa iwe hivyo, uhuru wa kuwaacha watu watafsiri wao ndo raha ya kazi yake ingawa yeye anajua hasa kwanini alichora na maana yake hasa ni nini! Kwa heshima ya sanaa ilibidi nikubali matokeo. Toka umeanza kumjua na kufuatilia kazi yake, mara ngapi ushawahi kuskia Masoud yuko matatani? Yaani kakamatwa au hajulikani alipo? Kwangu mara kadhaa lakini haikuwahi kuwa kizuizi cha yeye kuacha kufanya afanyacho, kuogopa je? Nadhani kama binadamu kuwa na uoga ni jambo la kawaida, ila unafanyaje baada ya hapo ndo tofauti yetu.

Episode hii inajumuisha karibu yote ambayo niliwahi kutaka kumuuliza, mengine nilipata majibu nlotaka na mengine yalitolewa mbavuni, kwa ki vyovyote vile nili enjoy sana mimi na wenzangu na kutoka kwetu tunatumai nawe uta enjoy kama ambayo nasi tuli enjoy na kujifunza kutoka kwa MWAMBA huyu.

Love,

Salama.

Dec 08, 202201:51:27
SE7EP24 - SALAMA NA LULU DIVA | UKIPATA KINYAKUE

SE7EP24 - SALAMA NA LULU DIVA | UKIPATA KINYAKUE

Kuna mambo mengi wakati mwengine ambayo yanakua yanaendelea au yalitokea kwenye maisha ya baadhi ya watu ambao huja kukaa kwenye kiti chetu chakavu na meza yenye kigae. Ila kwasababu zilizo wazi za kuwataka wasijisikie uncomfortable na pengine kuwafanya hata ambao wangependa au ambao tungependa waje nao wasijiskie hivyo ndo kanuni ambayo tumeamua au niseme niliamua kipindi huko nyuma kuifuata. Nia na madhumuni ya session zetu hizi zaidi ni kuwapa watu maua yao wakiwa hai, sisi nasi kuskiliza hadithi za maisha yao ambazo zitatupeleka sehemu fulani katika maisha yatu na hili pia humuambia kila mgeni anapokalia tu kiti chetu chakavu kabla hata camera hajiwashwa ya kwamba… Sisi tuko hapa kwaajili ya kutaka ku inspire zaidi na si kumdhalilisha au kutaka kumuangalia kwa chini yoyote kwasababu tu kabla kuna kwikwi kadhaa zilishawahi kutokea kwenye maisha yake na tuka tumia hiyo kama ‘fimbo’ kumchapia nayo. Kama mwenyewe ana simulizi yake ya ‘majuto’ ambayo wengi wanaifahamu na haikumueka sehemu nzuri na angependa kuiongelea basi ruhusa ipo, ila kama ni kitu ambacho mwenyewe hayuko tayari kukiongelea basi kuheshimu hilo ni jukumu letu NAMBARI MOJA. Najua pengine inawezakana kabisa ukaona ah basi kuna haja gani ya kuongea nao then? Haja ipo na naamini tukipatacho hutosha, bila ya kuvunjiana heshima au kuwekana uncomfortable. Ukikua zaidi utaelewa zaidi .

Lulu Diva ni moja ya majina makubwa kwenye muziki wetu hapa nyumbani na pia kwenye kiwanda cha uigizaji, hustle zake za spidi KUBWA ndo ambazo zimemfanya awe anatambulika na mambo mengine kuweza kwenda vizuri kama jahazi kwenye hali ya hewa shwari huko baharini. Ila hayo yote hayakuja tu kwasababu labda yeye ni maalum sana, au mzuri sana au anajua kuimba sana, kiukweli wake, haya yamekuja baada ya jasho tele, mchozi tele na pengine damu kiduchu.

Jinsi alivyokua ilikua kwa malezi ya Bibi maana Mzee wake alikua na mambo mengi, Mama yake nae alikua akimpambania goli kama wengi ambavyo wamekua wakifanya kwa watoto wao. Kukua kwake kwa kiasi kikubwa ni Tanga na ananisimulia kwenye apisode hii jinsi ambavyo alikua akihama vijumba na maamuzi magumu ambayo aliyafanya yeye na Marehemu Mama yake ya yeye kuja TOWN. Lulu ananihadithia pia jinsi alivyokua akijituma ili aweza kumleta Mama yake mjini baada ya kuskia ameanguka kwa mara ya kwanza. Ni binti tu ambaye ndoto yake ilikua ni kuishi na Mama yake mzazi ambaye maisha hayakua hivyo wakati anakua. Ilikua inambidi afanye mambo kadhaa mpaka alipoweza kutimiza ndoto yake hiyo ya kumleta Bi Mkubwa hospitali kwa mara ya kwanza. Mengi yalitokea na ambayo yalikua nje ya uwezo wake ila kwa Rehema za Mwenyezi Mungu kadhaa aliweza kuyakamilisha ambayo kwa mujibu wa simulizi zake naamini Mama ametangulia mbele ya Haki akiwa na roho safi kwa Binti yake.

Story ya Mama Lulu ndo ambayo kwa kiasi kikubwa ilibeba mazungumzo yetu haya, ingawa pia kwa ki upekee kabisa tumeweza kuzungumzia mahusiano yake, kazi zake, ndugu zake, maisha nyuma ya camera , kazi zake, uandishi, muziki na filamu na hakua mchoyo wa kujielezea na kutuelezea hata kidogo. Yangu matumaini pia nawe utaskiliza na kuitimaza kwa MAKINI na kwa kiasi fulani utaweza kuelewa baadhi ya mambo ambayo yatakufanya hata ukimuona uwe na heshima fulani kwa Binti huyu.

Tafadhali Enjoy.

Love,

Salama.

Nov 30, 202201:15:15
SE7EP25 - SALAMA NA DORIS MOLLEL | HALF WOMAN, HALF AMAZING

SE7EP25 - SALAMA NA DORIS MOLLEL | HALF WOMAN, HALF AMAZING

Doris Mollel kwa kuanzia tu tuanze na jina lake, ni zuri lenye kukumbukwa ki rahisi, yeye mwenyewe pia ni mrembo na mkarimu, sana. Roho yake ni kama rangi yake, nyeupe na kwa bahati Mimi namfahamu yeye kiasi kwa kupitia rafiki zangu ambao yeye anafanya nao kazi na pia ana mahusiano nao mazuri, sana. Pia namfahamu mume wake ambaye tukianza shindano la kumtafuta nani mkarimu kati yao tunaweza kukamaliza kwa suluhu. Huwa naamini Mwenyezi aliwakutanisha ili kwa pamoja waweze kufanya makubwa kwaajili yao na familia zao na jamii ambayo imewanzunguka ambayo kwa kiasi kikubwa ina uhitaji wa yale ambayo wao wameyaona wanaweza kufanya jambo ili yawe mepesi.

Sasa tuanze kwa vipi Doris amekua akifanya ambayo anayafanya sasa ambayo baada ya kufanya kipindi hiki mengi ambayo aliyaongelea kama ya Serikali ya Uganda kumpa tuzo na kumkaribisha nchini mwao ili aweze kushirikiana nao bega kwa bega kwenye suala zima la kuwaokoa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani ‘NJITI’ na hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia S. Hassan kutoa MILIONI 70 kwaajili ya kuchangia mfuko wake wa Doris Mollel Foundation. Yeye alikua anataka tu kufanya kitu kwaajili ya kuisadia jamii yake, ananiambia wakati analizungumzia hilo huku akitafuta jambo la kufanya ndipo Mama yake alipomfugua macho kwa kumuambia masuala ya watoto njiti, taa iliwaka sasa baada ya Mama yake kumkumbusha kwamba hata yeye alizaliwa kabla ya wakati. Alipoambiwa hivyo hakukua na kurudi nyuma tena baada ya hapo.

Ananisimulia vikwazo ambayo aliwahi kupata mwanzo kuanzia nyumbani mpaka kwenye kutafuta hizo pesa ambazo zinasaidia mpaka leo hii, Doris ananihadithia jinsi ambavyo alipata bahati ya kuwa na watu ambao wamemsapoti na wanamsapoti mpaka leo kuanzia nyumbani kwa mume wake. Mtu ambae ndoa yao ilikua changa kuanza kuwa na vikao na watu mbali mbali mpaka usiku wa manane inamtaka mtu muelewa sana kuweza kuamini na kuyaacha mambo yaende. Mumewe alikua huyo mtu. Kwa ambao walimpigia simu mara ya kwanza baada ya kuona anchojaribu kufanya, watu kama Asas wa kule Iringa na wengine ambao wamekua wakijitokeza siku baada ya siku. Anakumbuka na anajua kwamba kutokata tamaa kwasababu ya changamoto kadhaa ndo ambapo kunamfanya awe ni mmoja ya watu wanao heshimika zaidi kwa mchango wake kwenye jamii yetu.

Binafsi naamini huu ni mwanzo tu wa mazuri mengi ambayo binti huyu halisi wa ki Tanzania anajaribu kufanya. Sekta ya kulea watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati inahitaji hela nyingi na kwasababu ambazo Mimi na wewe hatuzijui kumekua na vifaa VICHACHE sana vya kuwahifadhi watoto hao mara tu wanapo zaliwa. Doris na Foundation yake amekua akipigana vita hiyo kuhakikisha vifaa vinapatikana sio mjini tu, hata mikoani ili kuokoa maisha ya watoto hawa ambao wengine huishia kwenye debe la taka kwasababu tu walizaliwa kabla ya wakati wao.

Yangu matumaini utamuelewa na utapata nafasi ya kumfuatilia na kama utakua na lolote ambalo unaweza kuchangia basi yuko kwenye mitandao ya kijamii maana siku hizi kumpata mtu na kujua ambacho anakifanya imekua rahisi kupitia mitandao hiyo. Mimi najivunia sana yeye na yangu matumaini atafanikiwa sana kwenye sekta hii kama nasi tutaweza kumsaidia pale panapowezekana.

Tunahitaji kina Doris tele kwenye jamii yetu maana vya kusaidia viko vingi.

Yangu matumaini episode hii itasaidia kukufungua macho kwenye mengi ambayo jamii yetu ina uhitaji.

Love,

Salama.

Nov 24, 202201:15:48
SE7EP23 - SALAMA NA WALTER CHILAMBO | HABA NA HABA

SE7EP23 - SALAMA NA WALTER CHILAMBO | HABA NA HABA


Pengine jina la episode hii linaweza likakupa muangaza kidogo wa story fupi ya maisha ya mgeni wetu wa wiki hii kwenye kiti chetu chakavu na meza ya kigae ambaye leo hii tayari kashaona, tochi ya maisha kwake inamulika tu vizuri na mbele anapaona. Huyu ni Walter Chilambo ambaye miaka tuseme 14 iliyopita alikua hana uhakika wa chakula chake cha siku tu achana na sehemu gani atalala. Ruka ruka ya kule na huku na bahati ya kupendwa alonayo na ambayo inaendelea mpaka leo naamini inakuja kwasababu ya ukarimu wake na hii ndo silaha yake yenye makali ambayo inampeleka mbali mpaka leo hii. Kama mtoto wa kiume ambaye unatakiwa kwenda kujitafuta ki maisha Walter nae ilibidi afanye yale yale ambayo si watoto wa kiume tu ila wengi wetu tumefanya ya kutaka kwenda kutafuta chako, na yeye aliona basi bora afanye hivyo. Safari ya kuja town kutoka mkoani anatuhadithia kwa upana kwenye episode hii. Mtu ambaye alimpokea ni mwana tu ambaye alienda nae shule moja, stop ya kwanza? Keko Magurumbasi. Na si kwamba alikua hana Ndugu hapa Dar es Salaam yeye alijiamulia isiwe hivyo, ilikua ngumu kumshashiwi Mama yake ambaye alitaka kujua ramani nzima ya mwanae ambaye alikua anakuja mjini kwa mara ya kwanza. Baada ya kufanikiwa kushawishi Mama Walter, kijana alipewa nauli na ananiambia by the time anafika Dar alikua na shilingi ELFU MOJA TU kwenye mfuko wake, hapo ni Ubungo kwenye stendi ya mkoa. Imani yake kwa Mungu wake pia ni silaha ya pili ya Ndugu Walter Chilambo. Hii ndo ambayo kwa mujibu wake imemsaidia kumvusha na mengi, maisha huko Keko hayakua mazuri, sikutaka kutumia neno si kama alivyo yatarajia maana hata yeye hakua na matarajio yoyote kwasababu alikua hajui anakutana na mazingira gani wakati anaenda kwa mwanae huyu aliyesoma nae Sekondari ambaye walikua na majina ya Baba yanayofanana. Mwenzetu anaitwa Michael. Alikaa pale huku akiwa anajaribu kuji tafuta ila kila anachogusa kilikua cha moto. Ananihadithia jinsi alivyoanza kufanya kazi za kila siku ili angalau apate hela ya kula, kule kwa Mama alikua anajifanya kama kila kitu kinaenda vizuri kwahiyo hata vimzinga vidogo vidogo vilikua haviendi. Ulipofika wakati wa yeye na mwanae Michael kufunguana mashati maana alikua ashakaa saana na hana dira nzuri hapo sasa ndo kila kitu kilianzia. Unadhani mmoja anaweza kuwa na bahati kiasi gani kwamba mtu ambaye aliombwa amhifadhi kwenye ghetto lake wakati yeye anatafuta ustaarabu mwengine kuwa ni Ndugu yake? Pengine hii hutokea kwa wenye BAHATI TU, pengine Walter ni mmoja ya watu hao maana baada ya kujulikana hilo ndo angalau kukawa na ahueni ya kuwa na uhakika wa sehemu ya kuegesha mbavu, hii ni moja ya sehemu ilonisisimua kwenye simulizi yake, imagine mtu anavyokua kapigika alafu kutoka ambako hakujulikani mtu ambaye ameombwa akuhifadhi kwa muda anatokea kuwa ni Ndugu yako, hii ni Mwenyezi Mungu pekee ndo ambaye anaweza KUTENDA na kama utakua ushawahi kuishi kama ndege ambaye hajui analala wapi basi wewe utaweza kuelewa zaidi hapa. Walter Chilambo ni mshindi wa Bongo Star Search wa mwaka 2012 na baada ya kushinda alianza safari yake ya muziki rasmi. Safari yake haikua ya urahisi kama ambavyo naamini alitarajia au sote tulidhani. Kiwanda cha Bongo Flava ki usalama tunaweza kusema kina wenyewe na ukiwa mpya kabla hujajua fagio lipi ndo linafaa kusafishia wapi basi kazi utakua nayo. Kwa Bwana Chilambo ambaye alishinda taji na pesa hakukua na tofauti kabisa. Neema kwa upande wake ilianza kuonekana baada ya yeye kuamua kufanya mziki wa kumtukuza Mungu na baada ya hapo mengine ni story tu. Kwahiyo NINI hasa kilimfanya afanye maamuzi hayo? Kwenye kipindi ambacho kila mmoja ameamua kuimba nyimbo za mambo ya kitandani na mambo ya ndani je yeye kwanini aliamua kubadilisha gea? Maana Kama sauti anayo na kuandika anajua sasa sababu ni nini? Na pia wasiwasi wangu uko kwenye baada ya ‘kutoboa’ huko aliko na kupata umaarufu na sifa tele hatorudi tena huku kwenye kuimba nyimbo za kuachwa na kupendwa na kutendwa? Ana uhakika kiasi gani? Ukichukulia kama k

Nov 17, 202201:06:43
SE7EP22 - SALAMA NA ANNA TIBAIJUKA | LA PROFESSEUR

SE7EP22 - SALAMA NA ANNA TIBAIJUKA | LA PROFESSEUR

Nilipoandikiwa ujumbe mfupi na Edwin Bruno ambaye ni mkwe wa Professor kwamba Mama amekubalia kufanya kipindi na sisi siku hiyo ya Jumapili akishatoka church nilihisi kama naota. Mwenyezi Mungu anajua kwa kiasi gani tumekua tukitaka kufanya maongezi nae kwenye kipindi chetu. U busy wake na pengine mara nyingi kutokuwepo Dar es Salaam napo palikua panaleta ugumu, nyengine ilkua ni tarehe zetu za kufanya production na availability yake zilikua zinapishana sana. So unaweza ukaelewa excitement ambayo nilikua nayo baada ya finally samaki kujaa kwenye ndoana.

Professor Anna Tibaijuka ni LEGEND miongoni ma magwiji kwenye nchi hii kwa kazi yake na usomi wake na uzazi wake na kujibeba kwake. Kazi mbali mbali ambazo amewahi kuzifanya na kuliwakilisha Taifa hili zinajizungumza kwa sauti kubwa. Ila Safari yake mpaka anafikia kwenda kufanya kazi kwenye Taasisi kubwa duniani hakukumdondokea tu miguuni. Usomi wake ambao aliupambania toka akiwa mdogo na kupata ushirikiano kutoka kwa Marehemu Baba yake ndo kila kitu. Enzi ambazo mtoto wa kike alikua anaandaliwa kuwa Mama wa nyumbani, Baba yake aliamini zaidi kwenye kumpeleka mtoto wake shuleni na kwa mujibu wa Mama Tibaijuka Baba yake alikua aliwasisitiza wazee wenzake kufanya hivyo maana dunia ndo ilikua inaelekea huko, kuna ambao walimsikiliza na wengine ambao waliona anapoteza tu pesa na muda.

Mama Tibaijuka na Mimi tuliongelea kuhusu gharama za elimu enzi hizo Mimi nikidhani elimu “ilikua bure” pasi na kujua elimu kipindi hiko ilikua ghali pengine kuliko sasa na ukichukulia shule zenyewe zilikua mbali kweli kweli. Ananiambia pia suala la yeye kutaka kutomuangusha Baba yake ambaye baadhi ya watu walikua wanamcheka kwa kumpeleka Anna shuleni na kuingia gharama zote hizo. Pia ananiambia kuhusu Mama yake kufanya kazi zaidi ili masuala ya nyumbani aweze kuyafanya yeye ili kumsaidia mumewe ambaye pesa yake karibia yote alikua akilipia elimu ya Binti yake.

Mama Anna pia ananisimulia humu jinsi ambavyo aliposwa alipokua kidato cha tano na mchumba ilibidi amsubiri mpaka alipomaliza Chuo Kikuu. Nili enjoy kila sekunde ya maongezi haya ambayo kwa kiasi kikubwa naamini yatakua na faida kwetu sote. Ananihadithia pia jinsi ambavyo alienda Sweden na mumewe ambayo alikua huko kikazi na jinsi ambavyo alipata nafasi ya kusoma Chuo Kikuu BURE na ni nafasi ambayo aliipokea kwa mikono miwili na kuhakikisha hafanyi makosa.

