Ifahamu Corona
By Tanzania Development Information Organization (TADIO)
Ifahamu CoronaDec 13, 2021
Episode 6 - Usalama wa Chanjo ya Uviko-19
Maelezo: Kwenye kipindi cha sita cha Ifahamu Corona, tutasikia wataalam wa afya wakielezea usalama wa chanjo ya corona pamoja na waliopatiwa chanjo. Tutawasikia mkurugenzi wa afya ELCT Dr. Paul Mmbando na Dr. Charles Wanga wakielezea chanjo, pia tuawasikia Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi na Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Bukoba Methodius Kilaini pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Karibu
Episode 5 - Chanjo ya Uviko-19
Maelezo: Kwenye kipindi cha tano cha Ifahamu Corona, tutasikia wananchi, viongozi wa dini na wataalam wa afya wakielezea chanjo ya corona. Askofu mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dr. Shoo, Fredrick Shoo, Katibu mkuu wa Baraza la Waislam Tanzania BAKWATA Sheikh Alhaji Nuhu na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) askofu Gervas Nyaisonga watafafanua kuhusu Imani ya dini na chanjo ya corona.
Episode 4 – Dunia baada ya corona
Maelezo: Kwenye kipindi cha nne cha Ifahamu Corona tutasikia matarajio ya wataalmu juu ya athari za virusi vya corona kwa jamii.
Episode 3 – Makundi yaliyo hatarini zaidi na karantini
Maelezo: Kwenye kipindi cha tatu cha Ifahamu Corona tutasikia kundi gani lipo hatarini zaidi kupata virusi vya corona na kuhusu karantini.
Episode 2 – Jinsi ya kuzuia virusi vya corona
Maelezo: Kwenye kipindi cha pili cha Ifahamu Corona tutasikia zaidi kuhusu virusi vya corona.
Episode 1 - Ukweli kuhusu virusi vya corona
Maelezo: Kwenye kipindi cha kwanza cha Ifahamu Corona tutasikia ukweli kuhusu virusi vya corona.