Mama Anna ameshaifanyia Dunia hii mambo tele ya kimaendeleo wakati akifanya kazi zake UN na baada ya hapo alirudi nyumbani na kukifanya kazi Chama cha Mapinduzi kama Mbunge wa Muleba Kusini na Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi. Hapo kwenye uwaziri sasa… Kulikua na mengi yaliyotokea wakati yeye yuko kwenye cheo hiko na ambayo kwa ki ufupi tu tuliyajadili kwenye meza yetu. Mama Anna yuko na Respect ya hali ya juu kwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye kwa kiasi kikubwa alimfanya Professor Tibaijuka arudi nyumbani na kulifaidisha Taifa na yale alojifunza wakati anafanya kazi huko kwenye Umoja wa Mataifa.

Yangu matumaini utaokota kadhaa kwenye maongezi yetu haya na kwa kiasi flani yatakusaidia kwenye maisha yako. Tafadhali enjoy pia.

Love,

Salama.

Nov 10, 202201:01:36
SE7EP21 - SALAMA NA BILLNASS | MJUKUU

SE7EP21 - SALAMA NA BILLNASS | MJUKUU

Katika pita pita zangu siku si nyingi nilimsikia mtu akimzungumzia mgeni watu wa wiki hii kwamba ni ‘Jay Z’ wa Bongo na si kwasababu kamuoa mmoja wa wasanii hodari wa kike na ambao wako juu ki muziki, ila pia akili yake ya kibiashara kwa kiasi kikubwa imemfanya yeye aone hivyo. Kwa ufahamu wangu niliambiwa na kushuhudia suala la maneno na mawazo ‘kuumba’. Pale mtu au watu wanapo kuona na ukichanganya na juhudi zako na nia na madhumuni ya wewe kutaka kufika pale basi mengine kutimia huwa ni suala la wakati tu.

Hivyo pia ndivyo ambavyo mimi namuona Ndugu William Nicholaus Lyimo almaaruf Bill Nass. Mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho ni miaka kama sita au saba iliyopita wakati nafanya kipindi cha Ngaz kwa Ngaz special edition. Ambacho mimi na Josh Murunga tulikua tunafanya ilikua kuwapa nafasi wasanii hodari kuwa ma host wa countdown hiyo ya ngoma zao kali 20 kwa wakati huo na kuzitolea maelezo yake. Kwa Bill Nass ilikua kama kumtafuta Kuku tu, yaani RAHISI sana. Alikua natural wataalam wanasema, kuanzia matamshi (haya wengi huwashusha hadhi kwa kiasi flani) mpaka swagg ambayo mtangazaji anatakiwa awe nayo kwake ilikua ipo. Kuvaa kwake, kuheshimu wakati na kuskiliza maelekezo na kisha kuyafanyia kazi ilikua 100, na mimi kwenye hili nilikua mtazamaji tu, kazi kubwa aliifanya Ndugu Josh akiwa kama Director. Yangu matumaini Bill Nass siku moja atataka kufanya kitu kama kile maana kitamfaa mno na itakua moja ya income zake nyingi ambazo anazo.

Kwake yeye kuamua kumuoa mmoja ya wasanii hodari wa kike ambaye ana mashabiki wengi na pengine wengi wao ni wanaume nadhani lilikua si amuzi mdogo kwao wote wawili. Wawili hawa mahusiano yao yalikua hadharani kwa sote kuyaona na kuwa na maoni nayo. Kuanzia ku leak kwa video yao ya faragha mpaka mahusiano ya mkewe na Marehemu Ruge, kila kitu kilikua nje nje. Je haya yaliathiri au kuyajenga mahusiano yao kwa kiasi gani?

Vipi kuhusu suala la Marehemu Godzilla ambaye kulikua na shutma kwamba alikua anauiga style yake na baadhi ya Radio zilikua zinampa nafasi yeye ili kumficha Zilla? Na je suala la kifo chake ambalo lilimleta yeye karibu na mtoto wa Zilla? Hii ilikua inamsumbua vipi wakati watu wanasema hivyo? Na je alikua anaona jinsi ambavyo ilikua inamsumbua Zilla?

Ukiachana na muziki Nenga pia ni mfanyabiashara mzuri tu ambaye amekua akitumia jina lake ipasavyo ili kuweza kujitengenezea kipato cha pembeni ambacho ni cha uhakika zaidi kuliko mziki ambao anafanya. Nna uhakika na yeye anajua kwamba ana uhakika wa kuuza electronics zaidi kwa mara nyingi kuliko uhakika wa kuwa na hit song nyingi kwa mwaka. Na hiyo haimaanishi kama yeye si msanii HODARI ila zaidi kwenye suala la wimbo kuwa mzuri lakini watu wasiupokee kama matarajio yanavyokua.

Humu pia tulichambua kiasi kuhusu jina lake ambalo amelirithi. Majukumu, biashara, mapenzi, urafiki, usia na familia.

Ningependa u enjoy kama ambavyo sisi tu enjoy wakati tunaongea.

Love,

Salama.

Nov 03, 202201:15:49
SE7EP20 - SALAMA NA CAROL NDOSI | ANAMEREMETA

SE7EP20 - SALAMA NA CAROL NDOSI | ANAMEREMETA

Ushawahi kuwa na mtu ambaye mnafahamiana vizuri miaka nenda na miaka rudi na hata pengine kwa u busy wa maisha zikapita siku hamjaongea lakini unajua yuko sawa yeye na Familia yake na mambo yanaenda vizuri, na kama isingekua hivyo basi ungekua ushajua? Ambaye unajua kukiwa na situation flani basi yeye anatafanya jambo flani na kuzima au kuwasha moto, na kama kuna neno umeambiwa kasema unajua kabisa ni kweli au si kweli? Au kama una suala unataka kulifahamu vizuri linalohusu mambo fulani na jibu ambalo atakupa yeye ni la 100 na hatapindisha hata kidogo? Basi huyo ni Carol Moses Ndosi kwa Salama Jabir yangu.

Lini tulikutana? Yoh 😃! Wakati sote tunafanya kazi IPP Media,Carol alikua rafiki wa Tabea Kaduri ambaye alikua nae kwenye channel ya kiingereza ya 101.4. Si unamjua Carol na kizungu? Then ITV then EATV, mimi na Carol tukaja ku click zaidi kwasababu tabia zetu nyingi (za ujana) zinafanana. Pia tulienda wote Makongo Secondary School ingawa mimi huko simkumbuki maana mambo yangu yalikua mengi kiasi. Pia mimi ni Dada yake ki umri. Kuna story moja ya Carol ya kujifunza gari bila ya kunipa taarifa. Siku moja kaibuka tu ITV nje na kuniambia twenzetu kwa Kiula huku yeye ndo suka bila ya kujua lini hasa alijifunza kuendesha hilo gari! Nadhani hii ni moja ya memory nzuri kati yetu. Ukiachana na kwenda Chang’ombe kumfuata Steve Mbobo na gari letu ambalo AC Mungu ndo anajua,foleni ya Keko na sisi ilikua inafahamiana vizuri. Tumeishi na tunaendelea kuishi Alhamdulillah, na mambo yetu? Ah mambo yetu Allah anaendelea kuyabariki sana. Tunashkuru kwa kweli.

Kukua sasa ndo huku, kila mmoja kajiajiri kwa kuyafanya yale aliyo jichagulia. Carol kama wengi mnao mfahamu na ambaye humu kwenye maongezi yetu ya kwenye kiti chakavu na meza ya kigae yatakufanya umfahamu zaidi kwamba ni JEMBE. Mpambanaji kabisa ambaye nae kama binadamu mwengine wakati mwengine humfika hhaapa na pengine kutaka kukata tamaa. Lakini uzuri ni kwamba ana nguvu na kiu ya kutaka KUENDELEA na KUSHINDA, pengine hiyo ndo silaha yake NAMBARI WANI. Kwa utashi wake ameweza na anaendelea kuweza kuwafunza mambo wengi wetu juu ya masuala ya ki mtandao na kujielewa binafsi. Wakati wa Nyama Choma Festival Carol na kikosi kazi chake aliweza kufanya kazi iliyo tukuka ambayo ililifanya tamasha hilo liwe ni moja ya matamasha BORA kabisa ambayo yashawahi kutokea hapa Tanzania. Mitihani ambayo aliwahi kukutana nayo wakati tamasha hilo likiwa linaendelea ambayo mengine ilikua ya Mungu na mengine ya Binadamu ni Carol mwenyewe na team yake ndo ambaye anaweza kuelezea na kwa kiasi kiduchu sana, amegusia kwenye maongezi haya.

Heshima zangu kwake anazifahamu ingawa wakati mwengine tunakubaliana kuto kubaliana kwenye baadhi ya mambo lakini urafiki na u Ndugu wetu utabaki pale pale. Mimi na yeye tushafanya mengi, tushaona mengi, tushajifunza mengi na bado tunaendelea kufanya hivyo. Na nia hasa na madhumuni ya episode hii ilikua kutaka wewe unafahamu Ndugu yangu huyu zaidi. Na ningetamani sana kuweza kuyaweka wazi yooote na majina yake ila kwa staha na heshima, kwa leo tuishie hapa.

Yangu matumaini kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusaidia kwenye safari na vita zako binafsi.

Keep going.

Love,

Salama.

Oct 27, 202201:05:00
SE7EP19 - SALAMA NA DITTO | TUNER

SE7EP19 - SALAMA NA DITTO | TUNER

Lameck Ditto Sr ni Baba, Mwalimu, mwanamuziki, muandishi, mentor, mume na zaidi ya yote ni mwana tu ambaye maisha alopitoa kipindi anakua hayajawahi na wala hayatawahi kumsahaulisha yeye ni nani na wapi ambapo ametokea na wapi anataka sana kuelekea maana huko ndo kwenye kesho yake, na kwa kumsikiliza ambavyo nimemsikiliza, kesho yake anaithamini sana na amekua akiiandaa vizuri ili hata siku moja asije akakwama na kuanza kuishi maisha ya jana ambayo yalikua si mazuri hata kidogo.

Yeye na Baba yake mzazi walikutana kwa ‘bahati mbaya’ tunaweza tukasema hivyo maana wakati yuko zake Morogoro akiendelea na maisha ya kuishi yeye na Kulwa huku wakijilea wenyewe, Ditto au Dotto ananihadithia vile ambavyo Rafiki yake aliweza kumkutanisha na Mzee wake bila ya yeye kutegemea.

Alikua ananiambia vile ambayo ilikua inabidi apambane kupata ya kula na pa kulala baada ya kuja jijini Dar es Salaam na haya yote ni baada ya yeye tayari kuwa umeshatoka na WATU PORI enzi hizo na hapo pia ni baada ya kupata nafasi ya kurekodi album moja na producer PFunk enzi hizo, PFunk huyo huyo ambaye alikua akilitikisa TAIFA kwa kazi nzuuri alizokua akifanya na wasanii kadha wa kadha ikiwa pamoja na Juma Nature.

Lameck anakumbuka jinsi alivyokua analala ndani ya kiduka kidogo cha mwanawe mmoja ambaye alishamsomesha ili amstiri ki hivyo, alivyokuja Dar alikua anakaa kwa mwanae mmoja ivi na mkewe ila baada ya ahadi za album kutoka na kwamba mambo yatabadilika kugonga mwamba, Lameck ilibidi atafute ustaraabu mwengine.

Nilitaka kujua kama hiyo ndo ilikua lowest moment ya maisha yake? Au kifo cha Mama yake? Au Mamu kukataa album yake kwa kusema haikua na kiwango kile?

Sasa ni Baba na mchumba wa muda mrefu wa Binti mmoja ambaye nae alikutana nae ki ajabu ajabu tu na ambaye pia alimzungusha sana kabla hajanasa kwenye ndoana. Baba wa mtoto ambaye Mimi baada ya kukufanya nae mazungumzo nilikutana nae uwanjani akiwa ameenda kumuangalia Lameck Jr akifanya yake kwenye moja ya mechi za soka za shule ambayo anasoma. Kwenye meza aliniambia moja ya ahadi ambazo amejiwekea ni kuhakikisha yuko pale kwaajili ya mtoto wake, jambo ambalo yeye hakuwahi kulipata mapema.

Mwanzo nilikuambia yeye pia ni muandishi, muandishi wa mashairi ya muziki na pia ni muandishi wa matangazo, kazi ambayo anasema Marehemu Ruge Mutahaba ndiye ambaye kwa kiasi kikubwa alimuelekezea huko. Na mentor wake mwengine ni Ndugu Ruben Ncha Kalih ambaye kwa asilimia KUBWA amempika na akapikika.

Tulizungumzia pia umuhimu wa mmoja kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha kupata pesa, kuweza kukabiliana na MSIMU ambao unakua huna wimbo (au kazi) lakini bado ukaweza kuishi, kuhusu maamuzi ya yeye kwenda THT wakati tayari alikua ARTIST ambaye ameshajijenga. Tuliongea pia kuhusu Ruge, Barnaba, Amini na mambo mengine tele. Binafsi nilikua na wakati mzuri sana wakati tunaongea haya na yangu matumaini itakua hivyo kwako pia.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Oct 20, 202201:20:36
SE7EP18 - SALAMA NA FAROUK KAREEM | SAILOR

SE7EP18 - SALAMA NA FAROUK KAREEM | SAILOR

Hii nayo ni moja ya zile ambazo ziliuliziwa sana na kwa muda mrefu nasi kwa upande wetu tumekua tukiifukuzia tuweze kukaa na mwamba huyu hodari kutoka Zanzibar. Mimi mwenyewe ambaye nimekua nikifanya kazi kwenye kiwanda hiki cha burudani nilikua na hamu ya siku moja kuwa kwenye meza moja na Ndugu yangu huyu, kuweza kumtazama usoni na kumuuliza yote ambayo nilikua nataka kumuuliza kwa kipindi kirefu sana. Maana hata mimi nimekua nikimsikiliza miaka nenda miaka rudi na siku zote emeemdelea kutuhabarisha kwa sauti ile ile na spidi ile ile. Ukiskia mtu ameweza kuwa bora toka siku ya kwanza basi moja ya mifano hai ni Farouk Kareem wa ITV na Radio One. Nikiwa mzanzibari wa kuzaliwa, Farouk amekua ni moja ya watu ambao nimekua nikiwaskiliza na kuwaheshimu sana. Mchango wake kwenye tasnia ya uwandishi wa habari na kuziripoti habari hizo Taifa zima unalijua, toka enzi zile za kipindi cha Spoti Leo cha Radio One ambacho yeye alikua alishiriki kama reporter kutoka Zanzibar na baadae na yeye akajiingiza katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uongozi kwenye Chama cha Mpira cha Zanzibar yaani ZFA na akapata na katika watu ambao walipiga kazi iliyo TUKUKA enzi hizo na ambayo iliacha alama basi Farouk ni mmoja wapo. Nani aatasahau kama moja ya idea zake ilikua ile ya kutaka Zanzibar iwe na kiti chake kwenye Shirika la Mpira la Afrika na la Dunia yaani CEFAFA na FIFA. Farouk Kareem alikua ndo injinia wa kutaka hilo LIWEZEKANE. Mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wawili tu na wote wa kiume, Farouk Karim ni Kaka wa mmoja kati ya ma Pilot hodari na wa muda mrefu ambao hii nchi imeshawahi kuona ambaye na yeye sasa ana mtoto pia ambaye naye ni Rubani. Kaka huyo Kapten Arif Jinnah na mwanawe First Officer Amour Arif. Ki ufupi familia yao imejaa watu wa kazi kabisa. Naamini si wengi ambao tulikua tunayajua mahusiano hayo ya wawili hawa ambao kila mmoja wao amekua akiandika historia yake kwa upande wake. Farouk ni Baba wa watoto kadhaa wa Kike ila miaka si mingi sana Allah pia nae kampa mtoto wa kiume. Kwenye episode hii tumezungumzia familia na majukumu, tumezungumzia jinsi mmoja anavyoweza kutafuta kwa njia zake na wazazi nao wakitoa baraka zao basi hakuna ambalo linaweza kushindikana kama tu nia na madhumuni yapo. Anakumbuka jinsi ambavyo alimaliza skuli na kisha akawaambia wazazi wake kwamba yeye anataka kuwa BAHARIA na wao WAKARIDHIA. Anasema kipindi hiko kulikua na wimbi la ma Seaman tele ambao walikua wakirudi likizo nyumbani Zanzibar wanakua wako ‘vizuri sana’ na hiyo ni moja ya mambo ambayo yalimvutia sana. Na wazazi wake waliridhia na kuhakikisha kijana wao anatimiza ndoto zake kwa kumuwezesha. So, kwenye habari nako alifikaje? Hii ni moja ya episode nzuri sana ambazo nimewahi kufanya msimu huu na yangu matumaini nawe uta enjoy kama ambavyo sisi tuliburudika wakati wa mahojioani haya. 

Love, 

Salama.

Oct 13, 202201:23:40
SE7EP17 - SALAMA NA ROSE MUHANDO | NIPE UVUMILIVU

SE7EP17 - SALAMA NA ROSE MUHANDO | NIPE UVUMILIVU

Katika binadamu ambao walinipa wakati mgumu na kusubiri kwingi kabla ya kuja kukaa kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu basi mmoja wao ni Rose huyu wa Muhando. Upatikanaji wake ni kama ukitaka kumuona SIMBA mbugani, lazima uamke asubuhi na mapema au uwe na bahati ya mtende kama ambayo sisi tumepata. Ingawa tulisubiri kwa masiku tele na miezi tele katikati ya mwaka huu tuliweza kumpata na kukaa nae chini ili tuweze kuzungumza nae.

Rose ni wa moto sana, kalenda yake imejaa safari tele za nje na ndani ya nchi, anazunguka mara kwa mara kwaajili ya kutoa elimu na burudani kwa watu wengi ambao nao pia wamekua wakimgojea kwa hamu na kwa masiku tele. Kipaji chake cha kipekee ndicho ambacho kimemfanya awe maalum miungoni mwa wasanii wanaofanya muziki wa Injili na uzuri wake mwengine ni kwamba amekua akitoa huduma hiyo kwa miaka mingi bila ya ‘kuchuja’.

Sasa nini hasa siri ya mafanikio hayo?! Ukiachana na panda shuka tele ambazo Rose amepitia toka akiwa na umri wa miaka 6, kukata tamaa ni jambo ambalo halipo kabisa katika mambo ambayo huwa anayawaza. Pengine kujiuliza kwanini na anatokaje kwenye hilo zito alilo nalo linaweza likawa ndo swali, ila kusema kwamba hatoweza au haiwezekani hilo jambo kwenye kitabu chake au kichwani chake huwa halipo kabisa.

Ukiskiliza kwa makini maneno ambayo yanatoka katika mdomo wake utagundua Rose ni mmoja kati ya wanawake jasiri sana ambao wamewahi kutokea katika kiwanda hiki cha Sanaa hapa Tanzania. Ukimuangalia macho yake, mikono yake ambayo imejaa makovu na nna uhakika pia kuna sehemu nyengine kwenye mwili wake pia zimejaa makovu lakini hatukuweza kuona unaweza ukapata tu idea ya makubwa na mazito ambayo amepitia na ambayo yameacha makovu makubwa tu si mwilini mwake tu bali hata kwenye moyo wake. Ananihadithia kwenye episode hii jinsi ambavyo watu walikua wanamuadhibu ki mwili na ki akili ikiwa ni pamoja na kupigwa, kuchomwa moto, kukatwa na kunyang’anywa mali zote ambazo amewahi kutengeneza tokea wakati anaanza muziki ila hayo yote hayajawahi kumkatisha tamaa wala kumrudisha nyuma.

Rose anaamini na aliamini kwamba ana uwezo wa kuvipata vyote ambavyo watu walimdhulumu kwenye kipindi flani kwenye maisha yake, aliamini hakuna ambaye anaweza kumnyang’anya kipaji ambacho Mwenyezi Mungu amempatia na kwa kupitia hiko kipaji na akiwa hai na mzima basi vyote ambavyo aliwahi kuwa navyo na vikapotea basi alikua na uwezo wa kuvirudisha na ni kweli, kuvirudisha ameweza na vimekuja maradufu yake.

Simulizi zake za safari yake toka siku ya kwanza alipokua mdogo nyumbani kwa Baba na Mama yake huko kwao Morogoro wakati anaumwa ni moja ya vitu vya kufikirisha sana ambavyo nimewahi kuvisikia toka tumeanza kukalia kiti chakavu, na yangu matumaini maongezi haya kwa kiasi kikubwa yatakupa ile vibe ambayo huwa naizungumzia kwenye intro ya kipindi chetu hiki.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Oct 06, 202201:20:02
SE7EP16 - SALAMA NA ZAHIR ZORRO | KIMULIMULI

SE7EP16 - SALAMA NA ZAHIR ZORRO | KIMULIMULI

Zahir Ally Zorro ni mkongwe wa muziki wa dansi na kwa habari ambazo nimepata ni kwamba enzi zake alikua wa moooto sana tena kwenye kila nyanja, kuimba, kuandika, kupiga gitaa na mpaka uvaaji, alikua handsome boy sana na ulimbo kwa kina Dada enzi hizo. Utashi na ucheshi na u sharp wake ndo ambao ulikua unamfanya asimame PEKEE kwenye kadamnasi ya wanamuziki wengi wa kipindi hiko. Naomba nikukumbushe pia kwamba enzi hizo zilikua pia si za kuzichukulia poa kabisa, maana ushindani wa bendi na vipaji binafsi ulikua wa hali ya juu sana, na yeye kama yeye alikua moja ya wale WAKALI wa kipindi hiko. Kama muajiriwa wa Jeshi Mzee Zahir alikua shujaa wa aina yake enzi hizo za ujana wake, kama askari alikua akijituma na ndo maana hakua na cheo cha kinyonge, na kama muandishi na muimbaji na mpiga gitaa pia alikua na nafasi yake ya kipekee. Ukimuangalia hata rangi yake imekaa ki chotara na kwenye mazungumzo haya ana nikumbushia jinsi ambavyo Baba na Mama yake walikutana na ambavyo yeye alizaliwa. Interest yangu zaidi ilikua jinsi ambavyo yeye kama Baba ameweza kuwakuza watoto wake wawili ambao nao wamekuja kuwa wanamuziki wazuri tu tena, Marehemu Maunda Zorro ambaye alifariki mapema mwaka huu (Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na Amrehemu) na Kaka yake Banana Zorro. Wakati wa kuanza Banana ndo alionekana kuwa angekua super star zaidi ila Maunda nae alipoikamata reli yake kila mtu alimfahamu vizuri. Malezi yao baada ya Marehemu Mama yao nae kutangulia mbele ya haki wakiwa bado wadogo naamini ilikua mtihani mkubwa kwa Mzee Zorro. Ila kwa Rehema za Mwenyezi Mungu Mzee huyo aliweza na ameweza kuhakikisha watoto wake wanakaa kwenye mstari ulio nyooka na kufanya mziki mzuri na kwa heshima na taadhima. Kwenye maisha yangu ya kazi hii nimeshawahi kukutana na Mzee Zorro ila hatukuwahi kufanya maongezi kama haya ingawa nyuma ya ubongo wangu siku zote nilikua nataka kufanya hivyo, na wakati mwengine nilikua nawaza hata ingekua viti VITATU upande ule yaani Baba na watoto wake wawili, kisha nikaona tutakosa kinaga ubaga nyingi, yaani hatutawafaidi sana kama tukiamua kufanya hivyo maana kati ya watatu hao kila mmoja ana story zake ambazo anafaa kupatiwa wasaa wake. Kwa bahati mbaya Maunda alitangulia mbele ya haki na wakati kwa upande wetu ulifika kwa sisi kutaka kukaa chini na Mzee Zorro ili tuyajue yake na kutaka kujifunza kutoka kwake. Mimi na Director wangu wa episode hii tulikua na wakati mgumu kiasi maana pengine tulitaka zaidi ya ambacho tuliweza kupata na hilo Mimi na Alex (Director wangu) tumekubaliana kwamba imetokana na kuondoka kwa Maunda, tunaamini toka Maunda amefariki Mzee Zorro hajarudi katika hali yake ya kawaida, na inaeleweka maana yule hakua tu Binti yake, alikua ni rafiki yake wa karibi saaaana pia. Mzee Zahir alikua analala na Maunda na Banana chumba kimoja mpaka siku chachu tu kabla ya Maunda kukua, na hiyo ilikuja baada ya Banana kumuambia Mzee wake kwamba pengine sasa umefika muda wa wao kulala tofauti. Ananiambia katika episode hii kwamba yeye waala hakua anaona tatizo lolote juu ya hilo maana wenyewe walikua wanaishi tu kwa upendo na maelewano ila baada sasa ya Banana kusema ndo hata yeye alipoona ni kweli muda wa kupeana faragha kwa kila mmoja kuwa na sehemu yake ulikua ushafika. Kwa mtu ambaye walikua wanaonana karibu kila siku na kuongea sana hata baada ya Maunda kuhamia kwa mtu wake ukaribu wao bado ulikua wa karibu sana. Mimi namuombea Mzee Zahir Ally Zorro wepesi katika kipindi hiki kigumu ambacho anapitia na In Shaa Allah arudi katika hali yake ya zamani ya ucheshi na bashasha tele na kwa hii ambayo tumeweza kufanya naye itakupa ufahamu wa kiasi wa legend huyu ambaye pia ni mjuzi wa mambo mengi ya historia na muziki wa jana na wa leo hapa ulimwenguni, ukitaka kuongea na Mzee Zorro hukusu culture ya Mexico, mabadiliko ya tabia nchi, timu ya Taifa ya Ufaransa, mapenzi ya Tabu Ley na Mbilia Bel yote atakua na la kukuambia. Special special human being. Tafadhali enjoy. 

Love, Salama.

 

Sep 30, 202251:22
SE7EP15 - SALAMA NA MCHUNGAJI RICH BILIONEA | SERMON

SE7EP15 - SALAMA NA MCHUNGAJI RICH BILIONEA | SERMON

Kipindi cha nyuma kidogo nilifanya lile ambalo huwa nafanya la kuwashirikisha rafiki zangu na team kuhusu list ya watu ambao wangependa kuwaona kwenye kiti chetu chakavu na sababu za kwanini hasa waje kwenye meza ile yenye kigae kwa juu maana tukisema tutaje majina tu bila ya sababu thabit za wao kuja pale tunaweza tukaondoa maana yenyewe ya kuwa na watu wenye story za kuvutia na kutufunza kama ambavyo tumekua tukifanya. Jina la mgeni wetu huyu lililetwa kwangu na Michael (Mx) Mlingwa na Ndugu yangu Elbogast Myaluko ndo alinipatia mawasiliano naye na kuanzia hapo mengine yamebaki kukhadithiwa kama hivi.

Sikua namfahamu Mchungaji Richard Hananja mpaka Michael alipo niambia nami nikachukua muda wangu wa kwenda kufanya ka research kangu kabla hajaja mezani, ambacho nilijifunza ni kwamba Mchungaji alikua ni mtu mashuhuri sana ambaye ana watu wengi sana pia wanao mskiliza. Ilinichukua takriban miezi miwili kuweza kumpata maana kila weekend (mara nyingi rekodi za kipindi huwa zinafanyika weekend) yeye huwa yuko safarini. Huitwa sana sehemu mbali mbali, na sasa Serikali nayo imekua ikimuita pia katika matamasha na mikutano mbalimbali. Kwahiyo mara utamsikia yuko Dodoma, mara Moshi, mara Iringa ilimradi yuko busy. Na wakati mwengine Jumapili yake inakua ya yeye kualikwa kwenye Makanisa mbalimbali ili akatoe neno, siku hizi yeye ameshastaafu kuhubiri kanisani na sasa zilizobaki ni hizo za mialiko maalum.

Kama kawaida mimi na wenzangu tulitaka kuanza kwa kumfahamu mgeni wetu maana kama nilivyokuambia hapo awali mimi sikua namfahamu zaidi tu ya kumuona kwenye mitandao akimwaga cheche, tulianzia kwenye kuzaliwa kwake na kukua kwake, mitihani mbalimbali ya ujana, bishara na kazi ambazo ashawahi fanya, na wakati naandika hii nimejifunza pia kuwa Mchungaji hana ambalo anaongeza chumvi maana baada ya sisi kufanya nae maongezi haya, nimeona ameenda sehemu tofauti tofauti na story yake haijawahi kubadilika.

Ujasiri wa ziada huhitajika ili tuweze kufanikiwa kwenye maisha yetu na pia kuwa kwenye mstari ili usiingie kwenye matatizo na vyombo vya sheria. Mchungaji ananiambia jinsi ambavyo alikua ana hustle kila kona, kusafiri bila ya kibali cha kuvuka mipaka ya nchi na boxing ambayo aliifanya kwenye kipindi flani kwenye maisha yake. Boxing imemuachia kovu ambalo kila siku linamkubusha mapambano ambayo ameshawahi kuyafanya kwenye maisha yake.

Boxing pia ndo ambayo imemfanya awe na discipline ya hali ya juu. Kwenye maisha yake ya sasa Mchungaji Hananja anatoa nafasi kwa kila aliye kata tamaa au ambae watu wamemkatia tamaa, yeye ndo huwachukua hao na kuwapa nafasi nyengine kwenye maisha yao, na amini usiamini wengi wao hunyooka na kuanza upya. Kwenye nyumba yake huko Madale Mchungaji anafanya mambo mengi ikiwa pamoja na kilimo na ufugaji. Swali langu lilianza kwa kutaka kujua hizo pesa za yeye kuweza kufanya mambo yote hayo, huwa zinatoka wapi?

Mchungaji Hananja ni MUME, na kwa mujibu wa maelezo yake, alichelewa saana kuoa na mkewe ni Rafiki yake wa kwanza. Yangu matumaini moja mbili tulizopiga humu zitakupeleka sehemu.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Sep 22, 202201:05:02
SE7EP14 - SALAMA NA COACH EVARIST | FIRST QUARTER

SE7EP14 - SALAMA NA COACH EVARIST | FIRST QUARTER

Evarist Mapunda ni moja wa makocha wangu wa maisha haya ninayoishi sasa hivi, ananifahamu toka nikiwa na miaka 17 mpaka sasa hivi ingawa hapa katikati baada ya ‘kuwa mkubwa’ nilipoteana nae kwenye mahangaiko ya kujitafuta na kutafuta maisha. Ila Mimi na yeye tunajua kila mmoja wetu ni mtu wa aina gani na anamaanisha NINI kwa mwengine.

Ukiwauliza watoto na wakubwa wengi wa Upanga watakuambia nini yeye pia anamaanisha kwenye maisha yao, lazima atakua na simulizi kuhusu mwalimu huyu hodari wa basketball na maisha, kama hadithi hiyo itakua haimhusu yeye directly badi itakua inamhusu Ndugu yake au mtoto wake au hata rafiki yake, na kama itakua hana hao wote basi hata ya kusikia atakua nayo.

Coach Evarist ni mmoja ya watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa mno vijana wa miaka ya 2000 kuwa na HESHIMA ya maisha, Heshima ya kazi na miili yao, kama umepita kwenye mikono yake basi utakua unajua hilo. Na kama ule usemi wa Kiswahili unaosema ‘majuto ni mjukuu’ basi ndo faida za yale alotufundisha sisi tunayaona. Tunayaona baada ya kukua maana wakati anatufundisha heshima ya muda na drills ngumu za basketball tulikua tunaona anatuonea sana sana. Binafsi nilikua naona hivyo, nilikua naona kama hanipendi maana kila mara yuko kwenye shingo yangu kuniambia lipi sijafanya vizuri. Sasa hivi nikikaa na kujiuliza kipi hasa kilinifanya nihame Pazi na kwenda kucheza basketball yangu Don Bosco ukiachana na kwamba rafiki zangu wengi walikua kule sasa ndo jibu linakuja kwamba Coach Evarist naye alichangia kwa kiasi kikubwa mimi kuamua hilo. Alikua kijana, mwenye kuujua mchezo na Don Bosco Queens ilikua ni moja ya team BORA zaidi za wasichana kuwahi kutokea miaka hiyo. Wengi wao nilikua aidha nimesoma nao Makongo au nimeenda nao Umiseta mara kadhaa kwahiyo maamuzi yangu hayakua ya kuwaza sana ingawa Pazi ndo ilikua nyumbani kwetu na itaendelea kuwa hivyo.

Coach Evarist pia ashawahi kukutana na mitihani kadhaa mikubwa katika maisha yake, ingawa wa yeye kupata ajali mbaya ya gari mwanzoni mwa miaka ya 2000 itaendelea kusimama kuwa mtihani mkubwa zaidi ambao amewahi kukabiliana nao, ukiachana na fainali tele ambazo yeye kama mchezaji au kocha ambazo zilikua dhidi ya timu ngumu na akawahi kushinda, huu ulikua wa aina tofauti sana. Alikua peke yake usiku wa manane wakati anaenda zake nyumbani baada ya kumaliza majukumu yake aliyojiongezea ya basketball ndo mtihani huo ulipomkuta, Coach Evarist anakumbuka idadi ya watu ambao walimzunguka na kumpiga vibaya baada ya ajali hiyo. Mungu pekee ndo anajua alimuokoa okoa vipi katika lile na kwenye operesheni zake zaidi ya kumi na tano ambazo amezifanya mpaka sasa hivi zinamfanya aishi na kwanini haya yote yametokea.

Coach Evarist ni muaminifu na mwingi wa imani, mpaka leo hii anaendelea kuishi maisha yake kama hakuna ambalo limemtokea na kubadilisha maisha na muonekano wake kwa maisha yake yote. Yule ambaye anakua na moyo kama ambao Coach Evarist anao pekee ndiye anayeweza kuishi kama ambavyo yeye anaishi. Ndo maana yeye ni wa kipekee sana.

Yangu matumaini maongezi yetu juu ya heshima na mustakabali wa mpira wetu wa kikapu na heshima juu ya mambo kadhaa yatakuvutia na kukufunza kitu. Yangu matumaini pia uta enjoy.

Love,

Salama.

Sep 15, 202201:19:50
SE7EP13 - SALAMA NA MARDHIYA | HIARI…

SE7EP13 - SALAMA NA MARDHIYA | HIARI…

Salum Mardhiya ni mmoja ya watu maarufu sana kwenye visiwa vya marashi ya karafuu yaani kule kwetu Zanzibar. Ni mmoja ya waalimu hodari anayeongoza kwa kutoa Da’wa kwa watu ambao wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali. Kwenye nyumba karibu zote wanamfahamu maana huonekana mara kwa mara kwenye maeneo mbali mbali ili kusaidia wale ambao wanahitaji kisomo chake. Binafsi nilifahamiana nae kupitia rafiki ambae alinitambulisha kwake mapema mwaka huu, tena haikua imepangwa wala, alikuja sehemu ambayo mie nilikuwepo kuja kupata chai na mimi bahati nzuri nilikua maeneo hayo so mtu akatutambulisha, na akaambiwa kama Mama yangu ni mgonjwa yuko hospitali na yeye akasema basi atakuja baadae kwaajili ya kumuombea dua, na jioni akatokea. Oh kama angependa kujua hali ya Mama yangu Alhamdulillah yuko vizuri. Tunamshkuru Mungu.

Kwa mujibu wa story za hapa na pale niliambiwa nilikua na bahati sana kumpata maana ratiba yake ya kutoa Da’wa ni tight sana na watu ni wengi wanaohitaji huduma zake ila muda anakua hautoshi wa kumtilia Dua kila mtu ingawa angependa kufanya hivyo, kwahiyo ilikua kama bahati sisi kukutana na kuanzia hapo tukaanza kuwa tunaonana kwa kiasi. Nikaona si vibaya kama nitamleta kwenye meza yetu ili na sisi tuweze kumfahamu zaidi. Wakati namuambia kuhusu mualiko wa kuja kwenye kiti chetu chakavu hakua na hiyana, aliangalia ratiba yake na akaniambia hiyo tarehe atakuwepo nchini.

Sheikh Mardhiya yeye huwa anasafiri sana, Da’wa zake huzitoa sehemu tofauti tofauti duniani, mara nyingi anakua zake Arabuni, mitaa ya Oman na Dubai na Abu Dhabi huwepo sana, kashatibu watu wa aina tele kwenye maisha yake. Kuanzia marajiri mpaka maskini, ambao walikua na imani na anachofanya na ambao hawakua na imani nae. Simu yake huita mara kwa mara na hiyo ni moja ya sababu za yeye kuwa na namba zaidi ya moja na kuwa na wasaidizi kadhaa.

So huku kwenye kutoa Da’wa alifikaje? Hii ilikua ndo mwanzo wa maongezi yetu haya. Akiwa kama kijana ambaye angeweza pengine kufanya kazi ya aina yoyote na kujipatia rizki yake, kwanini alichagua hii? Kaniambia tokea akiwa na umri wa miaka sita, alianza kupata upeo huo, bila hata yeye mwenyewe kujua ni nini hasa kilikua kinaendelea katika maisha yake, anakumbuka pia jinsi alivyokua anazimia na kupata uwezo wa kuwasomea walokua wanahitaji kisomo chake na wanakua poa kabisa, anasema hata hakumbuki alikua anawasomea nini baadhi yao ila sasa baada ya kuwa mtu mzima na kupata kuijua vizuri Quran Tukufu ndo anang’amua nini alikua anawasomea watu ule.

Mwanzo nilisema Mardhiya ni kijana kwahiyo kwa kiasi kikubwa ana style ya maisha ambayo vijana wengi wangependa kuwa nayo ila uwezo nayo hawana. Kama kuwa na maisha ya kifahari, magari mazuri na mke zaidi ya mmoja, pesa nyingi na nyumba nzuri zaidi ya moja na kusafiri mara kwa mara. Hii kwa ki aina flani imekua ikileta maneno na maswali kuhusu uhalali wa ambacho anafanya au ambacho amekua akifanya. Je maneno hayo yanamzui yeye kufanya ambacho anafanya kwa watu wenye uhitaji? Au kubadilisha aina ya maisha ambayo anaishi?

Tumeongea kuhusu masuala ya Husda na wivu, usafi na mmoja kuamua kujipenda zaidi. Je kuna makosa kwenye baadhi ya matamanio ya nafsi zetu? Vipi kuhusu Sadaka? Inatakiwa itolewe ki namna gani? Ipi ni sawa na ipi si sawa? Ipi ni dhambi na ipi ni nzuri ili kuweza kuwafanya na wengine watamani kutoa? Vipi kuhusu Heshima kwa kila mmoja? Wazazi? Nafasi ya Wanawake? Kuhusu imani na uchawi kwa ambacho yeye anafanya? Mmoja anaweza kujuaje kama hii ni kufuru na hii ni sawa?

Maswali yalikua mengi na majibu pia yalikua yanatoka kutokana na swali lilivyo ulizwa, yangu matumaini elimu ambayo Mimi nimeipata na kwako itakua vivyo hivyo.

Tafadhali Enjoy,

Love,

Salama.

Sep 08, 202250:58
SE7EP12- SALAMA NA DR TULIA | BULYAGA 1976

SE7EP12- SALAMA NA DR TULIA | BULYAGA 1976

Tulia Ackson ni jina kubwa kati ya majina makubwa kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kwa sisi kuweza kulipata jina kubwa na kukubali kuja kuketi kwenye kiti chetu chakavu ilikua ni BARAKA sana. Ila ukiachana na kwamba ni jina kubwa ila yeye ni binadamu, tena wa kawaida tu. Ni Mama, ni mke, ni Dada, ni Binti kwa Mama yake na ni Mbunge kwa wana Mbeya mjini lakini pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wadhifa ambao baada ya uchaguzi wa 2020 alirudi bungeni kama Naibu Spika ila baada ya aliyekua Spika kujiuzulu Dr Tulia aliona fursa ya yeye kuvaa viatu hivyo na wabunge nao walimpa kura zao zote za kuridhia Mwana Dada huyu AWAONGOZE.

Baada ya uchaguzi wa 2020 na yeye alirudi bungeni kama MBUNGE kamili, si tunakumbuka baada ya 2015 alienda bungeni kama Mbunge wa kuteuliwa ila mwaka 2020 aliamua kwenda kugombea jimbo la Mbeya mjini ambako Gwiji wa Bongo Flava Kaka yangu Joseph Mbilinyi aka Sugu alikua ndo Mbunge wake? Sugu alikaa kule kwa miaka 10 ilikua ni moja ya ngome za wapinzani ambazo walikua wanajivunia nazo, kwa Dr Tulia kuamua kwenda kugombea pale iliwafanya watu wengi watake kufuatilia mchuano huo mkali ambao mwisho wa siku Dr Tulia aliibuka kidedea. Na haya yalikua ni moja ya maswali ambayo nilikua na hamu ya kumuuliza na kwa urefu alinijibu tu vizuri sana.

Sasa nchi yetu inaongozwa na Rais mwanamke kwa mara ya KWANZA toka tulipopata uhuru wetu mwaka 1961, na hii haikuja kwa kupangwa ila baada ya kutokea ambalo Mwenyezi alikua ameliandika, na hata hili la kuwa na Spika Mwanamke (ingawa huko nyuma Mama Anne Makinda alishawahi kuwa) nalo halikua limepangwa maana Spika tayari tulikua naye baada ya Uchaguzi wa 2020. So suala la kuwa na Rais mwanamke na Spika mwanamke bila ya shaka linalipa Taifa letu utofauti na HESHIMA flani hivi ambao mataifa mengi yanavutiwa nayo.

So kwake yeye nini hasa kimebadilika? Yaani kutoka kuwa Naibu mpaka sasa Spika? Ilikua easy kwake kuichukua nafasi hiyo baada ya kuwepo na nafasi hiyo? Alifikiria mara mbili?

Kwa maongezi yetu haya pia nimegundua Dr Tulia alikua hapendi kabisa siasa, yeye aliyapenda zaidi maisha yake ya kuwa Lecturer pale Chuo Kikuu, alipenda zaidi kuandika na kusoma na kujifunza. Alikua akiwaona wana Siasa kama watu flani ambao pengine wanajiona tofauti na watu wengine, pengine wanajiona wa MUHIMU sana. Je na yeye sasa? Akiwa nao kule bungeni wanaishi vipi? Sasa pia kama Kiongozi wa mhimili huo wa NCHI nini zaidi kimebadilika? Nini zaidi kigumu?

Maongezi yetu yalianzia nyuma kiasi na mbele pia yakafika, pia humu tumeongelea Tulia Trust na vitu ambavyo inafanya ili kuwafikia wale ambao wana uhitaji. Na sasa amekua naye MWANASIASA, nini kimebadilika? Msemo wa Siasa ni mchezo mchafu, kwake yeye una maana gani?

Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza jambo kutoka kwa Kiongozi huyu ambaye pia ni Dada yetu.

Love,

Salama.

Sep 01, 202251:16
SE7EP11 - SALAMA NA MARTIN KADINDA | PLEASANT

SE7EP11 - SALAMA NA MARTIN KADINDA | PLEASANT

Martin Kadinda ni rafiki yangu, ni moja ya wale wana ambao hana makuu na zaidi yeye anapeeenda sana kucheka, hata ukiangalia picha zake yeye ana tabasamu tu. Pengine hiyo ndo siri ya mafanikio yake tofauti yake na wengine na pengine hiyo ndo sababu ya mimi kumpenda sana. Pia ni FUNDI, tena mzuri tu sana. Kati ya mafundi wachache WAKWELI wa nchi hii Martin ni mmoja wapo, kama hawezi hawezi, hata siku moja hawezi chukua kazi yako alafu siku ya siku akakuharibia shughuli au mtoko. Kama yuko busy na mambo yake atakuambia rafiki, hiyo sitoweza tafadhali mtafute mtu mwengine aifanye. Napenda jinsi alivyo honest maana mimi huamini sana kwenye ukweli mgumu kuliko uongo mtamu.

Urafiki wetu ni wa miaka zaidi ya kumi sasa, anakua namuona na bila ya shaka nae ananiona nami ninavyokua, na wote tunaona kustawi kwa kila mmoja wetu, maendeleo kati yetu, challenges na urafiki wa mashaka kwa baadhi ya watu tunao wafahamu pamoja na kung’amua mambo mbali mbali kwa pamoja. Sisi si wana ambao tunazungumza DAILY ila ni wana ambao kila tulikutana basi huanzia pale tulipo ishia mara ya mwisho tulipo kutana. Hatuna neno kati yetu na wala urafiki wetu si wa KULAZIMISHA.

Napenda jinsi ambavyo anasogea kwenye maisha yake, Martin ni mmoja ya watu wachache ambao nawafahamu ambao HAWANA HARAKA ya MAFANIKIO, HANA MASHINDANO na MTU, anafanya yake kwa SPIDI yake na anashindana na yule Martin wa mwaka jana ambaye alimuambia mwaka huu In Shaa Allah atakua kapiga hatua hii na hii na hii na kuhakikisha ile mipango na malengo YANATIMIA kwa usimamizi wa Maulana.

Martin anawajua watu tele kwenye industries tofauti hapa kwetu na wala hutakaa umsikia akirusha majina ya watu hao ili aweze kujiingiza kwenye mazungumzo ambayo hayamhusu au hayana faida na yeye. Mara zote huwa ana focus na yale ambayo yanamhusu na wakati mwengine hayo pia ambayo yanamhusu akiona hayana muelekeo au hasara ni nyingi kuliko faida basi pia si mtu wa kung’ang’ania jambo kwasababu tu ni la mtu fulani au lina line fulani, anaamini kwenye kuanza upya na kwamba kila siku mpya ni sababu nyengine ya kuwa bora kuliko jana na ni nafasi nyengine ya kuweza kutimiza ndoto fulani.

Baba wa mtoto mmoja ambaye alimpata akiwa mdogo tu, Martin anampa mwanawe uhuru wa kuwa mtoto na kuwa yeye na si kumtanguliza mbele kwenye maisha ya yeye kama Baba yake na kumyima uhuru wa kuishi maisha yake kama mtoto na HURU. Tushaona mifano tele hai ya ma celebrity wa Bongo ambao wanawaweka au waliwaweka watoto wao mbele na badala yake wakaishia kuwa target ya matusi kutoka kwa walimwengu na mwisho wake wazazi waishia kulalamika kujumuishwa kwa watoto wao kwenye maisha yao. Tunatakiwa kuamini kwenye kila mtu kujichagulia maisha yake ambayo anataka kuishi na hatusemi kumpost mtoto kwenye mtandao ni jambo baya sana, ila kwa jamii ambayo kumtukana mtoto na wazazi wake haioni kitu cha hatari au kuumiza au kushangaza, nadhani kwa mzazi kumuacha mtoto awe mtoto mpaka pale atakapo jitambua na kuchagua mwenyewe pengine huo ndo ungekua uamuzi sahihi zaidi. Na sisemi pia kama ni sawa kwa walimwengu kufanya hivyo, ila ukishaona kuna mwanya wa jambo kama hilo, mmoja kuamua kuchagua faragha ni jambo jema zaidi.

Hii haikua mara ya kwanza mimi na Martin kukaa chini na kuongea kwenye TV ingawa mara ya mwisho inawezekana ikawa ni miaka 6 au 7 iliyopita lakini bado kulikua na haja na kiu ya kufanya hii, kama nilivyo kuambia hapo juu, tulikutana haijalishi ni muda gani umepita, siku zote tutaanzia pale tulipo ishia.

Yangu matumaini simulizi za urafiki, biashara, wazazi, mtoto, kazi na kuhangaika na kuji panga na kujipa nafasi ambako kumeongelewa humu kutakusaidia kwa kiasi flani kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyengine. Na yangu matumaini pia uta enjoy.

Love,

Salama.

Aug 25, 202201:02:40
SE7EP10 - SALAMA NA DR CHENI | SUKA

SE7EP10 - SALAMA NA DR CHENI | SUKA

Growing up kwenye mitaa ya Dar es Salaam na TV stations kali wakati huo zilikua na presenters makini na vijana ambao kwa kiasi kikubwa waliifanya tasnia hiyo ipendeze sana. Kuanzia vipindi vya watoto, vya muziki, filamu kutoka nje na tamthilia kutoka nje pia zilikua tamu sana, ukianza kuangalia TV kuanzia jioni hakuna mtu alikua anabanduka mpaka saa nne au tano za usiku, na kama ulikua jobless kama mimi enzi hizo basi ulikua unaunganisha na kuangalia marudio ya vipindi vya muziki ambavyo tayari ulikua ushaviona jioni yake, ila kwasababu ya utamu wake na ku enjoy kile unaona kurudia ilikua easy tu. Sasa likaja wimbi la tamthilia za NDANI, kutoka hapa hapa nyumbani, na nikiwa kama mkazi na mtoto wa Magomeni (Mtaa wa Korongo namba 10 pale kama Downing Street) 🤣 ilikua ma star hawa tunawaona tu kwa mbali na kuwaangalia kwa admiration ya hali ya juu. Cheni, au niseme Dr Cheni naye alikua ni moja ya hao watu, ah, yale ndo yalikua maisha sasa.

Yoyote ambaye alikua anapata nafasi ya kuonekana kwenye TV alikua ananyooosha kweli kweli, chochote ambacho anaambiwa ‘acheze’ alikua anakipa uhalisia wa 100%, watu walikua na kiu ya mafanikio sana na jengine kubwa kuliko yote, watu WALIKUA WANAPENDA ambacho WANAFANYA. Na hii simaanishi kumvunjia heshima yoyote yule ambaye anaifanya kazi hiyo leo hii, ila nasemea miaka hiyo ambayo ili uweze kutoboa ilikua inabidi upate ‘upenyo’ ambao nao ukipatikana inabidi uutendee haki sana sana vyenginevyo atatokea mtu huko anakotoka ajipitishe tu kwa miondoko ya ambayo alipita nayo Dr Cheni na kupata nafasi ambayo mpaka leo ndo imefikisha hapo alipo. Again, si kwa ubaya, skuizi unaweza kuwa star wa kwenye social media tu na mambo yako yakakuendea na baada ya mwezi au wiki kadhaa kama huna jipya watu wanakusahau.

Dr Cheni anakumbuka kama ilikua jana jinsi ambavyo alipata shavu lake la kwanza la kuwa kwenye mchezo wa kuigiza wa TV, haikua imepangwa na wenye mchezo wao ila yeye alikua amejipanga vizuri tu, alikua amenuia kabisa kwamba vile ndivyo atakavyo fanya ili aonekane na boy alionekana. Kama mtu ambaye tayari alishaanza kushika hela kutokana na kazi zake za udereva, Dr Cheni anakumbuka jinsi ambavyo alianza kuzichanga zile ambazo alikua anazipata kidogo kidogo ili atimize ndoto yake, khadithi yake kwa kiasi flani ilianzia hapo, nami nilitaka kujua hiyo heshima yake na pesa aliitoa wapi? Kutoka kuwa dereva wa daladala mpaka kuwa mmliki wa gari. Huko alifikaje? Na jibu lilikua moja tu, HESHIMA kwa PESA na HESHIMA kwa NDOTO na MALENGO yake. Alifanikiwa sana mwenzetu. Na ndo huyu mpaka leo ambaye bado anaendea kuwepo na upepo kuuhamishia kwenye ku host harusi za watu mbali mbali ambao wengi wao humpa kazi kwasababu tu walishawahi kumuona kwenye TV wakati wanakua, ukiachana na ukweli kwamba yeye ni mmoja kati ya ma MC HODARI kabisa ambao wako sasa kwenye industry hiyo.

Akiwa kama Baba mwenye jukumu kubwa la kuiangalia familia yake inavyokua, Dr Cheni anajua kutimiza majukumu na wajibu wake wa kila siku, kupangilia mambo yake ili asiwakwaze wengine ambao wanamtegemea (hasa wale ambao anawafanyia kazi zao za harusi). Kwake yeye kuwa kwenye wakati muafaka ni kila kitu. Na hiyo kwa kiasi kikubwa imesababisha yeye kuwa chaguo la kwanza kwa wengi ambao wanataka sherehe zao zifane.

Na je vipi sasa kwenye suala zima la filamu na maigizo? Huko nako kashakimbia? Soko limekaaje? Mipango yake ya baadae je? Yote haya na zaidi yako kwenye lisaa limoja na na dakika 16 ya Podcast hii kama utaskiliza au lisaa limoja la kuangalia naamini litakufungulia mengi.

Tafadhali Enjoy.

Love,

Salama.

Aug 18, 202201:16:00
SE7EP09 - SALAMA NA DAMIAN SOUL | HARIRI…

SE7EP09 - SALAMA NA DAMIAN SOUL | HARIRI…

Damian Soul ni Superstar na siku ambayo sote tutakubaliana na hiyo statement basi tutaanza kufaidi matunda ya kipaji chake kwa uzuri sana, ila mpaka siku hiyo ifike ni wachache tu ambao wanamuelewa kwa upana huo ndio ambao wataendelea kufaidi kipaji chake kwa nafasi yao. Wale watu wa makampunj mbali mbali kwa mfano CocaCola ambao wanakua na events zao za ndani kwaajili ya watu wao na waalikwa wawili watatu huwa wanamfaidi sana kijana huyu hodari wa ki Tanzania. Na Damian kwa ukali wake akipata nafasi kama hiyo huwa hafanyi makosa hata kidogo, huhakikisha anapeleka mziki wote kwao ili wakati mwengine wanapokua na event basi jina lake liwe la kwanza kwenye list ya waburudishaji wao. Mzaliwa wa Dar es Salaam, mtoto wa Sinza kabisa, Damian amezaliwa kwenye familia ya kishua kabisa, jinsi ambavyo unaona anavaa ki nadhifu vile ukiachana na hereni zake, hivyo ndivyo Marehemu Mzee wake alivyokua ananyuka, nadhifu kabisa. Koti imenyooka na ilivaliwa inakaa hasa mahala pake, kiatu inang’aa vizuri baada ya kuipiga kiwi mwenyewe, Damian anakumbuka unadhifu huo na ki uhakika ameurithi na kuuendeleza. Shule kwake ilikua ni kitu tu ambacho ilibidi akifanye kwasababu pengine kila mtu au mtoto kwa matakwa ya wazazi ilibidi afanye hivyo na ili aweze kutoka pale alipokua ilibidi afunge mabegi yake mpaka Kampala nchini Uganda, kama utakumbuka vizuri kuna miaka ya kati ya 2000 hapo ilikua kama ‘fashion’ kwa watoto wa ki Tanzania kwenda kusoma kule, kwa khadithi nyingi nilizo zisikia wengi wao walikua sio waingiaji sana class na badala yake maisha ya ku party na kujitafuta na kujielewa ndo yalikua ki hivyo zaidi. Haikua tofauti pia kwa Damian Soul, Ila yeye sio kwenye ku party ila kwenye kujitafuta na kujua kwamba muziki ndo kitu alitaka kufanya kwa maisha yake yote. Anakumbuka mti ambao alikua anakaa chini yake na ‘kulicharaza’ sana gitaa na kila aliyekua anapita pale habari alikua nayo. Upekee wake wa kuanzia sauti mpaka style yake ya mavazi ndo unaomtofautisha yeye na wengine, ukimuona tu utajua kama ni Star maana jinsi ambavyo anajibeba ni tofauti na watu wengine. Hii pia inasababisha watu kujiuliza maswali kuhusu maisha yake na vitu apendavyo kama mtoto wa kiume. Yeye kwa mujibu wa maongezi haya na mengine ambayo mimi na yeye tushawahi kuwa nayo hayamsumbui kabisa. Anajiheshimu na kujielewa na pia anajua mipaka iko wapi. Na pengine kama binadamu tunatakiwa kuwaacha watu wawe wao, especially kwasababu hayo ni maisha yao, na kwa heshima na taadhima wanajua jinsi ya kujibeba kama binadamu na zaidi kama mTanzania. Anakumbuka jinsi ambavyo alikua Sinza hasa baada ya Baba yake kutangulia mbele ya haki, anasema mtaani palikua pa moto sana kwa kugumbikwa na wimbi la vijana kujihusisha na vitendo vya kihuni na wizi na kujikita kwenye matumizi mazito ya madawa ya kulevya. Anasema yeye alifanikiwa kukimbilia kanisani wakati anasubiria mambo yake mengine ya shule yakae sawa. Kanisani ambako alijifunza mambo ya muziki ikiwa pamoja na kujifunza kupiga instruments, ukiachana na sauti yake ya kipekee, Damian pia ni mpiga gitaa mzuri sana na muandishi hodari pia wa ngoma zake. Mimi ni mmoja wa mashabiki wake na binafsi nilichukua nafasi hii ili tukae chini na tuyajenge kama familia na watu wengine pia wapate nafasi ya kumskiliza na kumuelewa vizuri. Wengi wamekua wakimhukumu kwasababu tu ya muonekano wake na kama Dada na rafiki niliona kuna umuhimu wa sisi kupata nafasi ya kukaa chini na kumfahamu kinaga ubaga. Kama binadamu wote tulivyo, kila mmoja wetu ana mitihani yake ambayo anapitia, mengine mpaka leo inaendelea na mengine ilikua tunafaulu na mengine kufeli, ila kupitia huko ndo ambako kumetufanya tuwe bora na wapya na kujifunza ni jinsi gani mmoja anaweza kutengeneza maisha yake na akawa mfano bora kwa familia na jamii ambayo imemzunguka. Kama mtoto kwa Mama yake na kioo cha jamii, Damian yuko humble sana na wala hana papara kwenye kuhakikisha anafika pale ambapo anapaona kuna kitu cha yeye kuweza kukaa. Mpaka sasa hayuko pabaya hata kidogo maan

Aug 11, 202201:06:14
SE7EP08 - SALAMA NA SAMATTA | HEADMASTER

SE7EP08 - SALAMA NA SAMATTA | HEADMASTER

Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya mbuzi wakati anakua na mwisho wa siku akaenda kucheza kwa wazungu na bado anaendelea kutafuta rizki yake huko, hata kama sio ligi ile ambayo hata yeye mwenyewe angependa awepo ila BADO ni MWAMBA wetu. Samatta huyu huyu ndo ambaye alijitwika mpira kichwani na kuitika nyavuni mbele ya beki ambae anaaminika kuwa BORA kwa misimu hii miwili mitatu ndani ya Virgil van Dijk. Hata wakati naandika hii bado mwili unanisisimka kwa wazo tu kwamba nililishuhudia lile, pata picha kwa mtoto ambaye ana ndoto hizo. Lile goli lilimfanyia NINI kwenye ndoto zake. KRC Genk walipoteza mchezo ule wa ugenini wa kombe la mabingwa wa Ulaya kwa magoli 2-1 ila kwenye mitaa yote ya mikoa ya Tanzania ile mechi ilikua ya USHINDI.

Mbwana ametokea kwenye familia ya kawaida sana sana, wazazi wake wote kama kumbukumbu yangu itakua 100 basi walikua polisi, najua kwa hakika Baba yake alikua Polisi kwa asilimia 100. Kwa marehemu Bi Mkubwa wake ndo sina hakika sana ila kwa hakika jibu limo kwenye haya maongezi yetu. Anakumbuka jinsi ambavyo Mzee wake alikua anasisitiza kwenye suala la elimu na heshima, kama mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo, Mbwana aliupenda sana mpira, zile za kujiiba na kwenda kucheza mechi za mbali alishafanya sana na matunda ndo haya ya leo. Nadhani ilifika kipindi Mzee mwenyewe aliona basi sawa, twende huko utakako. Familia yao yote ni wapenzi wa mpira na Kaka yake Mouhamed bado anacheza hapa hapa Tanzania. Sasa akiwa kama kioo kikubwa sana kwenye jamii hii Samatta anazungumzia presha ambayo hupewa hasa pale anapoitwa kwenye timu ya Taifa, jinsi maneno mengi ya kashfa yanaporushwa kwake kutoka kwa wananchi na anakumbuka pia wakati bado anacheza T.P Mazembe kuna kipindi kocha aliacha kumuita yeye na Rafiki yake Thomas Ulimwenguna ilisemekana kama pengine hakuna na interest na team au hakua anatoa 100. Pengine kipindi hicho aliumia zaidi maana hiyo haikua jambo zuri kwake.

Mbwana anazungumza na mimi kuhusu urafiki wake na Ulimwengu na maisha ambayo walikua wanaishi pamoja wakati wako DRC, anakumbuka jinsi walivyokua wanapanga kufanikiwa pamoja na mipango yao endelevu kwenye career yao. Ulimwengu nae ana siku yake kwenye kiti chetu In Shaa Allah maana nae ana mengi ya kutuelezea. Majeraha ya mara kwa mara bila ya shaka yalisababisha kwa kiasi kikubwa ndoto zake za kucheza Ulaya kutochukua hatua ya juu kama ambavyo angependa, ila mimi naamini hayo yote maisha tu, kila kitu kilikua tayari kimesha andikwa.

Samatta ni Baba ambaye watoto wake wanasoma hapa hapa nyumbani, nilimuuliza kama watoto wake wanajua yeye ni nani na akanipa story ndogo ya yeye kung’amua kama wanafahamu fika Baba yao ni nani.

Mwenzangu humu kuna mengi sana ambayo yatakufaa na kwa nafasi ya kipekee ningependa kumshukuru Captain wa Taifa kwa kuchukua time kwenye ratiba yake ambayo ilikua imebana kweli kweli ili tu aje kutubarikia meza yetu kwa uwepo wake.

Yangu matumaini uta enjoy sana.

Love,

Salama.

Aug 04, 202201:00:51
SE7EP07 - SALAMA NA DR KUMBUKA | YAANI…

SE7EP07 - SALAMA NA DR KUMBUKA | YAANI…

Dr Kumbuka ni influencer mkubwa kwenye masuala ya mahusiano na maelewano inapokuja kwenye suala zima la ushauri na mashauri kwa watu wengi ambao wamekua wakimsikiliza na ambao wanamsikiliza kila siku za wiki anapokua kwenye kipindi cha Uhondo pale EFM. Na yeye kuwa pale hakufika kwa bahati mbaya. Ila pengine alipo anzia kazi yake pale Times FM ndo ilikua kama bahati kufika. Anakumbuka jinsi ambavyo alikua zake tu mtaani wakati mtangazaji wa Times FM wakati huo Bi Dida Shaibu alipokua mtaani akitafuta watu wenye kipaji cha ‘kuchamba’ watu wengine. Anasema wanawake ndo walikua wametawala jukwaa huku wakishusha maneno mengi ya karaha kwa wanaume, na hapo ndo yeye alipoona nafasi ya kupanda jukwaani na kuwawakilisha wanaume wenzie kuhusu ila na karaha ambazo na wao pia wamekua wakizipata kutoka kwa wanawake.

Huo ndo ulikua mwanzo wa safari yake hii ya kuwa mmoja wa watangazaji hodari wa radio kwa muda huo anapokua hewani, EFM walivutiwa na kipaji chake na wao wakaona bora wamvute kwenye radio yao ili awatumikie wao na kipaji chake. Akiwa Baba wa watoto 5 sasa Dr anazungumzia kashfa na maneno mengi ambayo yamekua yakisemwa juu yake na muonekano wake na uzungumzaji wake. Anasema pia akiwa kama Baba na mtoto wake wa kwanza na wa pili nao wameshaanza kutumia mitandao ya kijamii na kuona comments ambazo watu wanaacha chini ya post zake huwa zinamtia unyonge wakati mwengine, hasa ile ambayo inahusu zaidi jinsia yake, mengine ya kwamba anajichubua huwa hayamsumbui asilani maana hiyo ndo rangi yake!

Alilelewa zaidi na Mama yake mzazi ambaye katika umri mdogo kabisa Dr ilibidi naye amlee Marehemu Mama yake maana hakukua na mtu mwengine kwenye familia ambaye angeweza kufanya hivyo, kwa mtoto wa kiume kumuogesha, kumvalisha na kumfanyia mengine ya faragha Mama yake mzazi ilikua mtihani, ila kwa sehemu ambayo alikua wakati huo, hakukua na njia nyengine ya kufanya. Alikua akimaliza kumtaarisha Mama yake anamuacha kwa majirani na hapo ndo yeye anapata nafasi ya kwenda shuleni.

Ni wengi wamepita na kushuhudia mengi wakiwa wanakua na mitihani na majukumu bila ya shaka hutofautiana, kwake yeye anaamini ni Baraka mara dufu kwa yeye kuweza kupata nafasi ya kufanya hayo yote kwa Mama yake kipenzi mpaka Mwenyezi Mungu alipo mchukua.

Na Baba yake je alikua wapi wakati haya yote yanatokea? Na je alikua Mzee wa aina gani?

Majibu ya hayo maswali yote Dr Kumbuka anatupatia katika episode hii ilojaa story nyingi za kukutaka utake kusikia zaidi.

Kama Baba ambaye hakupata nafasi ya kuwa na Mzee wake wakati anakua, Dr Kumbuka anahakikisha watoto wake sasa anawalea mwenyewe na kuwapa asilimia 100 ya uangalizi wake, na hiyo haijalishi kama Mama wa mtoto bado yuko nae au la, kwa yeye kuwa pale ndo kitu ambacho kinamfanya yeye ajiskia vizuri zaidi.

Yangu matumaini kutakua na mengi ya kujifunza kutoka kwenye episode yetu hii ya SABA ya msimu wetu huu mpya ambao tunahakikisha unapata kuwaskiliza watu wa aina mbalimbali ambao story zao zitakuvusha sehemu flani.

Love,

Salama.

Jul 28, 202201:07:07
SE7EP06 - SALAMA NA MTANI | SO SILKY

SE7EP06 - SALAMA NA MTANI | SO SILKY

Ushawahi kukutana na wale watu ambao wao ni wa pole tu sana na wanajipenda tu sana ila hawana tu muda wa kuringa au kuji mwabafy kwasababu wao wako talented au wana kipawa kutoka kwa Allah na wanajua? Well mi nishawahi kukutana na watu kama hao na mmoja wao ni mgeni wetu RASMI wa wiki hii ya episode ya sita ya SalamaNa msimu huu. Anaongea kwa utaratibu na kujua kile atakacho, anakipataje na akisha kipata atafanya nacho nini. Huyo sasa ndo mwanangu Mtani Nyamakababi, aka Mtani Beskope.

Kijana wa ki Tanzania mwenye kuelewa somo la leo na ukiachana na mitihani ambayo anakua anaipatia na mara nyingi huwa anafaulu kwa masksi za juu sana, kama daraja basi lake huwa ni la kwanza kabisa! Ufahamu wake na kujiongeza kwake kwenye knowledge na udambwi dambwi kwenye yale ayafanyayo kwa hakika ndo kunamfanya awe trend setter na wengine ambao wanafanya kazi kama ambayo yeye anafanya wabakie kumuona kama Role Model, naamini kwa kiasi kikubwa haata yeye bado hajioni kama Role Model maana safari yake ya kufika kule anapo pataka na kupaota ndo kwanza imeanza kustawi.

Miaka 30 ya umri mwaka huu wa 2022 bila ya shaka ni mwaka mkubwa kwake, ukiwa mtoto wa kiume na tegemeo la familia kufikisha miaka 30 ni jambo kubwa, hasa ukiwa hujaoa na una ramani ya maisha kama alo nayo yeye bila ya shaka utakua na mipango mingi, mengine yanawezekana na mengine ni kwa Rehema za Mwenyezi Mungu zaidi. Najua yeye anajua kama Mzee na Mama wanataka kumuona kijana wao akiwaletea wajukuu na I hope wazazi wake hawato subiri kwa kipindi kirefu kama ambacho Mama yangu mimi ameendelea kungoja . Yeye tayari yuko kwenye mahusiano ya kueleweka tu na ambayo yanaonekana yanaelekea mahali pazuri kwa mujibu wa maongezi yetu haya.

Kama binadamu wa kawaida of course alishawahi kuumizwa kwa uongo na kutokua na uaminifu kwenye mahusiano ila hilo halikuwahi kumrudisha nyuma kwa kuamini huyo alonaye sasa ni wake na anamfaa sana, anamsaidia sana na anamuongoza sana, vitu kama hivi mmoja huhitaji kuskia, hasa yule ambaye tochi yake imefifia mwanga, mwangaza wa mapenzi. Anamkubali sana yule anaye share nae siri zake na struggle zake na ushindi wake mwingi na hata frustrations zake. Na anajua pia kama kuna kupanda na ku shuka kwenye mahusiano na maisha kwa ujumla.

Kwenye meza yetu kulikua na maongezi kuhusu wazazi wake na principle zao za maisha, mdogo wake… Biashara zake na ushindani, mapenzi na uaminifu. Urafiki, ku shinda na kushindwa na pia maoni yake zaidi kwenye vitu mbali mbali ambavyo vinahusu ambayo anafanya na vile ambavyo amekua akitamani kuvifanya. Wapi anajiona baada ya miaka 5 mengine? Well… Hatukuongelea masuala ya hela maana najua hiyo ingemfanya asiwe huru mbele yetu maana mambo kama hayo yanahitaji mtu ambaye hana noma za hivyo ila kwa Ndugu yangu huyu yeye noma anazo, tena nyingi kwahiyo kistaarabu kabisa nikaona NIMUACHE.

Yangu matumaini utaokota kadhaa humu ambayo yatakupa mafuta ya ZIADA ya kutaka kesho uamke salama na kwenda kuwa BORA zaidi ya JANA kwa lolote ambalo utaamua kufanya na lenye kheri na wewe. Mimi nakutakia BARAK ZOTE kwenye hilo maana mifano hai ya wanao jituma na kufanikiwa ipo. Maana yake ni kwamba, inawezekana. Wewe tu!

Love,

Salama.

Jul 21, 202255:10
SE7EP05 - SALAMA NA OSCAR OSCAR | UALIMU?! SI WITO!!

SE7EP05 - SALAMA NA OSCAR OSCAR | UALIMU?! SI WITO!!

Mwaka 2018 ndo nilimfahamu Oscar baada ya kukutana nae kwenye kituo changu cha kazi ya kutangaza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini. Alikua mmoja ya watu ambao walinikaribisha vizuri sana kwenye team na kwa wakati huo yeye ndo alikua anaishikilia rekodi ya kuwa ndo mtangazaji mdogo zaidi kwenye team ya watangazaji nami nikaja kama Binti PEKEE ambaye ambaye alikua anatangaza mpira wa miguu kwa lugha ya Kiswahili. Combination yetu ilikua nzuri sana na kwa kipindi hiko ambacho kilikua cha mwezi mmoja tulielewana na ku bond vizuri sana.

Oscar anapenda raha, anapenda kucheka na kuishi vizuri, anapenda ukweli na kubwa zaidi ni Rafiki mzuri sana. Pengine la zaidi ambalo nna uhakika Mama yake mzazi kule Kaliuwa anajuvunia sana ni la usomi, ni mwanafunzi mzuri ambaye anapenda kujiendeleza, sasa anamalizia Masters yake kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alishawahi kuwa Mwalimu kipindi cha nyumba kwenye maisha yake na kwa mawazo yangu ya haraka hii ndo ambayo inamfanya awe ni mmoja kati ya wachambuzi makini kabisa ambao nchi hii inayo, nguvu yake ni kuhakikisha pale kwenye ukweli unasemwa hata kama itakua kwa njia ya mas’hara, ila atausema!

Aliamua kuwa Baba na hili ni kwa mujibu wake baada ya kunikatalia katakata kwamba mtoto wake wa kwanza alikua ni wa ‘bahati mbaya’ kama ambavyo baadhi ya wazazi husema, Oscar anasem alikua anajua nini anafanya na Mama wa mtoto yule so kusema alikuja kwa bahati mbaya ni kama kumkosea mtoto yule ambaye alikuja kipindi ambacho Oscar alikua bado hajajiweka vizuri kwenye maisha yake na zaidi kwenye masuala ya kazi, na pia ananikumbusha jinsi alivyokua anajiona anajua saana na kama vile watu waliokua wanampa nafasi kipindi kile kama vile walikua hawanuelewi kabisa.

Anaamini kwenye kujifunza kila kukicha ili kupanua wigo wa uerevu na kwake yeye Elimu ndo ufunguo wa maisha toka siku ya kwanza.

Kama Baba wa watoto wawili ambao kwa kiasi kikubwa amekua hapo kwaajili ya vijana wake, Oscar anaamini kwenye kuwa pale kwaajili yao, kuwapa kile ambacho yeye hakukipata kutoka kwa Mzee wake wakati anakua, kuwa pale kwaajili ya watu wa familia yake na zaidi Mama yake ambaye kwa mujibu wa Oscar Mama ndo nguzo yake. Binafsi nayajua mengi ambayo amayafanya Kijijini kwao Kaliuwa kwaajili ya familia yake na hata ambao hawamhusu.

Humu mimi na Rafiki YANGU tulijadili mambo mbalimbali ya ki maisha na familia, kazi na muskabali wa biashara ya mpira kwenye NCHI yetu na dunia kwa ujumla, pia tuliongelea umuhimu wa familia na kupata mtoto ukiwa na umri mdogo, suala la ajira na hustle wakati tunakua nalo hatukulicha nyuma. Yangu matumainj nawe uta enjoy pia.

Love,

Salama.

Jul 14, 202201:11:15
SE7EP04 - SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO | شيخ

SE7EP04 - SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO | شيخ

Sheikh Hilali Shaweji Makarani au Sheikh Kipozeo ni mtu wa watu, au niseme kama ambavyo tunasema kwetu Uswazi, Sheikh ni mwana wa wana, anaweza kuwapa wana darsa kwa lugha yao na wakawa huru na wao kusema maoni yao au uelewa wao kwa raha na bashasha nyingi na naamini hii imemfanya yeye awe ni mmoja ya Ma Sheikh wanao tambulika zaidi kwenye mitandao ya kijamii nje na ndani ya Tanzania. Lugha hiyo ya wana ambayo anaitumia inasaidia sana kufikisha ujumbe ambao ameukusudia kwa wakati huo na ikapata mpaka majadilioano, majadiliano hayo ndo huzaa majibu ya maswali mengi ambayo wengi hujiuliza.


Kwetu au kwangu ilikua ni kaji task ambako nilikua najua inabidi nikakamilishe, na jina lake kurejea kutajwa mara kwa mara na watazamaji wa kipindi hiki pia ilichochea dhamira hiyo kwa kiasi kikubwa. Nilikua sijawahi kukutana nae kwahiyo hii nami ilikua ni mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho, shabiki yake? Oh yes, mkubwa tu. Nimekua nikimskiliza na kumuangalia kila nipatapo nafasi ya kukutana na mafunzo yake, kwahiyo hamu ya kutaka kuongea nae ilikua inaongezeka kila siku zinavyozidi kwenda. Wakati ambao Mwenyezi Mungu ameupanga ndo wakati sahihi kabisa. Na naamini huu ndo ulikua muda ambao tulikua tumepangiwa haya mazungumzo kutokea na haikua huko nyuma ambako pengine tulidhani tungemtafuta na kuweza kuongea nae.


Alikua mkarimu kwangu, humchukua muda pia kuongea kama yule wa kwenye video maana kama Mwalimu nadhani huwa anaangalia spidi ambayo uko nayo na kujua anaenda na wewe vipi ili iwe imekaa mahala pake. Na naam, tuliweza kwenda vizuri, alinifanya nami niwe huru na muwazi kwa yale ambayo tulikua tumepanga na wenzangu kumuuliza.

Akiwa Baba na mume mpedwa kwa familia yake, Sheikh Kipozeo amekua akipata mialiko sehemu mbali mbali ili aweze kuwapa watu ‘dawa’. Humu zaidi sisi tulitaka kujua jina lilipo anzia na jitihada zake za kufikisha neno la Mwenyezi Mungu kwa wanaohusika. Alituambia pia kuhusu asili yake na ‘urithi’ wa dini ulipotokea. Lini hasa alijua kwamba ambacho anakifanya sasa ndo ambacho alikua anatakiwa kufanya kwenye maisha yake yote?


Yangu matumaini dawa itaingia na uta enjoy kuangalia au kuskiliza episode hii yetu ya nne.


Love,

Salama.

Jul 07, 202258:43
SE7EP03 - Salama Na Quick Rocka | SWITCHER

SE7EP03 - Salama Na Quick Rocka | SWITCHER

Abbot Charles ni jina maarufu kwa wanaoijua historia na wana zuoni, pengine umaarufu wa jina ndo sababu ya Baba yake kuamua kumpa mtoto wake wa kiume akitegemea na kijana wake atakua na ukubwa huo kwa lolote ambalo ataamua kufanya kwenye maisha yake, unaujua ule usemi kwa kiswahili kwamba maneno huumba? Mwenzangu, hata majina huumba, tena sana tu kwahiyo wakati mwengine utakapokua unafikiria jina la mwanao ni vyema kujiridhisha kwanza, unafanya kazi flani ya kipolisi ya kuchunguza ili mwanao asije akawa mtu fulani asiye na dira.

Quick Rocka aka Switcher aka Baba aka Kaka Fule ni mdogo wangu, hizo aka alozojipa ni maana halisi ya uwezo wa kuishi kwenye kila character ambayo anayo na ameamua kuiishi. Ni Quick na anaweza kuku rock wakati ana rap, na anaweza ku switch na kuwa singer na mambo yakaenda vizuri tu, au aka switch na kuwa Kaka Fule, aka kufanya utake kuendelea kumuangalia tu kwenye Jua Kali au filamu ambazo amekua akifanya. Switcher pia ni producer mzuri tu wa muziki ambao anaufanya.

Katika vijana wa kuwaangalia jinsi wanavyoelekea kwenye mafanikio yao yeye pia anafaa kuangaliwa na hii naamini inatoka kwenye kampani ambayo amekua nayo tokea siku ya kwanza alipojua anataka kufanya mziki, group aliyokua nayo kwenye Rockers ilikua imesheheni mafundi ambao pengine focus yao haikua kama ambayo Switcher amekua nayo au pengine walikua na vitu vyengine ambavyo ni vizuri pia vya kufanya na kuamua kuachana na muziki, pengine kufanya muziki haikua priority yao ila kwa Quick mambo yalikua tofauti. Ukaribu wake na Master Jay kwa kiasi kikubwa umemsaidia kuweza kuwa focused na mambo yake ya msingi na pia alikiri kwenye maongezi yetu haya kwamba kuna kipindi baada ya msiba wa Marehemu Kaka yake, alikua sehemu mbaya sana kifikra ila Master Jay alimsaidia kwa kiasi kikubwa kurudi kwenye mstari. Na kuanzia hapo sasa focus ya vitu ilianza kuwa 100% na ukiachana na kwamba Master Jay ndiye alimchomoa Quick kutoka kwenye kundi na kutaka asimame mwenyewe kama Solo Artist.

Pia Marco Chali ndiye aliyekua anamtengezea muziki wake wote, na kamsoto flani ambako alikapitia ili kumfanye awe huyu ambaye yuko leo chini ya uangalizi wake kwa kiasi kikubwa pia yalimfanya asogee ki maisha, mambo yote ambayo tunakutana nayo kwenye njia ya kuelekea kwenye mafanikio ni lazima ilikua tuyapitie ili kutufanya tuwe bora kwenye haya maisha tunayoishi sasa. Ambacho hakiku uwi kinakufanya uwe jasiri tu. Na jasiri Quick alikua. Aliweza kufungua studio yake mwenyewe ambayo alimfanya awe huru zaidi na kujijenga zaidi, hapo studio pia alitoa nafasi kwa wenzake ambao nao pia walikua wanatafuta sehemu ya kutokea. Kwenye studio ya Switcher ndiko ambako OMG ya Salmin Swaggz, ConBoy na YoungLunya ilizaliwa, tuseme kwa Quick Rocka kuliwapa tafu ya kufika mjini. Ma producer mbali mbali pia walianzia pale na kupata nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi kwenye sehemu nyengine.

Mimi na enjoy kumuona Abbot anavyokua na kujielewa na kujithamini, anavyo jibeba na kusogeza mambo yake kwa spidi nzuri. Kama kijana nna hakika ana mapungufu yake na kuna makosa alishawahi kufanya huko nyuma na probably hata mbeleni kwenye maisha, ila huwa hatumhukumu mtu kwa makosa aliyowahi kuyafanya bali kwa jinsi ambavyo alitoka kwenye hayo makosa na kuwa mtu bora zaidi.

Yangu matumaini uta enjoy story hizi ambazo zilikua zinapigwa kwa uhuru wa iana yake.

Love,

Salama

Jul 01, 202201:05:14
SE7EP02 - Salama Na Engineer Hersi | A BREATH OF FRESH AIR

SE7EP02 - Salama Na Engineer Hersi | A BREATH OF FRESH AIR


Kama kichwa cha habari kinavyosema, Engineer Hersi ndo chachu ya furaha kwa mashabiki wa moja ya timu kongwe kabisa ya Taifa hili, timu ya wananchi, timu yenye mataji mengi zaidi yaani mabingwa wa ki historia. Nikiwa kama shabiki wa Simba Sports Club basi sina la zaidi la kufanya ila kumpa mtani wangu Hongera ya kuongeza taji jengine kwenye historia yao na pia kumsifu round hii kwa kutuzuia kuchukua ubingwa kwa mara ya tano MFULULIZO.Engineer Hersi Ally Saidi aliingia pale kwa njia ya mdhamini (GSM) ila baada ya kuonekana kazi nzuri ambayo ameifanya kwa kipindi cha miaka miwili, Yanga sasa inaingia katika mchakato wa kuifanya timu iwe na muekezaji na mchakato huo yeye ndiye ambaye anauongoza. Kama mshabiki wa klabu, suala la GSM kuwa mdhamini mkuu kulileta chachu ya yeye kuweza kuongoza mabadiliko hayo ambayo yataanza hivi karibuni. Na yeye ndiye anatabiriwa kuwa Rais wa klabu yake pendwa baada ya uchaguzi ambao utafanyika mwezi ujao.Narudia tena, kama shabiki wa SIMBA, mchakato ambao watani wetu wanaenda nao mmoja anaweza kuwa kakaa mbali na kutamani tu yale ambayo yanaendelea na kuomba (kwa nia njema) wenzetu wafanikiwe zaidi ya pale ambapo sisi tulifika kwenye mabadiliko hayo. SIMBA ndo ilikua timu ya kwanza kwenda kwenye mchakato huu ila inaonekana kama kuna sehemu zoezi limekwama na maswali mengi yamekua yakijitokeza na kuulizwa na baadhi ya mashabiki, mashabiki ambao pia wengi wao ni watu wenye vyeo na mamlaka. Tena, yangu matumaini wenzetu wataweza kukamilisha zoezi hili mpaka mwisho ili wengine waweze kujifunza.Engineer pia ni Engineer, Baba, Kaka, Rafiki na mtu poa sana, mfanya biashara pia kwa upande wake mwengine wa maisha. Ametoka katika familia ambayo ilihakikisha anapata elimu na kuwa mfano bora kwa jamii ambayo inamzunguka. Amekua Baba mzuri kwa watoto wake watatu, Engineer mzuri kwenye kazi yake, moja ya kazi yake ni ile HQ ya GSM pale mtaa wa Samora na kiongozi BORA mbele ya macho ya wana Yanga Afrika.Niliongea nae pia kuhusu maoni yake kwenye suala la mfupi wa elimu hapa Tanzania na kama huwa anasaidia maoni yake hasa kwenye kitengo cha elimu ya ufundi zaidi ukichukulia yeye ni mmoja wa uzawa wa shule za ufundi.Yangu matumaini basi uta enjoy na kujifunza jambo kama ilivyo kawaida yetu. 

Love,

Salama.

Jun 23, 202201:29:48
SE7EP01 - Salama Na ZUCHU | SINDANO

SE7EP01 - Salama Na ZUCHU | SINDANO

Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa hiyo kazi yenyewe.

Kazi ya Zuchu ilianza kabla hajaipata hiyo kazi yenyewe na ilikua kazi haswa kuipata na Mama yake Bi Khadija Kopa ndo alikua kinara kwenye hiyo connection ambayo Binti yake alikua anaitaka ili aweze kuwa msanii wa Diamond, na hayo ndo yalikua maneno yake hasa, toka alivyorudi kutoka Nigeria kwenye mashindano ya kusaka vipaji na alikua hajielewi elewi kwa kiasi flani ni kitu gani alikua anataka kufanya na kama basi kutakua na la kufanya inabidi liwe kutoka WCB na sio sehemu nyengine yoyote na agulia nini kilitokea? WCB aliipata na kilichokua kinatakiwa baada ya hapo ni UVUMILIVU wa HALI YA JUU.

Kwenye vitabu vyangu vyote Bi Zuhura Othman Soud ndo muandishi wangu BORA wa KIKE kuwahi kutokea katika kizazi chetu hiki cha Bongo Flava, na naweza sema hivyo wakati wowote iwe usiku au mchana, kipaji hicho ndicho kilichonifanya mimi nistaajabu sana na kutaka kuongea nae na kumuuliza yote yale ambayo nilikua nataka kumuuliza, ingawa humo humo nilikua nishajijibu kutoka kwenye historia ya familia atokayo ingawa hiyo haikutakiwa ndo iwe lazima, lazima mtoto wa Khadija Kopa na Othman Soud awe muandishi mzuri maana wazazi wake wamejaa vipaji tena na Baba yake ndo muandishi mkubwa wa nyimbo nyingi za Mama yake zilizowahi kuvuma.

Kwa umri wake wakati mwengine hujiuliza kajuaje haya maneno yote, anajua maana yake hii? Kasikia wapi hili neno au pengine je huwa anamfikiria Mama yake (ambaye ndo kipenzi chake na ndo amemlea) wakati anaandika hii? Anaona aibu? Je huwa wanaongelea hayo mashairi wanapokua wawili tu? Mazungumzo huendaje?

Sasa turudi kwenye kazi hiyo ya kuanza kuifanya baada ya kuipata sasa WCB, ukiachana na msoto mrefu alopitia, WCB wenyewe walikua waangalifu sana kwenye mipango ambayo ilikua ikiandaliwa kwaajili yake, yeye ndo msanii wa KWANZA wa KIKE kuwahi kutokea kwenye label kwahiyo ukichana na kipaji pia uwekezaji wa hali ya juu ulitakiwa ufanyike and boy they did that. Toka single yake ya kwanza mpaka wakati naandika hii Zuchu hakuwahi kuwa na kazi chafu, album yake ya kwanza alotoka nayo ya I am Zuchu ilikua na nyimbo 7 ambazo zote zilienda kufanya vizuri, na mpaka leo kila wimbo ambao anaachia ni wa moto, tukisema namba moja nadhani namba zake pia zinasema hivyo za kila sehemu, hakuna chumvi yoyote ndani yake.

Vipi sasa anaweza ku maintain hii schedule yake ilojaa mambo kuanzia asubuhi mpaka usiku? Kutoka Jumatatu mpaka Jumapili? Je ana muda kwaajili yake? Ana mpenzi? Mipango yake je? Endelevu? Vipi hizi title ambazo tunampa anazichukuliaje? Kuna pressure yoyote? Na kuhusu familia je? Kuna pressure yoyote kwenye baadhi ya mambo na maamuzi? Na kwenye label nako? Watu na furaha na kazi yake?

Kwa kuanzia msimu wetu wa TANO nadhani introduction ya Ms Zuchu inatufaa sana na yangu matumaini uta enjoy pia.

Asante kwa support ya toka siku ya kwanza ulipoanza kutupa macho na masikio yako.

You’re the best, nakukumbusha tu kwamba mengi yajayo yatakufurahisha In Shaa Allah maana kazi ndo kwaanza imeanza.

Love,

Salama

Jun 16, 202255:55
Ep. 55 - Salama Na PROFESA | MAPINDUZI HALISI

Ep. 55 - Salama Na PROFESA | MAPINDUZI HALISI

SALAMA NA PROF JAY

Feb 25, 202101:27:20
Ep. 54 - Salama Na VANNY BOY | NDAGHA

Ep. 54 - Salama Na VANNY BOY | NDAGHA

Kutoka kwao Mbeya mpaka Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta maisha bora na maendeleo kama wengi wetu ndo ilikua nia na madhumuni ya Raymond wa enzi hizo. Ingawa kuna kipindi ilifika alikua hataki kabisa kuskia habari za muziki, ila alipoambia kama kuna pesa ndani yake katika huo mchongo wa mashindano ambayo aliitiwa na akiangalia nyumbani moja haikai na mbili haijulikani ilipo akaona basi sawa, kwani nini? Na huo ndo ulikua mwanzo wa safari nzuri ya ki superstar ambayo anaishi nayo sasa.

Najua wengi wenu mlikua mnadhani labda yangezungumziwa madhila alokua nayo sasa ila kwa bahati mbaya (kwako) na nzuri kwetu, sisi tulizungumza naye kabla. So hii ilikua free na natural kama ambayo utaiona au kuiskiliza. Wengi wetu huwa tunapitia madhila na mitihani mingi tu kabla ya kujielewa na kusimama sawa sawa, na kupitia hayo ndo kujifunza na kuwa BORA kunatokea. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaoenda kama, ‘asipo chafuka, atajifunzaje’, something like that.

Mimi Ray huyu nilianza kumsikia vizuri zaidi kutoka kwa AY ambaye ali spend naye muda mwingi hapa Bongo wakati wanafanya rekodi remix ya Zigo na nchini Afrika ya Kusini wakati Zee ameenda ku shoot video ya wimbo huo ambao Diamond Platnumz ndo ameshirikishwa, ila Vanny Boy alikuwepo all the way na mpaka kwenye video akatokea. AY aliniambia kuhusu ucheshi wake na uhodari wake, na uhodari huo ameuzungumza humu kwenye maongezi yetu mimi na yeye. Aliniambia jinsi ambavyo alikua akitumia kipaji chake enzi hizo kwa kuwaandikia wenzake wimbo mmoja na pengine mpaka album kwa shilingi ELFU THELATHINI TU.

Njia ambazo watu wengi wamepita haiwezi kuwa ndo njia ambayo kila mmoja wetu atapitia pia, ila kunaweza kuwa na mifanano ya hapa na pale, na hii ndo nia na madhumuni ya kipindi hiki. Tunataka wewe usikie na ujifunze ili ujue ‘unatokaje’ au watu walipenya vipi mpaka wakafika!

Sasa ni mmoja ya wasanii wakubwa tu hapa barani Afrika na duniani anafahamika. Bango la album yake linaning’inia kwenye mitaa ya Times Square huko NY City kwenye mji ambao raia wa nchi mbalimbali duniani wanaishi na kupitia. Sidhani kama wakati anahangaikia kufua nguo zake zilizomwagikiwa mafuta ya mawese wakati akiwa safarini kwenye lori kutoka Mbeya kuja Dar aliwahi kuwaza jambo kama hilo.

Mimi na yeye tulizungumzia pia mahusiano yake na wazazi wake, familia ya kufikia ya Baba yake ambaye aliachana na Mama yake na kuhamia na mtu mwengine si mbali na wao walipokua wanakaa. Tumeongelea mapenzi yake na muziki na kipaji chake cha uandishi. Tumeongelea jinsi ambavyo Madee alimpokea na Babu Tale ambavyo alikua na kama kusita hivi kwenye suala la yeye kusajiliwa WCB na mambo mengine mengi ya maisha. Yangu matumaini kama ilivyo ada, hapa utajifunza jambo pia.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Feb 18, 202101:14:32
Ep. 53 - Salama Na NANDY | MNOGESHAJI

Ep. 53 - Salama Na NANDY | MNOGESHAJI

Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu amable nafahamiana naye sana, ambaye nishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndo ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua.

Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, kipindi hiko kilikua cha masikitiko kwao na kwake pia. Nandy alikua na ukaribu mwingi na Ruge, alishawahi kumtembelea hospitali mara kadhaa na pia alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa karibu wa familia kipindi kile ambacho Ruge alikua hana tena mawasiliano naye moja kwa moja. Siku ambayo Ruge alitangulia muelle ya haki, muda si mrefu kabla ya hilo halijatokea Nandy ananiambia alizungumza na nesi wa zamu siku hiyo na pia alimuekea simu kwa ukaribu na alimsikia akiwa anapumua. Wapi alikua wakati anapata habari hii iko kwenye maongezi yetu haya, humu pia utaelewa connection ambayo sisi binadamu tunayo na watu ambao tunawapenda na wanao wanatupenda.

Najua siku hazigandi kama ambavyo Lady Jd alishawahi kuimba na ndo  nikawaza, hivi ushawahi kuwaza Nandy amekua kiasi gani toka msiba wa Ruge utokee? Unakumbuka baadhi ya maneno yalosemwa juu ya career yake baada ya msiba ule? Tunafahamu kwamba alipoteza rafiki, mentor, baba na kama tochi yake? Mimi huwaza haya sana, na hilo la yeye kujidhatiti na kukaza mwendo ndo ambalo lilifanya mimi binafsi niseme you know what, it’s time.

Nandy ni MPAMBANAJI, anaupenda muziki na kama mtu mwengine yoyote mwenye jitihada basi Mungu humfungulia milango ya Kheri. Kaniambia humu kwenye mangezi yetu kwamba safari yake ya kwanza kwenda nchini Nigeria kwenye mashindano ya kuimba alimuambia Mama yake wakati yumo ndani ya ndege, alipomaliza hutuba yake fupi alizima simu na wheels up, to Lagos ambako alihakikisha anapigana mpaka fainali na kumaliza nafasi ya tatu. Si kitu kidogo kwa binti ambaye aliamua kuweka shule pembeni ili atimize ndoto yake, ndoto ambayo hata Mama yake mzazi hakua na taarifa nayo.

Siku zinakwenda, maisha yanasonga na yeye ameendelea kukimbiza ndoto yake na mpaka tunaenda mitamboni, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wakubwa sana hapa nyumbani na barani Afrika na hata Ulaya na Marekani na ukitizama vizuri utajua kwamba huu ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yatatokea katika maisha yake. Mimi na yeye tulizungumzia mahusiano hayo pamoja na kukimbiza ndoto zetu. Tuliongelea Bill Nas na kiwanda cha muziki wa Bongo Flava. Tuliongelea muziki wake na collabo ambazo amewahi kufanya. Hapo hapo nilitaka kujua pia yeye ni mtu wa aina gani na ni vitu gani vinamsukuma kutaka atake zaidi na sehemu ambayo anajiona huko mbeleni In Shaa Allah.

Yangu matumaini kama kawaida ni kwamba utajifunza mawili matatu ambayo yatakusaidia kupambana na mitihani ya maisha kwasababu tu umejifunza kutokana na sehemu wenzetu hupitia kwenye maisha yao.

Tafadhali Enjoy.

Love,

Salama.

Feb 11, 202101:04:04
Ep. 52 - Salama Na HAJI | ALIYE KUTWIKA NDIYE ATAKAYEKUTUA

Ep. 52 - Salama Na HAJI | ALIYE KUTWIKA NDIYE ATAKAYEKUTUA

Haji Sunday Manara nlitaka kusema ni rafiki YANGU ila vacati navaza hilo nikakumbuka mmh, Haji Sunday Manara ni rafiki wa WATU WENGI hususan mashabiki wa klabu wangu pendwa na zaidi kwa watu ambao hawapendi hata mpira ila wanampenda tu jinsi anavyoseti mambo yake na anavyoigeuza sehemu yoyote aendayo kama sehemu yake ya kujitamba na kujitutumua na tofauti yake na WACHACHE ambao wanafanya kazi kama yake ni kwamba yeye anaweza KUYATEMBEA yale anayo YAONGEA.

Mapenzi yangu kwake ni ya first class na namini hata yeye analifahamu hilo, huwa namtazama kwa kuvutiwa hasa kwababu ya anavyojibeba na kukiaminisha kile ambacho anakisema, iwe kuhusu Simba, bidhaa ambayo anaitangaza au hata simulizi za maisha , vyovyote vile vitakufanya utake kumskiliza kwa umakini, na pia ni lazima ucheke. Utashi wake kwenye mambo mengi pia ni jambo la kupendeza, ukiniuliza mimi nitakuambia sawa, hata kama ni mtoto wa Kariakoo, ni watoto wa Kariakoo wangapi ambao wewe unawajua wana kipaji cha kuongea na kumfanya mtu ajiskie kama ambavyo Haji anafanya baadhi ya watu wajiskie? Iwe kwa kuzodoa au kusifia wangapi? Maneno ya papo kwa papo au hata ya kujindaa (hapo ndo utachoka kabisa), yupi?

Urafiki wetu ulianzia pale kwenye USIMBA DAMU na tuli click tu moja kwa moja, niliamini timu wangu ido kwenye mikono salama kabisa kama jina langu, tufungwe atasema maneno ya kutufanya tunyoshe mgongo na kusimama vuzuri na tukishinda well tukishinda mziki unaufahamu vizuri tu, na tukisajili je? Ahaha… Huyu mtu huya ananipa raha sana, Nba hiyo neo ilikua sababu ya Mimi na wenzangu kumvuta kitini.

Maneno mengi yamekua yakisemwa juu yake na pia mdomo wake huo ulishawahi kumtia matatani kipindi flani kile ambacho Bwana Mo Dewji alipopata matataizo, si unakumbuka? Haji alitiwa ndani siku kadhaa mpaka alipokuja kuwa cleared kwamba hakua anahusika, sikuongea nae kuhusu hilo kwasababu tu za kutotaka asiwe comfy kwenye kiti chetu ( ingawa najua ningeuliza asingekua na hiyana hata). Maneno mengine ni kuhusu urafiki wake na matajiri wa mjini ambao wengine ni wamiliki wa time pinzani za muajiri wake, hili likoje? Huwa anasumbuka wananchi wanapolileta kwenye comments za ukurasa wake maarufu wa Intagram?

Mzaliwa wa Udachini kule nchini Holland, Haji amekua hapa Dar es Salaam kwa malezi ya Bibi na Babu zake maana kipindi hicho Mzee wake alikua anakipiga nje zaidi, mimi nilitaka kujua hiyo historia yake na mpira na Mzee wake, Yanga (ambayo tunaweza kusema ni team ya familia), elimu yake na mambo ya ndoa na scandal za mitandaoni za hapa na pale. Pia tuliongelea pale alipokua wakati shabiki wa Simba Bwana Hamisi Kingwangalla alipohoji uwekezaji wa Mo Dewji na bilioni 20 za uwekezaji, na mano yake hasa kuhusu hiyo situation.

Nimecheka sana, nimeskiliza sana, nime admire sana na zaidi nimejifunza mengi ambayo nilikua siyafahamu kuhusu mtu huyo maalum na tunu ya Taifa hili. Yangu matumani utaelewa na kujifunza jambo hapa.
Tafadhaki enjoy rafiki.

Love,
Salama.

Feb 04, 202101:23:44
Ep. 51 - Salama Na Babu Tale | JUGGLER

Ep. 51 - Salama Na Babu Tale | JUGGLER

Hamis Tale Tale ni MWAMBA wa maisha yake na ya wale walomzunguka kwa miaka nenda miaka rudi na kutoka upande huu wa muandishi na mtangazaji ni heshima tu kwenda mbele. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili kuhusu nyani ambaye unamkuta mjini. Ya kwamba anakua kashakwepa MISHALE ya kutosha kwahiyo unapomkuta town inabidi umpe heshima zake za kutosha.

Kwa waasisi wa Bongo Flava jina lake kuwa juu pale na haiwezi kuwa kosa hata kidogo na kuna wasanii kibao ambao wana mshutumu kwa mambo mengi lakini kuna wale ambao hawawezi kumsahau maishani mwao kwa sababu ya mchango mkubwa ambao amewapa. Na vile vile ukimtaka mtu wa kukuelezea tabia na uzuri wa watu wa iaina zote katika industry hii basi Babu Tale ndo ambaye atakuelezea hilo kwa kinaga ubaga maana akiachana na ucheshi wake, Tale pia ni msimuliaji habari mzuri tu.

So kuanzia kwa Marehemu Kaka yake Abdu Bonge mpaka kwa huyu anayevaa kaunda suti zilizonyooka ndo sisi tulipopataka, ametoka umbali gani? Haya yote aliyonayo ilikua ndo mipango yake? Ki ukweli mmoja kama anaamini ya kuwa kuna yatu wanakua wamekaa tu wanaangalia progress zeta kwa mbali na kuona haswa umbali gani watu wametembea mpaka kufika kwa mfano ambapo Tale amefika basi bila ya shaka atakua ametia nne yake huku akiwa kapendeza sana na kumpigia makofi tu kwa yale aliyoweza kuyafikia mpaka sasa. Ukichukulia huyu ni Kijana ambaye kuna wakati flani katika maisha yake ilikua inabidi asubiriane na mmoja ya ndugu zake ili waweze kubadilishana aidha viatu au uniform ili na yeye aweze kwenda shule!

Nimekutana na watu wengi  katika maisha yangu na Tale yeye yake tabia ni kutokua na breki pale anapokua na lake, yale mambo ya sijui kulainisha maneno ili pengine asikuumize hisia zako yeye hana, kinda like me, la kusemwa lisemwe kisha maisha yaendelee, na hiyo ni kwa kumtakia mtu mema tu, pia anachekesha na anapenda kucheka pia, also… Mkali, sio wa ‘kulealea’, sio babysitter hata kidogo na hiyo yote ni kwa kutaka JEMA kwa mtu ambaye anamsimamia. Najua kama binadamu atakua na mapungufu yake na hayo ndo yako pia kwenye maneno ya baadhi ya wasanii ambao ameshawahi kufanya nao kazi.

Tale ana khadithi ya kila mmoja wetu kwenye kiwanda hiki cha muziki na burudani na nna uhakika miaka kadhaa ya mbele atakua na khadithi za wanasiasa wenzake na viongozi ambao kuanzika mwaka huu anaanza kuwa nao kwa muda mrefu kwenye maisha yake.

Mwaka jana Babu Tale alimpoteza mke wake kipenzi ambaye alitangulia mbele ya haki na kumuachia watoto ambao sasa yeye ndo anaye waangalia kwa msaada pia wa baadhi ya ndugu zake. Hii ilikua habari nzito kwa kila mtu, mke wake amble wengi tulikua tunamfahamu zaidi kupitia mitandano ya kijamii, mimi nishawahi kukutana naye mara kadhaa, alikua Mrembo sana wa sura na roho, Mwenyezi Mungu Amrehemu. Mengi sana yalisemwa na kwa ufahamu wangu nikaona basi hakuna wa kutuambia ambayo tunadhani tuna haki ya kuyajua zaidi yake YEYE. Nini haswa kilitokea?

Natumai maongezi yetu haya yatakupa somo flani kwa mambo kadhaa ambayo tunakutana nayo maishani mwetu, Tale amanitajia watu ambao kwa kiasi kikubwa wanamsaidia kumpa faraja baada ya mkewe kutangulia mbele ya haki, na watu hao hata sio NDUGU ZAKE, ingawa najua nao kwa kiasi chao wanamsaidia ki vyao. Hili kwangu liliingia haswa.

Humu kuna mengi tuliyagusia na hakua na hiyana kutuambia mawazo yake na kwa hilo napenda kumshukuru. Tafadhali enjoy session hii ambayo kama kawaida natumai itakufunza mambo mawili matatu, iwe kuhusu mapenzi, maisha, kazi, watoto, muziki, marafiki na hata siasa, Na pengene hata jinsi ya kukimbiza naoto zako!

Love,
Salama

Jan 30, 202101:16:40
Ep. 50 - Salama Na SUGU | UJIO WA UMRI

Ep. 50 - Salama Na SUGU | UJIO WA UMRI

Turudi nyuma mwaka 1999 wakati nilipomaliza kidato cha nne kwahiyo nilikua sina mitkasi mingi zaidi ya kumkimbia Mama inapofika mchana ili niende kucheza zangu basketball pale Msasani kiwanja cha Pazi. Nlikua natokea zangu Mbagala Charambe nachukua zangu basi mappa Mbagala Rangi tatu then muunganisho unaendelea mpaka nafika zangu mazoezini, nilifanya urafiki na makonda na madereva weeengi kiasi kwamba nilikua ‘staff’ kwenye daladala nyingi, na huwezi kuamini nyingi pia nilikua nikiingia basi radio nlikua namiliki MIMI. Station gani tunaskiliza au tape gani tunaweka ili safari inoge na muziki. Nakumbuka jinsi ambavyo Sugu alikua anaikosha, anakosha nafsi yangu na ya abiria wote ambao walikua wanasafiri nasi basi moja. Chini ya miaka 18 ilikua inaongea na mimi haswam inanifanya nisitake kuwa yule binti ambale Sugu alikua namuongelea ASILAN! Mikononi mwa Polisi… Album kali kama Nje ya Bongo, Millenium, Muziki na Maisha zilifuata na wakati hizi nyengine zinatoka nami tayari nilishaacha kumtia wasiwasi Mama yangu wa kurudi nyumbani usiku na kuwa DJ wa muda ndani ya Daladala za Mbagala Posta au Mbagala Kariakoo na kuweza kupata kazi yangu ya kwanza pale Times FM kabla sijajiunga na EA Radio na TV.

Mapenzi yangu kwa Sugu na muziki wake yako wazi na naamini na yeye anajua maana huwa namuambia kila tunapokutana, pia napenda kuwa around na yeye maana confidence yake ni kitu cha kujifunza. Haogopi, anajiamini na uthubutu wake katika mambo yake mengi ni jambo ambalo wengi wetu tunajifunza sana kutoka kwake. Kuanzia jinsi alivyokua anajibeba, mapinduzi ya uandishi na muziki ambayo amefanya na anaendelea kufanya mpaka leo hii ni kitu ambacho kama utakua unamfuatilia kwa karibu basi utakua huna la kufanya zaidi ya kupenda jinsi anavyofanya mambo yake.

Siku zote nimekua nikitaka saaana kufanya nae interview lakini kama tujuavyo, Mungu ndo mpangaji wa yote na round hii ilikua ndo wakati muafaka. Nilimcheki naye akakiambia kwamba Mimi ni mtu pekee ambaye angependa aongee naye so mengine yakawa historia tu.

Brother alikuja Dar es Salaam malum kabisa kwaajili ya kuongea na sisi na kwa hilo tunamshkuru sana. Mambo ya kisiasa yalikua sio focus yetu hata kidogo na badala yake tulitaka kumfahamu yeye zaidi na pengine mmoja anaweza kujifunza kwa kufuatilia tu nyenendo zake kwenye mitandao.

Kaka alishawahi kwenda jela, amempoteza Mama yake kipenzi pia muda si mrefu baada ya yeye kutoka. Sisi tuliongea naye kuhusu mapenzi yake na Mama yake kipenzi Desderia ambaye hata jina la hoteli yake ameipa jina la Mama yake. Nilitaka kujua ukaribu wao huo ulitokana na nini, jinsi ambavyo Mama alimpa support kipindi hicho ambacho muziki ulikua unaonekana kama uhuni tu. Maoni yake kwenye masuala mbali mbali na kuhusu urafiki na mafanikio. Pia nilitaka kujua historia yake ya muziki na njia alizowahi kupita. Mambo mengine ni kuhusu suala la yeye kuwa Baba na mapenzi kwa ujumla.

Yangu matumaini una enjoy maongezi haya na Kaka mkubwa na pia confidence yake kwenye masala mbalimbali itakufanya pia ujibebe kuelekea mbele!

Tafadhali enjoy.

Love,
Salama

Jan 21, 202101:10:30
Ep. 49 - Salama Na MAVOKO | WINGMAN

Ep. 49 - Salama Na MAVOKO | WINGMAN

Kwa muda mrefu nimekua nikitaka kuongea na Mavoko ila ratiba zetu zilikua hazijawahi kuwa sawa na hivyo tukawa tunapishana tu. Kama mimi sina program naye basi yeye atakua free, na mimi nikiwa free basi yeye atakua na mipango ya kutoa kazi mpya ambayo itanifanya ningoje ili viende pamoja, au atakua kasafiri, au mimi nitakua nishaset watu wengine, ilikua kama tunacheza kidali po ila katikati ya mwezi wa kumi na mbili hatimaye yakatimia.

Hakuna doubt juu ya uwezo wake popote pale utakapoenda ingawa baada ya yeye kuamua kuondoka kwenye label ya WCB kulikua na mengi yalosemwa na kutendwa na baadhi ya mashabiki yalikua yanaweza kukuaminisha jambo na mpaka kufikia pengine ku doubt huo uwezo wake. Mambo mengi yalisemwa, ya kusikitisha, ndoa haikuvunjika vizuri ila ambacho nilikiona kwake ni ustaarabu wa hali ya juu, wa kuwaacha walimwengu waseme na kufanya watakayo huku yeye akiwa ame focus kwenye kipaji chake na kujipanga upya.

Moto wa Mama Richard anaujua mziki mwingi, ana uwezo mkubwa wa kuimba na kuandika na kucheza pia, ila kabla hajaingia kwenye label alikua anajulikana tu, ila kumfahamu vizuri na kuthamini kipaji chake kulikuja baada ya yeye kushirikiana na mmoja kama si msanii bora zaidi kuwahi kutokea na kuipeperusha zaidi bendera ya Tanzania ndani ya Diamond Platnumz. Ushirikiano wao ulitupa ‘anthem’ kadhaa ambazo mpaka leo ukiziskiliza hazichuji. Ilikua kama team ya wenye vipaji pekee, kama ni mfuatiliaji wa mpira wa kikapu hii tunaweza kuifananisha na ile zile team mbili za Mashariki na Magharibi ambazo zinakusanya wachezaji wenye uwezo wahali ya juu.

Saasa, ikawaje hasa mpaka akaona aachane na all star hiyo na kupeleka team yake uwanjani akiwa solo? Nini hasa kilifanya mpaka afikie maamuzi hayo? Kuna mtu  au kitu kilimshinikiza? Je yalikua maamuzi sahihi? Pia kuna masuala binafsi ya kifamilia na suala la yeye kutomfahamu Baba yake takati anakua, elimu yeke, ndugu zake, Mama yake na muziki ulichomfanyia katika maisha yake.

Mavoko huyu ambaye mimi namfahamu nilikutana naye Kampala, Uganda kama maka saba iliyopita na mazungumzo yetu yalikua yanahusu kipaji chake na jinsi ambavyo nilikua naona ‘hapewi’ nafasi maana kama ngoma zake zilikua nzuri tu, video ndo usiseme ila hakuna na spotlight aliyokua anastahili, peleka mbele miaka mpaka 2021 ambapo alipata nafasi kwa miaka takriban miwili na nusu kufanya kazi na lebo bora zaidi ila baada ya muda akaamua kubwaga? Kwanini hasa? Sote tunajua kama nyasi za jirani huonekana zimestawi kweli kweli ila ukifika na kuziona kwa ukaribu utaelewa kwamba si kila kitu kina fanana na kionekanavyo.  Ila mpaka kuamua kukusanya na mabegi na kuondoka kwenye ‘jumba kali’?

Majubu yake yalikua ya moja kwa moja tu na nafsi yake ilikua tayari kuhamia nyumba nyengine mwenzangu. Natumai kwa kiasi flani utasoma jambo, ingawa kwangu mimi natamani ningepata zaidi na zaidi ila inaonekana bado hakua tayari kutufungukia mazima. Binafsi namshkuru kwa kuja mezani kwetu na pengine tutaweza kukutana tena mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini bado utaokota mawili matatu.

Love,

Salama.

Jan 14, 202101:05:30
Ep. 48 - Salama Na JK | MSOGA UNO

Ep. 48 - Salama Na JK | MSOGA UNO

Muda si mrefu iliopita nilirudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu ya mawasiliano ya kwanza kabisa kati yangu na moja wa wasaidizi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho wa Kikwete na hiyo ilinirudisha nyuma mpaka mwezi wa tatu mwaka 2020. Kama mtu mwengine yoyote hii ilikua ndoto tu ambayo kwa Rehema na Baraka za Allah ilibidi itimie. Kwa Baraka zake hizo mimi na wenzangu tunashkuru sana sana kwa kuweza kulikamilisha hili.

Shukran za dhati ziende kwa Doris Mollel ambaye kwa msaada wa Sadam ‘Almando’ Sanare alinimbia Doris anaweza akatu unganisha na mmoja wa wasaidizi wake ili tuweze kuona kama tunaweza pata hii nafasi, na kama ujuavyo, mengine yote yamebaki kuwa historia tu tena, maana yametimia.

Mimi kama wewe tu, shabiki nambari moja wa Jakaya Mrisho Kikwete na kukutana naye, kukaa naye chini na kuweza kumuuliza maswali tuliyokua tumeyaandaa (kwa muongozo wao) ilikua raha isiyoelezeka. Mzee charming, mwenye roho nzuri na muelewa kabisa. Mengine yalofuata baada ya hapo ndo ambayo utayaona au kuyaskiliza katika maongezi yetu haya. Mengi yalikua ni juu ya yeye alivyokua na uelewa wake kwenye mambo mengi. I wish tungeweza kuongea nae kuhusu masuala meeengi zaidi kuhusu kiila kitu ila ki ukweli hii inatosha kwa sasa na Mungu atajaalia tutakutana naye tena siku nyengine In Shaa Allah.

Mheshimiwa JK aliongea nasi kuhusu Wazazi wake, elimu, uelewa wake wa mambo, yeye kuwa mwanajeshi. Jinsi alivyokutana na Mama Salma. Historia ya nyuma kidogo kuhusu mapenzi na jinsi Marehemu Mzee wake alivyomtaftia mke na kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza ambaye ni Ridhwan. Kuhusu kitabu chake, mapenzi yake na basketball na muziki. Pia Kobe Bryant na mapenzi kwa wajukuu zake.

Kama ilivyo kawaida yetu, yangu matumaini utapata kadhaa humu ya kukufunza jambo. Na napenda kuchukua nafasi hii kumshkuru kila mtu ambaye alisaidia hilo kutimia na zaidi team yangu yote ya ‘YahStoneTown’ ambayo ilifanya kazi iliyotukuka kukamilisha hili.

Nikutakie Kheri ya mwaka mpya na kila lenye Kheri nawe.
Enjoy.

Love,
Salama.

Jan 07, 202101:01:48
Ep. 47 - Salama Na JOTI | SIMPLY SPECIAL

Ep. 47 - Salama Na JOTI | SIMPLY SPECIAL

Lucas Mhaville ni maalum sana, kwa ki vyovyote vile utakakavyotaka wewe, ki maisha, ki muonekano, ki uelewa na jinsi anavyokua mpya kila siku kwenye ulimwengu wake, jinsi anavyo jipa matawi na kujigawa kisanaa. Jinsi anavyotoa character wapya kila mara kwaajili tu ya kuleta ladha mpya kwenye sanaa yake, hili linamfanya aendelee kuwa mchekeshaji pekee kwenye kizazi chetu ambaye huwezi kuona amechuja au hana jipya kwenye kukufurahisha wewe.

Kabla sijaiandika hii, kipande kidogo cha video kilienda kwenye ukurasa wangu wa Instagram (@ecejay) kwaajili ya kuwafahamisha watu kwamba JOTI atakua ndo mgeni wetu wa usiku wa leo, na kwenye hiyo video nilimuuliza kuhusu kabila lake ambalo kwa mujibu wake ni kabila dogo tu kutoka huko Morogoro na yeye na Baba yake mdogo ambaye ni Polisi ndo watu waarufu zaidi, ila kwa wingi wa replies kutoka kwa watu wengi wa kabila hilo inaonyesha si kabila dogo kama yeye alivyodhani, ila hiyo ni tisa, kumi ni jinsi ambayo watu WANAMPENDA na kusikiliza KILA ANACHOSEMA, hiko ni kipawa tofauti kabisa, sio kila mtu anaweza kuwa na uwezo huo.

Yeye ni mzaliwa wa Morogoro na alikuja Dar es Salaam baada ya mzazi wake mmoja kufariki, alichukuliwa na ndugu yake na kuja kulelewa hapa, amesoma hapa na sanaa yake pia ilianzia hapa alipokua shuleni. Nani alimsukuma? Na je alisoma mpaka daraja lipi? Mimi na yeye pia tunazungumzia umuhimu wa elimu na malezi bora. Maisha yake alipokua mdogo na mafunzo aliyoyapata growing up.

Joti si wa leo, akiwa na miaka yake 38 anajielewa vizuri sana tu. Maongezi yetu pia yalitupeleka kwa uanzishwaji wa kundi la Original Comedy ambalo lilitufanya sote tuwapende sana na enzi hizo za EATV wao wanapokua hewani basi nchi nzima ilikua inasimama kwaajili ya kuangalia walichotuandalia. Yalikua mafanikio haswa! So nini kilitokea mpaka wakaomdoka EATV? Na wao kama kundi kuna lolote kwa sasa? Au kila mtu ndo solo? Na vipi kuhusu Vengu? Yule mwenzao (mwenzetu) ambaye alipata matatizo makubwa ya ki afya na mpaka naandika hii bado yuko kitandani? Shida yake hasa ni nini? Haina tiba?

Humu pia tumeongelea mahusiano yake na Seki, ambaye alikua naye toka enzi za OC akiwa kama kiongozi na mtayarishaji. Mahusiano yake na Mpoki, Masanja ambaye sasa amejikita kwenye masuala ya ki kanisa, Wa Kuvanga na McRegan? Wako wapi? Kama kuna comeback ya kundi? Lini?

Wakati nafanya hii pia nilitiwa elimu na Director wangu wa siku hiyo (Ms Lydia Igarabuza) kwamba, ukitaka kuongea na mchekeshaji, ili upate utakacho, basi usimpe nafasi ya yeye kukuchekesha mpaka ukasahau kilichomleta pale, namshkuru sana kwa hilo maana nadhani ki kawaida kama wana tungecheka zaidi kabla ya kuyasikia yote ambayo tumeongea humu.
Respect nyingi ziende kwa Joti ambaye ameweza ku maintain status yake ya heshima ya juu kwenye kazi yake, na kama binadamu.

Yangu matumaini utaokota mawili matatu hapa ambayo yatazidi kukutia mafuta ya kukufanya utake maendeleo zaidi na heshima kwenye jina lako na maisha yako.
Tafadhali enjoy.

Love,
Salama

Dec 24, 202001:19:35
Ep. 46 - Salama Na HK | NJE YA BOX KIDDOGO

Ep. 46 - Salama Na HK | NJE YA BOX KIDDOGO

Sikuwahi kuujua ufahamu wa Dr Hamisi Kingwangala kwenye suala la dini kwa kiasi ambacho ameniambia wakati tunaongea kwenye kikao chetu hiki, na alinilelezea kwa majina yake ya kizuoni huku akiniambia nini kwa binafsi yake anaweza kukifanya kwa kituo pale anapotaka, lakini pia aliniambia juu ya suala la yeye kutokua anaswali sala tano kama ilivyokua zamani na kwamba si jambo analojivunia asilan!

Hii ilikua mara yangu ya pili kukutana na kuongea nae kwa kituo, kama ilivyokua kwa Taji nae pia niliongea naye miaka ya nyuma wakati nafanya Mkasi, na kwa kuongea naye round hii nimejifunza kwamba hawa ni kama watu wawili tofauti kabisa na si kwa ubaya, yule wa kwanza alikua si muongeaji kama huyo wa sasa  kwasababu amekua kwa kiasi flani na kukua ni jambo ambalo sisi wenyewe na wazazi wetu huangalia kwa makini kuanzia pale ulipokua tuseme miaka mitano iliyopita na sasa na mipango na maratajio yako. Kwa hili Sheikh HK kaserebuka nalo vizuri tu. Hakuna mtu asiyemfahamu Hamis Kingwangala ndani ya nchi hii na nje, jinsi ambavyo alifanya kazi nzuri ya kampeni ya kuitangaza Tanzania duniani kwa umaarufu wa vivutio vya utalii wetu na utajiri wa nchi yetu pendwa. Alichukua muda huo pia kutembelea karibu mbuga zote na nchi hii na wakati huo huo kupambana na majangili na waharibifu wa wanyama pori, vita ambayo ilikua ndo stori ya kipindi flani hapo nyuma. Yeye HK alikua anamalizana na maneno ya walimwengu ambao walikua wanaongea mengi kwenye mitandano ni kwa  yeye. kuendelea kupiga  kazi yake vizuri tu mpaka akamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais aliyempa cheo hicho kwa usalama tu, nasema hivyo kwasababu kuna wengi ambao walikua wanateuliwa lakini siku zao za kukaa ofisini hazikua nyingi sana ila HK aliweza kuendana vizuri na mawimbi kwenye bahari ya uongozi ambayo bila ya shaka ilikua na mitihani yake.

Pia umaarufu wake mwengine Bwana HK ulikuja baada ya kuwa ntumiaji mzuri sana wa Twitter, sehemu ambayo huitumia kwa kufanyia kazi yake ya kuitangaza nchi na pia kumalizana na ‘wabaya’ wake wote ambao wamekua wakila nae sahani moja kila mara panapokua na jambo ambalo yeye amesema au kuwakilisha mooni yake juu ya suala flani. HK hana tabia ya kuona haya kumjibu mtu ambaye kwa namna moja ama nyengine anakua kamgusa pale alipokua hapataki yeye au pengine tofauti tu ya mawazo, muda mwengine utakuta watu wamefika huko.

Kubwa kuliko ilikua hii ya mwaka huu ambayo alihoji juu ya uteuzi wa CEO mpya wa klabu yake pendwa ya Simba na pia suala la mwekezaji kutimiza ahadi yake ya kuipa Simba shilingi bilioni 20 za kuendeleza klabu. Hili suala liliamsha zogo kubwa kati ya HK, muekezaji wa klabu pamoja na mashabiki wa Simba, lilifanya pia tujue siri za ndani za kibiashara kati ya wawili hawa na jinsi ambayo wote wawili walivyokua wanajibizana mitandano ilifanya watu wengi wanyanyue nyusi kwa mshangao na kujuzwa mambo ambayo pengine yalikua hayana faida kwa watu wengine kujua. Hivi karibuni wawili hawa walimaliza tofauti zao huko huko kwenye mitandao hiyo hiyo ya kijamii kama walivyofanya awali.

Niloitaka kujua kama kuna muendelezo wa hayo maongezi yao, kama walishakutana toka majibizano yale yatokee, pia tuliongelea ajali ambayo aliipata akiwa kazini na ambayo pia ilizungumziwa na watu wengi. Pia niliongea nae kuhusu Rais Magufuli, uchaguzi wa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda  kwa ushindi mnono na jinsi ambavyo hakupata nafasi kwenye baraza la mawaziri na manaibu wake ambalo limeundwa hivi karibuni na ambavyo aliipokea taarifa hiyo.

HK ni mtu poa sana, kijana ambaye ni Kiongozi, Baba, Kaka na mfanyabiasha mzuri tu ndo darasa letu la wiki hii na yangu matumaini kana kawaida atakua na jambo la kukufunza kwahiyo tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

Dec 17, 202001:34:38
Ep. 45 - Salama Na TAJI | TABASAMU LA SWAHIBA

Ep. 45 - Salama Na TAJI | TABASAMU LA SWAHIBA

Pia anafahamkika kama Master T, mwenye sauti yake tamu ya kumfanya mtu abadilishe mawazo na kufanya anachosema yeye, lafdhi nzuri ya maneno ya Kiswahili na Kiingereza na tabasamu zuri kabisa lililokaa mahala pake na hiyo ndo tofauti ya Taji Liundi na watangazaji pamoja na hata viongozi wa department mbali mbali kwenye vyombo vyetu vya habari vya ‘siku hizi’.

Taji alibahatika kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo kwa kiasi chake na malezi bora aliyapata kwa Baba yake ambaye muda mwingi alikua akisafiri nchi mbalimbali kutokana na kazi yake na hii pia ilimfanya ajengeke kwa kiasi flani, kuweza kujiamini, kuongea lunga zaidi ya moja na mapenzi yake na muziki pia yalianzia hapo. Aliniambia katika maongezi yetu haya kwamba kukaa na Marehemu Mzee wake ambaye alikua busy wakati mwingi ndo ulimpa mwanya wa yeye kujifunza mambo mengi ya nje ikiwa ni pamoja na muziki na michezo kama football na basketball. Pia aliniambia alikua mpigaji simu kwenye radio mzuri sana tu, na kwa kiasi flani hiyo ilifanya mapenzi yake na radio yaanzie na aliporudi nyumbani na familia yake alipata msukumo wa kwenda kutafuta kazi kwenye radio.

Kuna tukio pia lilitokea vacati akiwa na umri kama miaka saba au nane ivi, ambalo lilikua linahusiana na wivu wa mapenzi ambao Mama yake alikua nao kwa marehemu Mzee wake na ndo ambalo lilifanya maisha ya Taji yabadilike sana sana. Na hihi simulizi alitupa kwenye kipindi chetu hiki, hii ni tettes ambayo niliiskia mara nyingi tu wakati nakua na kistaarabu kabisa ilibidi nimuulize Kaka yangu kama atakua huru tuizungumzie hapa, na hakua na hiyana kabisa. Tuliongelea jinsi ambavyo Mama yake aliwauwa ndugu zake na jinsi ambavyo yeye aliponea chupuchupum anatuelezea vizuri sana kwenye maogezi yetu haya.

Taji pia alikua boss vanga wa kwanza mimi kama Salama, kazi yangu ya kwanza yeye ndo alinipatia nafasi kwa moyo mmoja kabisa, aliniambia nifanye majaribio ya sauti na kusoma habari flani ya Tennis na mengine baada ya hapo ni history kama wazungu wanavyosema. Kwahiyo pia nilimuuliza kiaina ni nini hasa aliona ndani yangu na kama anaikumbuka hiyo siku, maana binafsi nakumbuka mpaka nilichokua nimekivaa Salama mimi. Maneno pekoe hayawezi kusimulia jinsi ninavyo mshukuru kwa kuniamini na nafasi, Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda, kumpa afya njema na kumtimizia kila takwa la moyo wake In Shaa Alla.

Kwa kumalizia pia mi Kaka yangu tulizungumzia mustakabali wa muziki wetu na  wanamuziki wetu, radio na watangazaji wa kisasa na pia muongozo kwenye masuala ya kazi, Taji pia aliniambia naye ameanza kutimiza ndoto zake kidogo kidogo kwa kutoa single yake ambayo hata mimi nilishtuka kidogo kwa furaha baada ya kuona yuko serious, na sio wimbo tu, ni wimbo MZURI.

Nilienjoy sana kuongea na Taji kwenye kipindi hiki na zaidi nilifurahi kwasababu anakua anapatikana pale unapomhitaj, hii inakuja hata kwako wewe, kama utakua unahitaji ushauri wa masuala ya kazi na hata maisha, Taji hatokosa la kukuambia ambalo litakufanya ujiskie vizuri, na kuzogeza mambo, hilo nakuahidi.
Hii nimeifanya kwaajili yangu na yako na yangu matumaini itakufunza jambo na kukufanya utabasamu.

Love,
Salama.

Dec 11, 202049:06
Ep. 44 - Salama Na MWAKINYO | VITASA OVERLOAD

Ep. 44 - Salama Na MWAKINYO | VITASA OVERLOAD

Hassan Mwakinyo kwa Mama yake ni kama ni kama mkate kwa chai tu, lazima ulainike. Sentensi hii imeanzia hapa baada ya kufuatilia kwa makini na kuambiwa hasa ni kitu gani kinachomfanya Champez atake kuwa bora zaidi na zaidi, na kutaka kupata kile anachokipata kwa nguvu zaidi na zaidi kila siku kila asubuhi anapoenda kukimbia, au kila jioni anapokua gym au anapokua ulingoni, na amini kwamba Mama yake ndo anayemfanya atake kuwa bora siku zote ili aweze kumbadilishia maisha yake kwa uzuri.

Champez Mwakinyo sio moto pekee kwenye familia yao na Kaka yake mkubwa alianza haya mambo ya ngumi kwanza kwa kujiingiza kwenye kick boxing na akawa sio mkali au hodari vile kama ambavyo Mwakinyo amefikia lakini muongozo wake ndo ulomfanya Champez awe hodari kiasi hiki na kuna mpinzani ambale alikua anamsumbua sana kaka yake ila baada ya miaka kadhaa Mwakinyo alimalizana naye vizuri tu na kuweka heshima kwenye familia.

So niliongea na Mwakinyo kuhusu ile fight ambayo ilitufanya sote tumfahamu uzuri, nilitaka kujua alifikaje kule Liverpool na yule mpinzani alimpataje? Vipi na yule jamaa ambaye alibeba headlines zaidi kuliko hata Mwakinyo mwenyewe? Walikutana vipi? Ni kweli alikua anamtaka Kelly Brook? Au yeye mkalimani ndo alikua na ajenda hiyo? Je kuna siku tutaweza kuiona hiyo fight?

Mambo mengi yalitokea wakati Mwakinyo akiwa Uingereza, kulikua na suala la kuchukua pesa na kuacha apigwe kulikua na suala la yeye kupotea kabla ya kwenda kupima uzito. Suala la Mama yeke kupata ajali kabla ya yeye hajaenda England na mambo mengine kibao. Alirudi pia nchini na akapata kudhaminiwa na kampuni moja kubwa ya masuala ya betting, huo mkataba uliishaje? Alipata faida yoyote?

Hivi karibuni alipigana na Jose Carlos Paz kutoka Argentina ili kuweza kutetea ubingwa wake wa WBF kutoka IBA hapa jijini Dar es Salaam, pambano lilikua la kiwangi cha juu, la kimataifa tuseme lila kwenye suala zima la uandaaji na viingilio kama lilileta utata kwa mashabiki zake. Nilimuuliza Mwakinyo kama kile ndo alichokua anataka maana kwa uelewa wangu, boxing ni mchezo wa watu wa chini hapa nyumbani kwetu, je ilikua sawa kwa yeye kukubali viingilio vile? Au inabidi tukubaliane kwamba enzi zimebadilika na kwamba mambo ndo yaka hivyo now?

Nini kinafuata kwake? Nini anataka kwenye maisha yake? Vipi kuhusu mpinzani wa hapa nyumbani ambaye wapenda ngumi wengi ndo wamngependa apigane naye? Maoni yake yepi? Kweli tutaweza kuona hilo pambano? Tulitegemee lini? Jibu lake ndo litakupa muongozo kama tunayoyataka yatakua au la!

Yangu matumaini Champez atakufundisha mambo kadhaa kuhusu heshima, mapenzi, malengo, dini na kujiheshimu na jengine lolote ambalo unaweza ukapata humu. Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.

Dec 03, 202001:02:06